Diamond amuita Jokate "makombo"

Diamond amuita Jokate "makombo"

mgt software

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
13,778
Reaction score
7,145
DONGO! Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond' amemuita mpenzi wake wa zamani Jokate Mwegelo kuwa ni makombo na kudai kama zilipendwa huyo anatembea na hasimu wake Ali Kiba, hakuna jipya kwani anakula makombo.

Diamond ametoa kauli hiyo Jumatano iliyopita wakati mwanahabari wetu alipotaka kujua anajisikiaje kuona wapenzi wake wa zamani Jokate na Wema Sepetu ‘Madam' wanamuunga mkono Ali Kiba.

Pamoja na kudaiwa kuwa Jokate ana uhusiano wa ‘kimalovee' na Ali Kiba na mwenyewe kutokubali, ameungana na Wema kuendesha kampeni ya nguvu kwenye mitandao ya kijamii kuhamasisha watu wampigie kura Kiba kwenye Tuzo za Kili 2015 kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kampeni ya kuuangusha ufalme wa Diamond kimuziki.

Baada ya mwanahabari wetu kuujua ‘mchezo huo' uliopamba moto kama moto wa kifuu mitandaoni ndipo alipomuuliza Diamond anauzungumziaje ambapo kwanza alikiri kuufahamu na kudai ameudharau maana hauna jipya.

"Hamna jipya waache waendelee kumpigia kampeni (Kiba) lakini mimi nafanya muziki wangu, mashabiki wanafahamu. Kwa hao watoto wa kike, hakuna kipya kwangu si kimuziki hata maisha yao binafsi.

"Wema namjua vizuri, Jokate ndiyo usiseme. Mwache huyo Kiba aendelee kula makombo kwa Jokate kama ameamua kipita njia nilizopita si mbaya, inaruhusiwa," alisema Diamond.

Jitihada za kumpata Jokate ili aweze kufunguka kuwa anajisikiaje kuitwa makombo na Diamond hazikuzaa matuda kufuatia simu yake kuita bila kupokewa, jitihada zinaendelea.


Chanzo: GPL

My Take:
Huku ni kudhalilishana kwa sababu wasanii wa kibongo kuchukuliana ndio fashien. Naye anayemtumia mke wa mtu hali makombo? Ifike hatua nao hawa wasanii wa mwaka 2006 waolewe wawapishe vijana wapya enzi zoo zimeisha wasije kukutwa na ndala wakati wa kuolewa.
 
Kwani jokate ana mdate kiba? Makombo huyajua makombo mengine mbona yeye anatembea na cougar uswahili bana Jokate nilikua namheshimu ila baada ya kumdate nikamuona hamnazo. Hasara za kudate mvulana lazima atangaze kila kitu.
 
Hahahahaa hizo ndala mbona wanazo?
Ila kama hii habari ni ya ukweli huu ni ulimbukeni sasa.Kwani yeye sio makombo? Katoka na wangapi?
Hii tabia ya kuponda wapenzi wa zamani ni ushamba uliopitiliza.
 
Dogo limbukeni jamani. Hivi vitu hakuwai kufukiria enzi hizo so msameheni bure tu.
 
Hahahahaa hizo ndala mbona wanazo?
Ila kama hii habari ni ya ukweli huu ni ulimbukeni sasa.Kwani yeye sio makombo? Katoka na wangapi?
Hii tabia ya kuponda wapenzi wa zamani ni ushamba uliopitiliza.

Usiamini sana magazeti ila jokate nae walewale maji mara moja unapakua tu juzi mwz kapakuliwa n ---- flani
 
Hivi daimond hizi kiki mavi ataacha lini???

Lazima atukane maex wake kutafuta promo ya nyimbo zake???

Hebu a-grow up ptuuuu
 
Nyapu haina makombo wewe. Anyway hii post ingewafaa kule MMU kwa kina Vitaimana
 
Last edited by a moderator:
Ama kweli mnahasira na Diamond, habari haina hata source mshaanza kuhororojoka!
 
Hivi huko aliko yeye sasa si kuna watu wanaita makombo yao....
 
Diamond kayasema lini na wapi?

Hiyo sheria ndio inabidi inyooshe watu kujua kazi zao na sio kuweka pesa mbele bila kujali mabaya wanayosababisha.

Diamond na Ney wameimba juu ya magazeti kwenye mwenye wao wakati yupo na Wolper na aamemtaja jina.

Ndio maana anasemaga siku hizi hasomi magazeti hivyooooooooii
 
Diamond kayasema lini na wapi?

Hiyo sheria ndio inabidi inyooshe watu kujua kazi zao na sio kuweka pesa mbele bila kujali mabaya wanayosababisha.

Diamond na Ney wameimba juu ya magazeti kwenye mwenye wao wakati yupo na Wolper na aamemtaja jina.

Ndio maana anasemaga siku hizi hasomi magazeti hivyooooooooii

Umeona eenh!Shigongo sasa hivi amezidi aisee halafu ili kudhihirisha uongo wake utaona ameandika"tulipompigia simu ya mkononi diamond iliita bila kupokelewa"
 
Back
Top Bottom