Diamond amleta GODFATHER bongo kushoot video

Diamond amleta GODFATHER bongo kushoot video

bidam90

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2013
Posts
273
Reaction score
202
Diamond Platnumz ameamua kumleta muongozaji wa video zake, Mike Ogoke maarufu kama Godfather na timu yake kuja kufanya video zake jijini Dar es Salaam.

Diamond akiwa na msaidizi wa Godfather, Mike Dube jijini Dar

Muongozaji huyo na timu yake ipo jijini Dar kwa siku ya tano tayari na siku zote hizo imekuwa ikifanya kazi. Ofcourse Diamond na Godfather hawajasema chochote kuhusiana na hilo lakini msaidizi wake Mike Dube ameumwaga ubuyu.

Kwenye Instagram, Dube amepost picha ya pontoni la kuelekea Kigamboni na kuandika: ?@i_am_godfather, diamondplatnumz Taking a vessel to set! #musicvideo #tanzania #diamondplatnumz #godfatherproduction.?

Kama unamfollow Diamond utagundua kuwa juzi alipost kipande cha video akiwa kwenye gari lake wakiingia kwenye pantoni hiyo na anasikika akiwauliza wageni wake kama wameipenda Tanzania.

Dube pia amepost picha nyingine akiwa na Diamond na Harmonize pamoja na wanawake watu wazima wawili na kuandika, Tanzania day 4 diamondplatnumz, @i_am_godfather, Shettatz #musicvideo.

Hii ni mara ya kwanza Diamond kumleta Tanzania muongozaji wa video kutoka nje ya Tanzania kuongoza video zake.

Kuna taarifa kuwa Godfather anashoot video ya Diamond pamoja na za wasanii wake, Harmonize na Raymond.

Chanzo: Bongo5
 
quality is expensive..

katika vijana under 30 wanaotekeleza slogan ya hapa kazi tu kwa vitendo nazani Diamond anaongoza,,

kweli yeye ni team hapa kazi tu
 
Platnum kama kawaaaa anawanyooshaaaaa.....


Cc Kimbley
 
Last edited by a moderator:
DIAMOND anatumia gharama sana kuandaa kazi zake halafu kanatokea kamtu fulani eti kanajishindanisha nae kisa tu alisifiwa na sepetunga na kupata tuzo za chibuku.

Hana namna kizuri chajiuza jamaa Kazi zake ni za gharama za chini tu ila hamlali hahahaaaaaa.... Kibaaaaaaaaaaaaaaa hatar sana
 
Back
Top Bottom