ubarinolutu
JF-Expert Member
- Oct 22, 2012
- 2,424
- 4,954
Mwanamamuziki dyna mdada ambaye ameonesha juhudi katika mziki wa bongo fleva amejikuta akilia wakati akihojiwa na mtangazaji wa radio 1 ebid, mwanadada huyo alirikodi nyimbo ya demo kwa kutumia biti ambalo alitengenezewa na producer mmoja underground, na katika mwimbo huo ambao alipanga kumshirikisha diamond alikuwa ameshawasiliana na diamond na akawa tayari ameshamtumia na ile demo kwa hyo ilibak tu kuingiza vocal. Matokeo yake diamond alimzungusha na kudai yupo busy , na baadae akaja kusikia katika uzinduzi wa video ya diamond my number 1 ambalo biti hlo lilitokana na melody a mwimbo wake, kwa hyo alichofanya diamond ni kufuata biti na kutengeneza melod ambayo ipo tofauti na original nyimbo ya dyna. Kiukweli ukisikia nyimbo zote mbili utagundua kuwa dyna amelipatia biti kuliko diamond, nawaombeni muzitafute hizo nyimbo zote mbili muone wenyewe diamond alivoiba biti lakini bado hakuweza kufunika kama alivoimba mwenye biti. Dada anadai diamond amemsaliti. Me nimeamini ila ngoja tumsubiri diamond atasemaje