Diamond anunua kifaa cha 40M (Wasafi Records)

Mshamba wa kusini

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2015
Posts
2,857
Reaction score
3,593
Mkali wa wimbo ‘Salome’ Diamond Platnumz amesema ameagiza mixer kubwa nje ya nchi ili kuboresha studio ya‘Wasafi Records’ ambayo tayari imeshaanza kushafanyahits kadhaa ambazo zinafanya vizuri katika chart mbalimbali za muziki nchini.

Muimbaji huyo wiki hii alitembelewa ofisini kwake na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira, January Makamba na kumueleza mambo mbalimbali ambayo atayafanya ili kuboresha ofisi hiyo.

“Kwa sasa tunasubiri mixer ifike kwa sababu tuliambiwahatuwezi kuichukua dukani mpaka tutoe order watutengenezee,” Diamond alimwambia Waziri January.

“Zingekuwa ni zile ndogo ndogo wangenipa lakini kwa sababu hii ni kubwa sana lazima utoe order, na tayari nimeshalipia kama dola 20,000 na kitu,”

Pia Waziri January Makamba alimsifia producer wa ‘WasafiRecord’ Lizer kwa kufanya maajabu kwenye wimbo mpya wa Diamond ‘Salome’ ambao kwa sasa unafanya vizuri.
 
Safi, huyo ndo bwana D, wakati wengine wanapoendelea kupigia wenzao majungu na lawama, mwenzao ana nunua vifaa, fanya kolabo , boresha muziki.
*ki ufupi ni kuwa jamaa anajituma , na anajua, ni kosa kubwa sana kumfananisha Domo na msanii yeyote hapa bongo.
 
Kijana nikimzoom nimtu wa aina yake kajipanga vyema sana bigup kwake
 
Hivi ile mixer ya serikali ambayo alinunua JK.. Iko wapi vileee
 
Kama na hich kifaa watashindwa kufanya mastering ili mziki wa bongo uwe na quality ya kimataifa itakua kazi bure....
 
Hii Dunia kuna vitu inabidi ucheke tu,japo ni vya kuumiza.
umemzidi pesa.
tuzo.
shoo.
mijengo.
unayo bendi.
unatumia gita.
una wasanii wanaokuingizia pesa kuliko anazoingiza yeye.
una lebel.
shoo zake ni kenya na tz. mwenzake karibia dunia nzima.
familia nzima ni maarufu.
ni balozi wa makampuni zaidi ya 5.
ana boooonge la timu linalomtegemea yeye.

WCB HUWA WANACHEEEEEEEEEEEEKA,WANAPOSIKIA VITUKO BADALA YA KUNUNA.

Wakuu mixer yetu inalingana kama sio kufanana na hii.
 
Salome - good melody ndani matusi matupu tena usiyohitaji kufikiri ili uyaelewe halafu Waziri anasifia
Kumbe DIAMOND huwa akiona habari zimemzungumzia vibaya,komenti mbaya ,kashfa, yeye huwa anacheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeka,kuliko watu wanavyochukulia siriazi huku kwenye mitandao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…