Diamond ana maslahi gani kupromote pombe?

Diamond ana maslahi gani kupromote pombe?

Kana-Ka-Nsungu

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2007
Posts
2,257
Reaction score
363
Diamond ni celebrity wetu na ni wazi kuwa wadogo zetu wengi walioko mashuleni watakua wanamuona kama role model na watakua wanaichukulia mistari ya nyimbo zake seriously. Alipotoa nyimbo ya 'mawazo' nikawa najiuliza sasa anaposema ' ningekua na uwezo ningekunywa pombe nipunguze mawazo' si atakua anawapotosha wadogo zetu? Si atawafanya waamini kwamba mtu ukiwa nazo na ukawa na mawazo basi solution ni kunywa pombe?. Kama hiyo haitoshi, nimeskiliza nyimbo yake mpya ya 'Nataka kulewa' ambayo pia maudhui yake naweza kusema kua yana promote pombe indirectly pia. Uwezekano ni mkubwa kuwa wadogo zetu ambao wengi ni wageni kwenye mchezo wa mapenzi, watakimbilia kwenye pombe kama suluhisho kila watakapokua na matatizo kwenye mahusiano yao.

Msanii kama Diamond naamini ana nafasi kubwa sana ya kuielimisha jamii hasa vijana juu ya madhara ya pombe na si kuiweka kwenye mashairi ya nyimbo zake na kuitukuza ionekane kama ni kitu kizuri na suluhisho la matatizo. Ukiachilia mbali matatizo ya afya kedekede yanayosababishwa na matumizi ya pombe pia kuna ajali nyingi za barabarani zinazosabishwa na pombe, watu wanapoteza maisha kila kukicha na wengine wana vilema vya maisha. Kuna wenzangu na mie ambao wakishaonja wakirudi home ni kudunda wake zao na watoto, na kuna wale ambao baada ya steam kupanda 'husahau' kua wana condom kwenye wallet wakati wakiondoka na bar maid au dada poa na matokeo yake wanaishia kuuza mechi na kuwapelekea wapenzi wao wa kudumu virusi!

Sina hakika kama yuko aware na impact ya nyimbo zake kwa wadogo zetu au anapata maslahi yoyote toka kwa makampuni yanayotengeneza pombe...Kwani kuna ugumu gani kuchomeka mistari ambayo ina discourage matumizi ya vilevi kwenye mashairi ya nyimbo zake nzuri?

Kana-Ka-Nsungu
 
Nimekuelewa sana mkuu ila wakati mwingine ukitaka kufuatilia kila kitu kwa undani sana utakwama tu. Kabla huyo Diamond hajatoa huo wimbo kulikuwa hakuna walevi? Mbona walevi walikuwepo tangu enzi zile Muhidin Gurumo anaanza kuimba? Ngoja na mimi nikuulize swali ili ujue ukitaka kufuatilia kila kitu kwa undani sana utakwama, hivi una maslahi gani kuanzisha hii thread?
 
akiimba kuhuku kilimo bora mtanunua?

Wakeeni vijana katika njia iliyonyooka, mtoto akuone wewe mzazi kuwa role model na si msanii
 
Wadogo zako wanatakiwa wafuate yale mazuri na kuacha mabaya, kuwa star haimaanishi uwe 100% perfect as no one is perfect. Nazani jibu unalo maslahi mbele.
 
Nimekuelewa sana mkuu ila wakati mwingine ukitaka kufuatilia kila kitu kwa undani sana utakwama tu. Kabla huyo Diamond hajatoa huo wimbo kulikuwa hakuna walevi? Mbona walevi walikuwepo tangu enzi zile Muhidin Gurumo anaanza kuimba? Ngoja na mimi nikuulize swali ili ujue ukitaka kufuatilia kila kitu kwa undani sana utakwama, hivi una maslahi gani kuanzisha hii thread?

Wasanii wetu wasiitukuze a kuhamasisha matumizi ya pombe!
 
akiimba kuhuku kilimo bora mtanunua?

Wakeeni vijana katika njia iliyonyooka, mtoto akuone wewe mzazi kuwa role model na si msanii

Nawafahamu wazazi kibao ambao ni role models wazuri tu lakin watoto wao wameshindikana kwasababu nyingi tu ikiwemo na hii ya kuiga yale yanayosemwa au kufanywa na celebrities.
 
yeye yuko kikaz na anafanya kile anachoona kitamuingizia pesa. Akiimba mambo ya maana hamnunui mbona nyimbo nyingi za maana zipo hamsikilizi wasanii wanaoziimba wamefulia
 
hivi hako ka bwana mdogo kamewahi kuimba wimbo usio wa manung'uniko?
 
