Diamond ameigwa na mnaijeria huyu?

orangutan

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2014
Posts
757
Reaction score
774
Habari wakuu.
Kwa waliopata nafasi ya kucheki video mpya ya msanii wa kike kutoka nigeria Chidinma na wimbo wake wa "Fallen in love" watakubaliana namimi katika hili. Huu wimbo wa bimdada umechukua vikorombwezo na ideas kutoka wimbo wa diamond platinumz "my number one remix".

Kuanzia beat, vionjo mpaka dancing styles zilizopigwa na akina iyobo kwenye ile ngoma ya mondi. Pia video ya mdada imechukua idea aliyoitumia mondi katika shooting ya video ya "nana " aliyomshirikisha diamond (hapa ninamaanisha zile romance za kishuleshule afu wanatoka class wanaanza ku-dance nje).

Ngoma hii ya Chidinma sio siri iko poa na ina-sound fresh kuisikiliza ila kwa asilimia kubwa naona kama huyu bimdada alikuwa motivated kwa kiasi kikubwa na my number one ya mtu mzima chibu(sioni ubaya wowote kuiga vitu vizuri).

Hii inaashiria ni kwa kiasi gani diamond amefanikiwa kupenya ipasavyo pande za west Africa na hii ni ishara njema kuwa sasa mziki kutoka bongo unazidi kupanuka siku baada ya siku. Bravo Diamond Platinumz, Bravo Chidinma!!!

Take your time to watch the video via the link below:
 
Kwa Midungo hapana labda sehemu iyo wanayocheza ngololo may be that! Naona Mondi kakukolea eeh mpaka kisogoni
Sio kwamba namkubali kiviiile. Ila na-appreciate juhudi na ubunifu anaoufanya kwenye music industry
 
Kuna kufanana kwa idea kutoka kwenye nyimbo mbili za Diamond. Number One, kwenye baadhi ya maneno, uchezaji na namna alivyoumalizia wimbo. Kutoka kwenye Nana, ni idea ya mtu kuchelewa darasani/shuleni na kucheza muziki kwenye mazingira ya shule.

Hili ni jambo la kawaida sana katika muziki. Hakuna mwanamuziki yeyote mwenye kitu kipya. Kila idea ilishakuwepo. Hata beef kama za Mondi na Kiba zilishakuwepo kabla. Ni jambo zuri kuona nasi muziki wetu unawafanya wengine wafanye kama wetu.
 
Mbona yeye mwenyewe aliiba hiyo idea Kwa dyna
 
Yeah. Hakuna ubaya wowote kuiga kitu kizuri. Ila sipati picha kibongobongo kiba amwige diamond, hilo povu lake!
 


Hahaha diamond akiigwa ni jambo la kawaida kwa wanamuziki, ila diamond akiiga kitu mnakuja mbio na reference za picha kwamba ame copy kwa flan
 
Ni kweli ameiga hasa hapo kwenye 'wololo', ila beat ni tofauti
 
Ni kweli ameiga baadhi ya sehemu, ila nadhani amefanya hivyo kwa nia nzuri tu ya kuappreciate kazi ya mondi, ila sasa kama mondi ndo angeiga hapa mjini pasingekalika.
sasa hivi nakwambia ingekua madale yote inachezeshwa mnanda[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ila akiigwa wananyamaza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…