Diamond apewa ardhi ya kuishi nchini Kenya

Robo heka nayo ni ardhi ya kukaa star!garden,parking,swimming pool,courts au ndio bora kitu kuliko kukosa kitu
Yategemea location yake mkuu. Imagine amepata eneo la upper hills
 
Good comment....nakubaliana nawe mia kwa mia
 
Adui wakiniudhi nami nikisumbuka
Mungu atavigeuza vitakuwa baraka [emoji445][emoji443]
 
Asisahau Kenya sometimes kunawaka marisasi so sio nchi ya kupeleka kundu lako n kulikalisha ovyo ovyo ....utakula marisasi time za general election.... Tanzania nzuri jmn ohooooooo
 
Unachosema ni kweli asee maana hata Tundu Lissu na Akwilina walikula marisasi huko huko Kenya. Diamond kuwa makini.
Kumbuka marisasi za Kenya ziliua watu wengi sana,it was civil war ,sio kama hyo ya lissu na akwilina.....
Kenya is not safe hasa times za uchaguzi
 
Hata Ben Saanane kapotelea Kenya
Nyie ropokeni tu...sjui mmeshiba pilau LA Jana.....mnafikiri vita ya Kenya inauaga MTU mmoja et?? N thousands of people collapse,n mass genocide.....angalieni na matakwimu jmn....Kenya akafanye business ila kuchukua uraia hapana kabisa....atachuta one day
 
Umajiona unajua sana kuliko sisi?
 
Tanzania ni nchi ambayo ina msimamo na maadili yake kitamaduni. Kutii na kuheshimu sheria ni moja ya msingi wa maisha watanzania lazima tuzingatie. Hakuna mtu ambaye yuko juu ya sheria na maadili yetu ya utamaduni wa maisha lazima yafuatwe, yadumishwe na kuimarishwa. Kama kuna mtu anafikiri anaweza kutumia bahati ya umaarufu wake kuli-undermine taifa letu kwa kukebei sheria zetu basi naomba huyo mtu aende na umaarufu wake kuishi huko anakofikiri anaweza kufanya upuuzi huo anao utaka kuufanya.

By the way Diamond ni nani hasa katika ulimwengu huu kiasi kwamba kuondoka kwake kukatupa shida sisi watanzania?

Watanzania wenye busara na akili timamu nawaomba mtambue kuwa Diamond hivi sasa sio mtu wa kawaida tena. Diamond amesha kuwa msanii ambaye amesha shikwa na watu wale ambao ni maadui wa maendeleo ya nchi yetu. Ni mtu ambaye anatumiwa na maadui wetu wa kisiasa, kijamii na maendeleo ya kiuchumi wetu ambao wakilala na kuamkua wana waza jinsi ya kutuharibia mafanikio yetu ya amani na umoja wetu na pia maendeleo ambayo tunayaona tunakaribia kuyapata.

Watanzania naomba pia mfahamu nchi kama Kenya haitapenda kusikia sisi kuendelea kiuchumi na hivi sasa tuko katika track nzuri ya kuwa beat wao. Hivi bado hamjagundua tu njama na juhudi zinazofanywa na wakenya kutuangamiza sisi? Mtanzania asiye yaona hayo basi ajue kuwa yeye amesha kuwa maiti au yuko katika state ya kuwa maiti yaani ni zombi.

Matokeo kama ya 1977, msaada wa wakenya kwa nduri Idi Amin Dada katika vita kati yetu na nduri huyo, jitihada za kuua sekta yetu ya utalii iliyo fanywa na wakenya miaka yote iliyopita nyuma, Tanzanite, biashara ya Shrimps, swala la Tundu Lissu na hivi sasa Diamond, hizo zote ni dalili ambazo zinaonyesha kiasi gani wakenya wanavyotumiwa na vibaraka wao kutaka kuleta machafuko ya amani ya nchi yetu ili sisi tufarakane na kuvunja umoja wetu. Tanzania ni taifa la watu wenye msimamo asante Rais wetu wa awamu ya kwanza kwa kutuwekea msingi wa ushupavu wa hali ya juu.

Mpenzi na mtu ambaye aliamini stability ya East Afrika ni hayati Rais Mpenzi Jomo Kenyatta tu, wengine wote walio fuata ni vidampa tu wa mabeberu. Sijaona nchi ambayo watu wake hawa jiamini kama Kenya. Ni nchi ambayo haiwezi panga badjet yake bila kutegemea msaada kutoka kwa mabeberu wao. Wana madeni mpaka yanawatokea puani. Hayo yote yamekuja baada ya wao kutaka kuishi zaidi ya uwezo wao. Wameongozwa pabaya?

Naapa kwa Mungu kama Diamond ataamua kuhamia Kenya ajue ndiyo kifo chake cha kuwa mwana sanaa maarufu kinakaribia. Mwambieni afanye hivyo aone kama hata mwaka utafika kama hajatoweka kwenye jukwaa la wasanii maarufu.

Yeye sio mtu wa kwanza kufanya hivyo Charly Chaplin actor maarufu duniani naye alifanya kitendo hicho cha kuiacha nchi yake akitegemea atabaki kuwa maarufu alisahau kuwa waamerika ndiyo waliomwezesha kuwa na umaarufu huo, matokeo yake aliyaona baada ya uamuzi huo. Huo ndiyo ulikuwa mwisho wa umaarufu wake mpaka kifo kilipomjia.

Kama Diamond anaona umaarufu alio upata yeye sasa ameguka kuwa ni mungu mdogo na kuanza kuwadharau watanzania ambao ndiyo waliomfanya mpaka kuwa katika position hiyo aliyo nayo sasa, ajue sasa yuko mbioni kupoteza mafanikio yake hayo yote. Ataanguka vibaya sana.

Asanteni sana wazalendo wa nchi yetu na mniwie radhi kwa wale nitakao kuwa nimewakwaza na hoja yangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…