Diamond awataka Wapinzani wake kwenye Muziki waongeze Juhudi

Mjanja M1

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2018
Posts
4,058
Reaction score
14,382
Msanii anaetamba na kibao cha "Mapozi" alicho washirikisha Jay Melody na Mr Blue msanii Diamond Platinumz, amewataka wapinzani wake waongeze juhudi maana hawamsumbui kabisa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Diamond ameandika,

"Dah Wapinzani wangu embu jitahidini basi jamani, maana namna hii hata Motisha yenyewe ya game inakuwa hamna sasa!".



Diamond aliambatanisha maneno hayo na chart inayoonyesha anaongoza kuwa na Views wengi kwenye Mtandao wa Youtube.

Nini maoni yako?

Written by Mjanja M1 ✍️
 
Tofauti na hao hapo, wapinzani wake wengine ni akina nani.?
 
Salute kwake.

Aendelee kumaintain top listed
 
Diamond alisema mwaka 2024 atatrend mwaka mzima
 
Aachane na bongo huku tunamjua vya kutosha, apambane huko dunian tumuone kwenye billboard na grammy
 
Na yeye aongeze juhudi amshide Wizikid ,Dacido na Burna boy maana anajuficha kwenye youtube ..lakini alipaswa kupambana kimataifa zaidi …
kuna Local na international musicians.

Simba la masimba anawataka wamatumbi wenzie wapambane
 
Takwimu za kubumba
Huyo d voice nani anamuangalia?
 
Kwa hiyo ile MTV EMA ulichukua ww mkuu???? Au zile stadium shows za kimataifa huwa unafanya ww kiongozi????? Au huko sio international ni mbwinde
Achukue kwan Grammys, ndo tutaona yeye ni bora, hizo tuzo uchwara hata Vanny boi anayo. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Showz za kimataifa zipi zitajee?
 
Achukue kwan Grammys, ndo tutaona yeye ni bora, hizo tuzo uchwara hata Vanny boi anayo. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Showz za kimataifa zipi zitajee?
Em taja MTV EMA aliyochukua Rayvanny, speaking of Rayvanny hizo ni efforts za Diamond pasipo Diamond Ray asingekuwa hapo.

Ukitaka kujua International shows zake ww tembelea IG page ya Diamond huwa anapost then utaleta majibu kuwa zile shows ni International au za muzikimnene
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…