Mimi naamini Diamond Platnumz anaweza kustahimili huku kutengwa na media za bongo kwa sababu anajulikana kimataifa na Africa in particular wasiwasi wangu ni hawa watoto wadogo akina Harmonize, Lavalava, Rayvany, Mbosso et al hawa nadhani hajawafikiria ipasavyo, kwa maoni yangu hawa vijana wake bado wanahitaji msaada wa media za Tanzania ili kufika hapo alipo Diamond Platnumz.
Migogoro kati ya msanii na media madhara makubwa huwa yanakuwa kwa msanii na siyo kwa media maana media ina content nyingi sana kiasi kwamba si rahisi kuathirika na kutokucheza nyimbo ya msanii mmoja au wawili, kwa mfano kuna vipindi vya habari, maigizo, michezo, utamaduni, sijui mambo ya mwambao, vipindi vya dini, vipindi vya majadiliano ya kisiasa, uchambuzi wa magazeti etc hizo ni baadhi tu ya contents ambazo utakuta media moja inazo. Rejea bifu la clouds media na Rubby, au na Jide utaona hakukuwa na impact ya moja kwa moja kwa clouds fm
Hivyo basi kunusuru hii hali Diamond aharakishe ujaji wa wasafi TV na wasafifm ili kuwanusuru akina harmonize la sivyo hali yaweza kuwa mbaya upande wake.