Diamond anunua kifaa cha 40M (Wasafi Records)

Diamond anunua kifaa cha 40M (Wasafi Records)

Story ya nyumba ya south imezimika kama sio kuyeyuka..
 
Nasubiri ikishafika amuite swizz bits aje agonge ngoma.
 
Mkali wa wimbo ‘Salome’ Diamond Platnumz amesema ameagiza mixer kubwa nje ya nchi ili kuboresha studio ya‘Wasafi Records’ ambayo tayari imeshaanza kushafanyahits kadhaa ambazo zinafanya vizuri katika chart mbalimbali za muziki nchini.

Muimbaji huyo wiki hii alitembelewa ofisini kwake na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira, January Makamba na kumueleza mambo mbalimbali ambayo atayafanya ili kuboresha ofisi hiyo.

“Kwa sasa tunasubiri mixer ifike kwa sababu tuliambiwahatuwezi kuichukua dukani mpaka tutoe order watutengenezee,” Diamond alimwambia Waziri January.

“Zingekuwa ni zile ndogo ndogo wangenipa lakini kwa sababu hii ni kubwa sana lazima utoe order, na tayari nimeshalipia kama dola 20,000 na kitu,”

Pia Waziri January Makamba alimsifia producer wa ‘WasafiRecord’ Lizer kwa kufanya maajabu kwenye wimbo mpya wa Diamond ‘Salome’ ambao kwa sasa unafanya vizuri.

Utumbo mtupu
 
Huyu wazili ajielewi inakuwaje support ipo kwa akina domo tu mbona studio zipo kibao mara kikwete mara waziri basi tutembelee wasanii wote tz huko ni kujipendekeza,sipendagi ujinga
 
Yap diamond anajua kutumia fursa aliyonayo amesoma mchezo ulivyo kwenye anajua kuna siku atahitaji kupumzika au kupumzishwa kwaiyo anatengeneza mazingira ya kubakia kwenye game ata km atakua ajatoa singo kwaiyo ataendelea kuingiza pesa kwa kupitia vitega uchumi anavyojiwekea, na itakua ngumu sana diamond kutokusikika ktk game kwa wakati huu kwa mwenendo alionao yupo right kabisa kwa kumshauri tu aendelee kuinvest ktk suala la mziki naomba awe na video production ya kisasa hapo atakua kamaliza ktk upunde wa sanaa na ikiwezekana anaweza anzisha kituo chake cha radio sababu rogo yake ya wcb inamfanya azidii kua na sababu ya kutafuta asilizike mapema achape kazi
 
Back
Top Bottom