Diamond ashinda tuzo za AELA awards 2016 nchini Nigeria

Diamond ashinda tuzo za AELA awards 2016 nchini Nigeria

MO11

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2014
Posts
19,057
Reaction score
39,387
Kijana wa kununua viewers timu ujanja ujanja amenunua na kupewa tuzo ya best collaboration of the year.

Nyimbo yake ya ujanja ujanja aliowashirikisha wajanja wajanja P square inayoitwa KIDOGO.

Waandaaji wa tuzo wamesema hawataki matusi kwa wasanii walioshindwa kwenda kwa wasanii walioshinda.

Pia wameenda mbali na kusema hawataki wasanii wa muziki mzuri maana unapendwa sana.

WATASHINDANA LAKINI HAWATASHINDA
 
Tuzo za AELA zilitolewa jana nchini Nigeria huko
1480324557365.jpg

Mtanzania Diamond platnumz akishinda Tuzo ya Best collabo kupitia wimbo wake wa kidogo aliowashirikisha Psquare.
1480324734353.jpg

1480324625295.jpg

Diomond amewashinda
Tiwa savage ft wizkid -- bad
Flaviour ft selebobo --- mgeme mgeme
Yemi alade ft sauti sol --- africa
Patoranking ft sarkodie --- no kissing .

Huku Korede bello akishinda tuzo ya best music video kupitia wimbo wake wa Romantic
Hongera sana diamond
 
Naona wanaigeria wanashindana kutafuta kiki kupitia mashabiki wa diamond na kuba kwa kuanzisha tuzo kila kukicha.

Hongera yake
 
MOND aliwauliza swali moja la msingi sana,kama wewe muziki wako mzuri kuzidi mimi vipi Mapromota hawakuoni wakupe shoo,hadi upate zile za Mombasa tena kwa hisani ya jamaa yako ........ Hongera MOND kwa tuzo.
 
Si ndio huu wimbo waliuponda sana humu ndani!

Leo kama vipi [HASHTAG]#Wakanywe[/HASHTAG] maji
 
Ali lazima atajwe ALI UTAWAUAAAAA
Ali kiba tunamzungumzia kwa kwa sabab ya uwepo wa diamond
Jamani DIAMOND si alisema hawez kusainiwa au yalikuwa mawivu?
Mkuu,
Ni kweli na ndiyo maana YouTube/ Google kitambo tangu mwaka 2012 wanafanya uhakiki wa mara kwa mara kuona ''umaarufu'' kuanzia Youtube Account holders binafsi au kampuni na pia account za msanii, mwanamuziki, label za kampuni kubwa za muziki n.k kama ni sahihi au la, hivyo ni ngumu sana mwaka 2016 msanii ''mkubwa'' akajaribu ku-''manipulate'' a.k.a kutumia ''maruhani wa Apps/ teknolojia'' kuongeza views n.k bila ''panga'' la Youtube kumpitia pamoja na ''onyo kali'' pia angalizo zoezi hili la uhakiki YouTube /Google ni endelevu.

Mfano AliKiba yupo na kampuni kubwa ulimwenguni Sony Alikiba Becomes the Second African Artist to Sign a Global Music Deal With Sony Music na Msanii mkubwa kupita wote Tanzania, Diamond Platnumz amesaini Universal Diamond amesainiwa Universal Music Group mwaka huu, hivyo wasanii binafsi kwa kuwatumia hawa wawili kama mfano waliosaini na kampuni kubwa uhakiki hupita kwa msanii binafsi na kampuni iliyomsainisha wakitupia vitu vyao Youtube moja kwa moja au kupitia washirika wao.. Soma zaidi mtandao wa : Fake YouTube Views Cut By 2 Billion As Google Audits Record Companies' Video Channels | The Huffington Post

Ali kiba akauze nguo kariakoo, hata huyo darasa mziki wake mzuri, ila haufiki hata chalinze
 
Ali lazima atajwe ALI UTAWAUAAAAA
Jamani DIAMOND si alisema hawez kusainiwa au yalikuwa mawivu?
Lebo yake ndio imeingia mkataba na universal music! ila yeye hajasainiwa tofauti na wale wa sonny ambao wanampangia msanii muda wa kutoa ngoma!
 
Back
Top Bottom