Diamond asema nimesitisha kupeleka matumizi ya watoto South

So what? kwani hapa ni ustawi wa jamii. ebo!
 
Ngoja na mimi wangu nimsitishie pesa ya matumizi (Matunzo)..
 
Dah mimi nasubiria wali wangu wa biriani hapa na kuku ..hizo habar zenu ntazisoma nikishashiba
 
Nonsense sasa hapa anawakomoa watoto au Zari? Hayo matumizi anayotuma ni kwa ajili ya ya watoto wake mwenyewe sasa shaka la kwamba Zari hapokei simu zake ndio iwe sababu ya kuto support kids wake mwenyewe? Namna hii huko mbeleni watoto wakishakuwa wakubwa si ndio hawatataka hata kusikia jina la Baba yao kama ilivyo yeye na Baba yake? Kutopeleka $2,000 kwa Zari kwa ajili ya child support hiyo kwa Zari sio issue course hana njaa can support watoto wake wote bila shida yoyote
 
Hapana mkuu, huyo zari naye ana tatizo kama kagombana na diamond kwann awaingize watoto ? Inaonyesha zari bado anamtaka diamond
 
Watoto hanawakataza kuongea na Baba Yao , pesa ya Baba Yao ( diamond) anachukua , huyo zari aache ujinga
 
Shida ya kina mama wengi unapogombana naye atajitahidi kukuweka mbali na wanao kama adhabu.Sasa sisi wanaume katika kikao chetu cha jana tumekubaliana ukiona mtalaka wako anakutenga na wanao kama adhabu basi unafunga mirija ya posho unatafuta watoto wengine.
 
Na wale mnaowafungia hiyo mirija ya posho huwa wanafanikiwa sana
 


Baba unanyimwa vipi mtoto wako , mnatelekeza watoto kwa kisingizio cha mama zao wanewanyima
 
Tatizo jamaa ana wivu sana...

Alafu alidhiani yule mwanamke wake ataanza kumlilia njaa kama ma-ex wake wengine...



Cc: mahondaw
 
Wakikua watamtafuta. Kipindi hiki hawana maamuzi, yeye awawekee chao watamdai tu. Na ni mapito tu hayo. Waliochukuliwa wakati wa biashara za utumwa, wapo walioanza kufuatilia chimbuko Lao Afrika. Time will tell
 
Ugomvi wa Wazazi unawadhuru Watoto wasio na hatia.

Upumbavu tu....!
 
Kwahiyo kumkataza asiongee na watoto wake unaona ni sawa? Hata Mimi ukinikataza nisiongee nao hela situmi.siwezi kumtumia hela mtu ambae ana nionesha kiburi na jeuri. Huyo zari kinamuuma nini diamond akiongea na watoto.tabia za kiswahili hizoo
Pesa kwa ajili ya Nani? Unatakiwa kuniuliza kabla hujatuma, ule sio msaada Ni jukumu lako Kama unavyojinunulia chakula

Tatizo wengi kutoa matumizi mnachukulia Kama kutoa msaada mtu mpaka ajikombe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…