Diamond amemliza dyna kwa kumuibia biti la my number 1

ubarinolutu

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2012
Posts
2,424
Reaction score
4,954
Mwanamamuziki dyna mdada ambaye ameonesha juhudi katika mziki wa bongo fleva amejikuta akilia wakati akihojiwa na mtangazaji wa radio 1 ebid, mwanadada huyo alirikodi nyimbo ya demo kwa kutumia biti ambalo alitengenezewa na producer mmoja underground, na katika mwimbo huo ambao alipanga kumshirikisha diamond alikuwa ameshawasiliana na diamond na akawa tayari ameshamtumia na ile demo kwa hyo ilibak tu kuingiza vocal. Matokeo yake diamond alimzungusha na kudai yupo busy , na baadae akaja kusikia katika uzinduzi wa video ya diamond my number 1 ambalo biti hlo lilitokana na melody a mwimbo wake, kwa hyo alichofanya diamond ni kufuata biti na kutengeneza melod ambayo ipo tofauti na original nyimbo ya dyna. Kiukweli ukisikia nyimbo zote mbili utagundua kuwa dyna amelipatia biti kuliko diamond, nawaombeni muzitafute hizo nyimbo zote mbili muone wenyewe diamond alivoiba biti lakini bado hakuweza kufunika kama alivoimba mwenye biti. Dada anadai diamond amemsaliti. Me nimeamini ila ngoja tumsubiri diamond atasemaje
 
Kama ni kweli basi diamonda ana matatizo sana. na huu ni wizi kama wizi mwingine.
Na hili swala siyo mara ya kwanza kumkumba, hata kwenye wimbo wake wa nataka kulewa alilamikiwa na msanii mwenzie.

Diamond haya mambo ataacha lini kama ni kweli? kwa nini anapoteza nguvu nyingi kwa kitu ambacho kina ukakasi namna hii?

Diamond ana matatizo anatakiwa kujirekebisha.
Hivi ni kweli alishindwa kutafuta melody au beat nyingine?
cc heaven on desert
 
Last edited by a moderator:

ndiyo mjuwe hizo habari siyo za kwel dada anatafuta kiki ya kurudi..
afu mleta mada mbona hajasema alichokisema producer ambaye ndo mhusika na alihojiwa.
iko hiv kwa kifupi..
hiyo bit ilitengenezwa toka mwaka jana na producer Dayna akaenda atudio akiwa na lengo la kurecod tena kwa kumshilikisha diamond..na beat hiyo ilikuwepo tayari dayna akapewa kuifanyia demo(sampo)beat hakuipenda akasema ni mbaya wakaachana nayo..coz walikuwa wanapishana na diamond ikashindikana ndo akafanya tu wimbo mwingine na mr blue.
So diamond coz mala kwa mala huenda studio na kurecod nyimbo tofaut tofaut(mashairi hutungia hapo hapo studio akiiskia tu beat na kesharecod nyimbo nying sana kaz yake ni kuziachia tu)
so alipoenda producer akamskilizsha beat ile ambayo kipnd hcho haikuwa na mtu tena.coz dayna aliikata ..diamond akaikubLi kuifanyia wimbo..na kwa uungwana producer alimuita kabisa dayna na kumwambia kama beat huitak bas diamond anataka aitumie dayna akasema hakuna tatizo.kaz ikafanyika
so iweje leo mtu kafanya kitu kizuri unaibuka from no where unananza kulia kwenye media eti umeibiwa?
kwa kisingizio cha demo yake alokwisha ifanya kabla ya kuikataa?
WATU WANAOANZA KUPOTEA KWENYE GEM WANA MATATZO SANA.. WANALAZIMISHAGA HURUMA
 
Last edited by a moderator:

Acha ujinga wewe,kama huyo dada bit hakuipenda why Diamond aibadilishe??why asiitumie kama ilivyo??mwogope mungu na acha kudanganya kijana....wote humu ndani ni watu wazima na hamna mtoto

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Hakuna cha u2 uzma wara nn alkataa b3at wach wajanja wanaojua waishosh3e
 
liambie hilo..linaongea tu mambo ya kusikia...
ishu yote hiyo inatokea me nilikuwepo jitu linabisha bisha kiushabik

leo umejitahidi kuandika vizuri..!
Ila hiyo aina yako ya uandishi kama vile sio ME kamili
 

Mimi muziki siujui na wala sikatai kuwa siujui!
ila hili la wewe kuwa msemaji wa Diamond ,kama kweli ndiye msemaji wake inakupasa sasa uende shule ukasome uandishi!
La haliwezekani,tafuteni mtu awe anafanya hii kazi!
 

Hapo kwenye blue ndio kunaweza kuwa mwisho wa matatizo yote kama kweli hilo lilifanyika? je hilo lilifanyika na kipindi cha wimbo wa "nataka kulewa" ambayo beat inafanana na melody ya wimbo wa pasha?

Pengine nianze kufikiri hapa Tanzania watayarishaji wa nyimbo wana matatizo sana? na nina anza kujiuliza ina maana dyna ni kichaa kuanza kulalamika wakati alikubali mwenyewe?.Hivi Diamond alishapata wasaa wa kumuuliza Dyna kuhusu hiyo beat?

Na kipindi cha maongezi ya Dyna na producer, Diamond alikuwepo au ameambiwa tuu na producer kuwa dyna kakubali?
Hivi kati ya Diamond na producer ni nani alitakiwa kuhakikisha Dyna ametoa baraka kutumika kwa beat yake?
 

beat siyo mari ya msanii.ni mari ya producer in case ulikuwa hujui
 
acha ujinga wewe... hakuna guarantee kwamba beat ni mali ya prodyuza... inategemea na makubaliano aisee coz kama msanii hayuko label na ametoa pesa yake.. it will never happen beat inakua ya producer... itakua ya msanii... coz kalipia.. sijui hii case ya hawa but niko page moja na wewe.. diamond is good siamin kama ni mwizi wa nyimbo.. jamaa ana hit ngap kulinganisha na hizo kashfa za nyimbo mbili. muachen domo jaman
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…