Diamond Awachana BASATA

Diamond Awachana BASATA

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
Ni msanii ambaye anaweza kuwa ametajwa zaidi kwenye tuzo za KTMA 2014 lakini Diamond Platnumz hajaliacha Baraza la Sanaa Tanzania likae kwa amani kwa uonevu ilioufanya kwa Jux, Madee na Snura kutokana na kuziondoa nyimbo zao kwenye mchakato wa KTMA 2014.
Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’.

Kupitia Instagram, Diamond ameandika:

“Ikiwa kweli tunalengo la kutoipotosha kimaadili jamii yetu na vizazi vyetu pendwa, nafikiri ni vyema tungeanza kuzuia Video na nyimbo za kutoka nje, kuliko kuzuia nyimbo na video za nyumbani ambazo uchafu wake Haufikii hata robo ya uliopo kwenye Nyimbo zinazopewa kipaumbele toka nje…

“Hii ni sawa na kuzidi kuukuza mziki wa nje huku tukiudidimiza na kuua mziki wetu… Will the target of reaching our goals ever be achieved?? #Ni_Mtazamo_tu.”
 
Lengo ni kuzuia uchafu au kuzuia kiasi cha uchafu? Haya mambo ya "kufikia hata robo" yanatoka wapi?
Huyu jamaa bana! Reasoning mbovu sana..
Hapo katumia hii opportunity kulalamika kiaina kuhusu kufungiwa ile video aliyovaa t-shirt ya kijinga!
 
Ila asiwe anakeng'enua mijino hivyo noma! Chapati anakunja kweli?
 
Anaiombea kijanja video yake ilitopigwa stop, akajambie mbele huko kwani Bongo tu mbona hata South na Nigeria n.k nao hufungia video zao za ndani kwa kukosa maadili sembuse hizo kunyimwa tuzo. Hata video ya Skibobo ya marehemu Goldie (R.I.P) ft Ay nchini Nigeria imepigwa stop haina maadili tho huku bongo inapigwa tu
 
Diamond hana ujanja wa kuandika hiyo sentensi ya kiingereza!kwani akiandika tu mwenyewe kiswahili bila kuandikiwa hiko ki English na wapambe na madame ujumbe haufiki?
 
Anaiombea kijanja video yake ilitopigwa stop, akajambie mbele huko kwani Bongo tu mbona hata South na Nigeria n.k nao hufungia video zao za ndani kwa kukosa maadili sembuse hizo kunyimwa tuzo. Hata video ya Skibobo ya marehemu Goldie (R.I.P) ft Ay nchini Nigeria imepigwa stop haina maadili tho huku bongo inapigwa tu

Na nyimbo ya Ashawo ( malaya ) ilipigwa marufuku Nigeria lakin nilishangaa Tanzania inapigwa hadi kwenye maharusi na sherehe ata za kitaifa.

Na ile nyimbo imejaa matusi mwanzo mwisho
 
Jamani ya Shilole Chunabuzi ipo kikaangoni. Ni chafu zaidi ya hizo
 
Aliyekuambia ya kuwa kuachivu golz inatokana na kupewa uhuru usio na mipaka ni nani ?

MJ, Bob Marley, UB 40 ,ABBA na wengine wameachivu hizo golz bila ya kuimba wala kuandaa video zisizotazamika na familia.....

......ANAYEJUA ANAJUA TU, MR DIAMOND.....hata ukiimba na kutengeneza video ukiwa umekaa tu kwenye kiti mwanzo mwisho jamii itakuelewa.
 
Na nyimbo ya Ashawo ( malaya ) ilipigwa marufuku Nigeria lakin nilishangaa Tanzania inapigwa hadi kwenye maharusi na sherehe ata za kitaifa.

Na ile nyimbo imejaa matusi mwanzo mwisho

Teh labda lugha na sio hizo tu kuna nyimbo nyingine nchi zao husika hazipigwi ila huku bongo ni kujilipua tu hahaha
 
Aliyekuambia ya kuwa kuachivu golz inatokana na kupewa uhuru usio na mipaka ni nani ?

MJ, Bob Marley, UB 40 ,ABBA na wengine wameachivu hizo golz bila ya kuimba wala kuandaa video zisizotazamika na familia.....

......ANAYEJUA ANAJUA TU, MR DIAMOND.....hata ukiimba na kutengeneza video ukiwa umekaa tu kwenye kiti mwanzo mwisho jamii itakuelewa.

Sawa kabisa, ukiwa na kipaji huhitaji kufanya utumbo ili kuuza nyimbo zako. Mbona Lady Jay Dee anaimba nyimbo zisizo na mambo ya ovyo na anauza sana tu?
 
Back
Top Bottom