Kwa kumbukumbu zangu enzi izo nafatilia miss tanzania kuanzia ngazi ya kitongoji hadi taifa Wema wakati anagombea miss dar indian ocean then miss kinondoni then miss tanzania alikuwa anaandikwa ana miaka 18 means kazaliwa 1988 huo ulikuwa mwaka 2006 kwahiyo kwa rekodi ya miss tanzania kule kwa sasa atakuwa na miaka 26 na hata rafiki zake wa utotoni aliocheza nao Sinza niliokutana nao wana age hiyo.
Jokate nae tangu anaanza miss Kurasini mwaka 2006 then Temeke no. 1 then miss Tanzania aliandikwa ana miaka 19 hii inaonyesha alizaliwa mwaka 1987 ila nayeye sikuiz kajitahid kurudisha mwaka nyuma anasema kazaliwa 1988.
Uwoya naye mwaka huo huo 2006 kutoka Miss Chang'ombe then Miss Temeke no. 2 then Miss Tanzania top five nayeye aliandikwa kazaliwa mwaka 1988 na kipindi hicho alikuwa na miaka 18.
NB: Ili ushiriki miss Tz inabidi uwe na miaka 18-25 na mwaka 2006 mwenye umri wa miaka 18 ni aliyezaliwa mwaka 1988.
Ni hayo tu.