Kana-Ka-Nsungu
JF-Expert Member
- Oct 4, 2007
- 2,257
- 363
Diamond ni celebrity wetu na ni wazi kuwa wadogo zetu wengi walioko mashuleni watakua wanamuona kama role model na watakua wanaichukulia mistari ya nyimbo zake seriously. Alipotoa nyimbo ya 'mawazo' nikawa najiuliza sasa anaposema ' ningekua na uwezo ningekunywa pombe nipunguze mawazo' si atakua anawapotosha wadogo zetu? Si atawafanya waamini kwamba mtu ukiwa nazo na ukawa na mawazo basi solution ni kunywa pombe?. Kama hiyo haitoshi, nimeskiliza nyimbo yake mpya ya 'Nataka kulewa' ambayo pia maudhui yake naweza kusema kua yana promote pombe indirectly pia. Uwezekano ni mkubwa kuwa wadogo zetu ambao wengi ni wageni kwenye mchezo wa mapenzi, watakimbilia kwenye pombe kama suluhisho kila watakapokua na matatizo kwenye mahusiano yao.
Msanii kama Diamond naamini ana nafasi kubwa sana ya kuielimisha jamii hasa vijana juu ya madhara ya pombe na si kuiweka kwenye mashairi ya nyimbo zake na kuitukuza ionekane kama ni kitu kizuri na suluhisho la matatizo. Ukiachilia mbali matatizo ya afya kedekede yanayosababishwa na matumizi ya pombe pia kuna ajali nyingi za barabarani zinazosabishwa na pombe, watu wanapoteza maisha kila kukicha na wengine wana vilema vya maisha. Kuna wenzangu na mie ambao wakishaonja wakirudi home ni kudunda wake zao na watoto, na kuna wale ambao baada ya steam kupanda 'husahau' kua wana condom kwenye wallet wakati wakiondoka na bar maid au dada poa na matokeo yake wanaishia kuuza mechi na kuwapelekea wapenzi wao wa kudumu virusi!
Sina hakika kama yuko aware na impact ya nyimbo zake kwa wadogo zetu au anapata maslahi yoyote toka kwa makampuni yanayotengeneza pombe...Kwani kuna ugumu gani kuchomeka mistari ambayo ina discourage matumizi ya vilevi kwenye mashairi ya nyimbo zake nzuri?