Diamond anatangaza kuoa, Jokate kuolewa, Wema?

Diamond anatangaza kuoa, Jokate kuolewa, Wema?

Interest

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2015
Posts
3,434
Reaction score
7,072
Pamoja na vyuma kukaza, bado anga la burudani lina shamra shamra kila uchwao!

Ndani ya mwaka huu matukio mengi ya burudani yamefululiza na bado yajayo yanafurahisha, swali la msingi hapa ni je upo tayari?!

Tukiachana na mapichapicha ya Tunda na Casto 'komando kipensi', tukasahau ya Basata na Wasanii mpaka visa vya N/Waziri Shonza, tukasahau na kupotezea kabisa mambo ya maua mekundu, meusi, meupe na kadhalika.. Bado yajayo inaonekana yanafurahisha!

Wema katangaza jambo kubwa kutokea Juni 30 na hata kutoboa kuwa atakuwa mtangazaji wa Wasafi Media. Huyu tumuache kwanza!

Kama Jokate ataolewa mwaka huu kama anavyosisitiza kila siku pasipo kutaja lini na nani.. Na Diamond naye kusema hayo hayo. Hili halipigi kengele?

Pengine wote wameweka nadhiri iwe isiwe lazima mwaka huu kieleweke pasipo kujua watakielewesha na nani; ni vipi sasa kama wakakutanisha dhamira zao na kufanya kweli wao wenyewe?!

Nawaamini wote wawili katika kupambania maisha na career zao. Ni ndege wafananao, waruke pamoja!
 
Labda anayetaka kuolewa in Wema,ndio maana unaona kimya.
 
Back
Top Bottom