Naamini mwanangu hamjui diamond. Diamond mnajua nyie watu wa dar es salaam mliokosa maaadili.
 
we dont care about maadili the only we care is business imani ya diamond haimruhusu hata kuingia bar/club hata kufanya mapenzi mpka harusi sio mimi ni imani yake ndio inavyosema maana nilimsikia kwenye interview moja kuwa yeye ni mtu wa dini fulani sembuse huo wimbo? mkuu tukijichunguza sana hata sisi kama watu wangekuwa wanajua maovu yetu hakika usingeweza kutoka nje, tuongelee mambo mengine ambayo yanaweza kuleta impact kubwa kwenye jamii maana suala la maadili linaanzia kwa mzazi wako na familia yako usisubiri diamond aje akuelimishe. ndipo waswahili wakasema usipofunzwa na mama yako utafunzwa na diamond(ulimwengu).
 
Pombe siyo kitu cha kuki discourage, Pombe ni kitu kizuri na moja ya matumizi yake ni kupunguza mawazo, lakini pombe imekatazwa kunywewa na watoto wa umri chini ya miaka 18. mimi nafikiri ukiona watoto wako wanakwenda huko waambie tu kuwa diamond alikuwa anawalenga watu wazima. Manguli kama sisi.
 
Pombe siyo kitu cha kuki discourage, Pombe ni kitu kizuri na moja ya matumizi yake ni kupunguza mawazo.

Mkuu unajua ni watu wangapi wamekufa au wapo mahospitalini kwa ajili ya pombe? In my opinion, alcohol is more harmful kuliko hata cocain na heroin! Na unaweza ukapunguza mawazo ukiwa na steam lakini ikikata mawazo yanayokusumbua yatakua palepale. Na kwa uzoefu wangu kama kuna issue inakusumbua kichwani ukipiga tungi mawazo yanaweza yakakuzidia ukaishia kuangua kulio au kama kuna muhusika ukamfata na kumtolea uvivu kwa maneno au hata kupigana- ukajikuta unaishia jela, hospitali au kaburini.
 
Nawafahamu wazazi kibao ambao ni role models wazuri tu lakin watoto wao wameshindikana kwasababu nyingi tu ikiwemo na hii ya kuiga yale yanayosemwa au kufanywa na celebrities.
Vipi kuhusu wale wenye maadili mema wakati hao maceleb wakiendela kuisifia pombe?
 
Mkuu unajua ni watu wangapi wamekufa au wapo mahospitalini kwa ajili ya pombe? In my opinion, alcohol is more harmful kuliko hata cocain na heroin! Na unaweza ukapunguza mawazo ukiwa na steam lakini ikikata mawazo yanayokusumbua yatakua palepale. Na kwa uzoefu wangu kama kuna issue inakusumbua kichwani ukipiga tungi mawazo yanaweza yakakuzidia ukaishia kuangua kulio au kama kuna muhusika ukamfata na kumtolea uvivu kwa maneno au hata kupigana- ukajikuta unaishia jela, hospitali au kaburini.

Hivi, kwani wasiokunywa pombe hawafi? Wasiokunywa hawafungwi jela? Wasiokunywa hawaendi hospitali? Wasiokunywwa hawatukani watu huko mitaani? hii ni shida kwa wasiokunywa kudhani wapo salama zaidi ya wanaokunywa. Tatizo lenu ni kuwa mnapinga sana pombe lakini hamtumii kondomu wala net au mnaendesha magari vibaya na mwisho mnakufa kwa ajali
 
There you go Mr Senior Expert, kuna mambo mengi tu kama hayo uliyoyataja ambayo wasanii wetu wanaweza kuyaingiza kwenye mistari ya nyimbo zao na kuielimisha jamii, sio lazima iwe pombe tu.
 
Sasa si bora diamond mpotosho wake no rahisi? Wanaoimba mapenzi ndo wanaharibu watoto, manake wanakuwa wanafikiria in a certain way about mapenzi. Just saying!
 
akiimba kuhuku kilimo bora mtanunua?

Wakeeni vijana katika njia iliyonyooka, mtoto akuone wewe mzazi kuwa role model na si msanii
jaman kwenye simu hamna kitufe cha kulike ningelike maana umetoa point nzuri sn na siku zote unakuwaga reasonable kama jina lako BADILI TABIA, i really like it.
 
Sifa za kijinga zinamfanya asahau Mungu wake hasa ukizingatia yeye ni Muislamu, na msimamo wa Uislamu uko wazi kabisa juu ya Pombe. Sio kua ni haramu kuinywa bali hata kuiuza, kuibeba, kuisifia, kutengeneza, kuhudumia etc.

Mwenzake Mzee Yusufu, ameepuka mtego huo. Mwache alewe sifa, maana hiyo ni zaidi ya pombe.
 
Back
Top Bottom