Diamond ametengwa na Media Kuu Tatu nchini... Ila Mungu yupo..

Kati ya Diamond na Raia wa Syria nani yupo ktk wakati mgumu unaostahili Mungu kuwa upande wao? Wananchi hasa watoto wa Syria wamemkosea nini Mungu hata wawe jehanamu ya hapahapa duniani? Ungekuwa wewe Mungu ungeweza ungemsaidia nani kwanza?
Wa syria wana tuhusu nini? Sisi wa Africa wanao tutukana kila kukicha wacha wafe au wewe una damu ya Asia. Nenda kawasaidie wa Asia wenzako. Waafrica tuna jipendekeza.
 
Mimi naamini Diamond Platnumz anaweza kustahimili huku kutengwa na media za bongo kwa sababu anajulikana kimataifa na Africa in particular wasiwasi wangu ni hawa watoto wadogo akina Harmonize, Lavalava, Rayvany, Mbosso et al hawa nadhani hajawafikiria ipasavyo, kwa maoni yangu hawa vijana wake bado wanahitaji msaada wa media za Tanzania ili kufika hapo alipo Diamond Platnumz.
Migogoro kati ya msanii na media madhara makubwa huwa yanakuwa kwa msanii na siyo kwa media maana media ina content nyingi sana kiasi kwamba si rahisi kuathirika na kutokucheza nyimbo ya msanii mmoja au wawili, kwa mfano kuna vipindi vya habari, maigizo, michezo, utamaduni, sijui mambo ya mwambao, vipindi vya dini, vipindi vya majadiliano ya kisiasa, uchambuzi wa magazeti etc hizo ni baadhi tu ya contents ambazo utakuta media moja inazo. Rejea bifu la clouds media na Rubby, au na Jide utaona hakukuwa na impact ya moja kwa moja kwa clouds fm

Hivyo basi kunusuru hii hali Diamond aharakishe ujaji wa wasafi TV na wasafifm ili kuwanusuru akina harmonize la sivyo hali yaweza kuwa mbaya upande wake.
 
Amelewa umaarufu dogo..ashawah sema siku hz hategemei media hata youtube inamtosha..kazkaz
Acha kupotosha! How come aseme hategemei "media" wakati bado huwa anafanya media tours na ni juzi kati tu hapa alikuwa Times!

Alichosema ni kwamba hategemei Radio & tv PEKE YAKE!

Hutaki, unaacha lakini huo ndo ukweli wenyewe! Anatumia sana social media na ndio maana mara nyingi kama sio zote, ukimsikia redioni basi anakuwa tayari keshaachia ngoma kitambo YouTube huku akiwa amepiga promo za kutosha Instagram & Twitter
 
Anafanya show za nyumbani mond?
Mpe shoo uone kama atakataa!! Lakini kama unataka shows za 10M; wapo wasanii watakaokupigia show kwa hiyo rate au hata kwa 5M lakini sio Diamond!!

Sorry, nothing personal but strictly business!!
 
Radio gani hii mkuu niache kuisikiliza
 
efm/tve washamalizana.
 
Kweli, saiv efm wanapiga ngoma za mond ila huko nyuma walikuwa hawapigi tena za wasafi kwa ujumla, na hapo kwa ipp sio kweli, ni eatv na ea radio ndo hawapigi lkn itv, radio one na capital radio wanapiga
 
Ngoma ikivuma sana hupasuka
Hio ni kanuni ya maisha
Kitendo cha kuachana mzazi mwenzie lazima kitamuwinda maisha yake yote.
Ishu inaitwa laana kwenye familia ni real.
Ataishia kama ilivyo baba yake.
Ni suala la muda tu
 
Mashabiki wa Mondi acheni kulialia na badala yake pambaneni na hali yenu. Kuna uzi uliwekwa humu kuhusu EATV na Mondi, wakati huo alikuwa vizuri na Clouds, mashabiki wake walitema shit sana kwa EATV kwamba hata wasipogiga clouds wapo na ndiyo wana ushawishi zaidi. Nilionya humu kuwa ipo siku hao Clouds wanaweza kuzipiga chini nyimbo zake na akakosa pa kukimbilia. Kiko wapi sasa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…