Hivi ukiwa unapanda Huko mlimani unaenda na simu au simu huruhusiwi ? Na kama simu zinaruhusiwa je, ikikata charge unacharge wapi ? Na kama hairuhusiwi , inawezekanaje mtu usiwasiliane na ndugu zako kwa muda wote huo mpaka utakaporudi toka kileleni ? Na hata kama zinaruhusiwa na pakucharge papoo , je network vipi zinashika ?
Kwa wenye mauzoefu ya kupanda huko tupeane info maana najipanga panga nami nikajaribu , so kuna haja yakuanza kujiandaa kisaikorojia ya kutokumia simu na kutokuingia JF kwa wiki na ushee
Mkuu naomba nikujibu kwa kadri niwezavyo.
1. Kuhusu kwenda na simu•
Simu zinaruhusiwa kabisa hakuna mtu atakayeshughulika na kukukagua simu au camera(isiwe yakibiashara)...
Vitu visivyoruhusiwa ni kama vile sigara, bangi na vitu vyote vya makopo kopo mf. Zile chupa za maji ya Kilimanjaro na mifuko ya plastic haviruhusiwi ili kuweka mazingira safi.
2.Simu zikiisha chaji inakuwaje?
Hapa lazima ujipange kidogo either uwe na powerbank na simu yako iwe na uwezo wa kutunza chaji, kuhusu kuchaji unaweza kuchaji! Kwenye vituo vya wale macare taker wanahuduma ya kuchaji na inaweza kukugharimu hadi Tsh 2,000/=
Kutokana na baridi chaji huwa inaisha haraka sana.
Mfano simu au camera ikiwa full charge 100% na usipoiweka vizuri itaisha tu hata kama usipoitumia. Kama unataka kuselfika ukiwa Uhuru peak, wewe mpe hicho kifaa guide wako au atakuelekeza namna yakuhifadhi ili ukiwa juu kiwe na uhai.
Kuhusu network kuna maeneo yana network mkuu tena nzuri tu. So unaweza kuwasiliana na ndugu zako vizuri.
Kwa route ya Marangu, network iko poa pale Horombo. Kwa machame, Baranco pana network nzuri...
Karibu sana mkuu, Mlima Kilimanjaro ni mzuri sana.
Kama unaswali usisite kuendelee kuuliza.