Narudia tena kusema huyu ' Jamaa ' mtamsema, mtamtusi na kumdhihaki kadri muwezavyo ila matunda ya Kazi zake, Kujituma Kwake, Kuwa mbunifu na Kujipanda ndiko kila siku kunamweka na bado kutamweka Kileleni Kimafanikio. Nasib Abdul ( Diamond Platinumz ) anatupa ' Funzo ' zuri na kubwa sana akina Sisi wenye ' akili kulala ' au ' akili mlegezo ' kama si ' akili goigoi ' kupambana na kutokata tamaa katika kuyatafuta mafanikio ya kweli.
Namuombea kwa Mwenyezi Mungu ( Allah ) mafanikio zaidi na hakuna Siku ambayo nimewahi kumuombe Mtu ' baraka ' kwa Mwenyezi Mungu na asinijibie Kwake hivyo naamini Nasib Abdul ( Diamond Platinumz ) atazidi kuwa juu na juu na Sisi wengine tusichoke kumchukia, kumteta, kumdharau na kumzushia kwani yawezekana hii roho mbaya Yetu Kwake basi Maulana ndiyo anaigeuza kuwa Shani na Baraka Kwake.