STAA wa Bongo Fleva , Nasib Abdul ' Diamond
Platnumz' amefanya kufuru kwa kumzawadia
gari
mama yake mzazi , Sanura Kassim ' Sandra ' .
Diamond amemzawadia gari mama yake wakati
wa
bethidei ya kutimiza miaka 55 hapo jana katika
hafla iliyohudhuriwa na mastaa kibao.
Gari lililotolewa ni Toyota Lexus New Model
yenye
thamani ya milioni 38. 1. Diamond amekabidhi
gari
hilo kupitia kwa meneja wake, Babu Tale wakati
yeye akiwa nje ya nchi .
Sasa kufuru iko wapi hapo?Anyway,mi naona kama kachelewa nilidhani ashamnunulia
binamu mimi nasubili tu kufuru ya private jet, kwa kipato cha diamond kumnunulia mama yake gari sioni kufuru maana alishamnunulia gari marehemu gurumo fun cargo. mama yake anastahili zawadi hiyo, atakuwa anakwenda nalo wapi hilo gari?
bado diamond ana tatizo la kuwa na washauri uchwara bila shaka kuna mjanja kalamba commission yake kwenye ununuzi wa hilo gari, hapa nazidi kuona umuhimu wa shule. je mama yake anakabiashara chochote cha kumuingizia kipato hata diamond akifa ghafla mama mtu asitiye aibu kama mama yake kanumba?
Diamond anajua thamani ya mama, ila kuhusu hilo lexus asitudanganye apa
Diamond anajua thamani ya mama, ila kuhusu hilo lexus asitudanganye apa
Kulikuwa na ulazima hii habari kupelekwa kwenye media? Kama kweli mama yako unaishi nae sehemu moja sijaona sababu ya kufanya matangazo kwa sababu tu yakumnunulia kigari tu,huu ni zaidi ya ulimbukeni
Si unajua wengne wanapenda ku make headline na wao waonekane wapo angempa tu kimya kimya basi
Binamu dadavua zaidi.
Mimi sina uhakika sana kama kweli kamnunulia hiyo gari, na hata kama kamnunulia anataka tu kumuua mama yake, ananikumbusha jiran yangu, yeye hata gari kuendesha alikuwa hajui vizur kakimbilia kununua kluger ilichomfanya hana hamu tena na magari.
Sina uhakika sana kama mama yetu ni dereva, na hata kama akiwa dereva sidhan kama atakuwa ni wa kiwango cha hivyo, unajua mama dai ni mtu mzima na magar ndo hivyo tena wamebarikiwa kipindi hichi sasa kuanza kumkabidhi mama wa watu gari kama harrier lexus sidhan kama anamtakia mema mama yake, angenunua tu gari dogo la chini vya wanawake kama ist,passo au vits new model yan unaendesha vizur taratibu, sasa anampa hilo limzigo mmh
Usitake kuniambia ma wewe umeamini hilo gari limenunuliwa kweli? Hao attention seeker tu wanajua jins ya ku make headline, sasa mama sanura sijui na harrier lexus wap na wapi , si anataka tu kumuua mama yake huyu, mmh simpatii picha mama ndomo ndani ya lexus, watamkomaje mtaa wa pili?
Hata number plate wameficha kwani utakuta ni T.....BNN