Teh tehSafi nimeipenda hii tena angefanya hata laki 3 kabisa
Nasema hivi kwa sababu ingekuwa ya bei ya chini kila mtu angenunua matokeo yake watu mkitembea mnakuwa mnanukia harufu moja kila mtu kitu ambacho sikipendi
Bora allivyofanya hivyo,wale watanashati tunaojua kutupia tutanunua tu ila wale wazee wakuunga unga waendelee ni spray zao za buku 5 tano
ishi kwa uwezo wako. Wewe huwezi toa.. Ila wapo wanaoweza toa..Kila mtu anakula kwa urefu wa kamba yake..No need to hate.😀😀Yaani nitoe laki kwa ajili ya kunukia tu!?
Kwa tope alilopaka Shilole Kiuno, iyo perfume hata kuipaka kwenye kwato za ng'ombe siwezi...
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji119]Mkuu labda ungeshauri atoe bidhaa kwa watu wote wachini wawe na bidhaa zao za chini na wajuu tuwe na bidhaa zetu za juu (Hahahahah), sema soko la watu wa chini lina masimango sana, usiombe masikini atoe buku afu asiridhike na hiyo bidhaa,
Hyo kuruthumu ya laki moja nan anunueTena unakuta hii yangu ya buku 5 inanukia vizuri kuliko hiyo Chibuku
Tatizo lenu ni kwamba hata kama ninyi ndiye washauri wa huyo bwana basi mtazidi kila siku kumshauri vitu ambavyo sana sana vitamchelewesha kufika akutakako..Utajiskiaje siku upo mbele ya kadamnasi halafu unakuta watu kama 20 mnanukia harufu moja?
Well said na kama mtu ni mtumiaji mzuri wa perfume 100k ni very reasonable.Safi nimeipenda hii tena angefanya hata laki 3 kabisa
Nasema hivi kwa sababu ingekuwa ya bei ya chini kila mtu angenunua matokeo yake watu mkitembea mnakuwa mnanukia harufu moja kila mtu kitu ambacho sikipendi
Bora allivyofanya hivyo,wale watanashati tunaojua kutupia tutanunua tu ila wale wazee wakuunga unga waendelee ni spray zao za buku 5 tano
Diamond hata alipokuwa anafanya tamasha la diamond are forever pale M-City kwa mara ya kwanza kwa kiingilio kikubwa watu walimbeza na kudai kuwa hatopata watu wengi lakini matarajio ya wengi yakawa tofauti kwani jamaa alijaza sana ingawaje kiingilio kilikuwa ni kikubwa sanaTatizo lenu ni kwamba hata kama ninyi ndiye washauri wa huyo bwana basi mtazidi kila siku kumshauri vitu ambavyo sana sana vitamchelewesha kufika akutakako..
Subiri nikupe mfano mdogo tu ambao hata yeye kama atasoma hapa naamini atauzingatia.. Diamond nasikia ana zaidi ya mashabiki Million 2 kwenye mitandao. Kati ya hao almost 90% ni vijana below 30 yrs na kati ya hao 90% ambao ni vijana karibia 70% yao ni wanafunzi na vijana wasio na uwezo/kipato cha kueleweka.. Kwahiyo tunaweza sema 80% ya mashabiki wake sio watu wenye vipato vya kueleweka.. Sasa hauwezi ku ignore 80% ya mashabiki wako udili na 20% ambao pia huna hakika kama watapenda kile unachokiweka mezani kwa sababu mbalimbali, either bei au prestige ya hao mashabiki (unafahamu matajiri wetu wanavyohusudu vya nje).
Sasa tuanze kudili na hao 90% ambao ni almost 1.8 Million ambao kila siku wako kwenye mizunguko either ya kishule au kutafuta maisha. Ukiweka kinywaji ambacho utauza kwa shilling 500 tu na kila siku kati ya mashabiki wako hao 1.8M, asilimia 10 pekee ndio wakanunua (hizi ni estimation za chini kabisa pia tumeignore ambao sio mashabiki na wale ambao hawako kwenye mitandao) kwahiyo angalau kwa siku akawa anauza bottles 180,000 kwa hao watu 180,000 kwa shilling 500/- ina maana kwa siku atatengeneza kiasi cha shilling 90,000,000/-.. Hiyo Turnover ya million 90 kwa siku kwa profit margin ya 10% (mostly common to many fast moving products) itamletea faida ya 9,000,000/- kila siku.. Yaani kila mwezi anakuwa na uhakika wa faida ya Million 270.
Hizo perfume hao 20% wakinunua wanaweza kutumia hata mwaka mzima.. Yaani mtu anapulizia akiwa ana special event/occasion ya kuattend na si kupulizia kila siku akiwa kwenye mizunguko ya kawaida.. Unaweza kuta kwa mwaka faida ya hizo perfumes pamoja na bei kuwa kubwa wala isizidi Million 100 wakati akiweka cheap product ambayo kila shabiki ataafford kama mfano wangu hapo juu anatengeneza Million 270 kwa mwezi mmoja tu..
Sisi wa Tandale na Tandika ni ghali bibie, angefanya elfu 10 tu [emoji1] [emoji1] [emoji1]
Hahaaaaa gud night usiku umekua mwema c kwa mpulizo huu itasubiri sana dukaniHiyo ni bei kwa chupa. Mashabiki wake mpaka leo wananunua perfume kwa mpulizo. Kama mpulizo mmoja 500, ukitaka 4 unalipa 2000
Bonge la ushauri, yan huu anatakiwa aulipieHivi ile clothing line yake aliyoanzisha ya WCB inafanyaje sokoni?
Kama ile ameshindwa hivi kweli perfume nani atanunua kwa hiyo bei? Exposure yote aliyonayo pamoja na kwenda ulaya kila siku bado hajui apart from mziki nini kitampatia pesa matokeo yake yeye kila siku kujaribu jaribu tu mambo.. Mara App sijui ya kuuza mziki, huko hajafanikiwa karukia perfume..
Diamond una jina kubwa sana, clothing line sijui maperfume havijawahi kumtoa msanii yeyote mkubwa hata huko duniani. Tafuta biashara ambayo inagusa matumizi ya watu ya siku kwa siku.. Angalia biashara wanazofanya akina Mo na Bakhressa.. Ushauri tu ebu jaribu hata kutengeneza kinywaji chako, iwe Juice au Soda kama za Azam au Mo hapo utatoboa mara moja maana mashabiki wako wengi ni wanafunzi na watoto wa uswazi ambao hawana kipato kikubwa ukilinganisha na hizo bei unazoweka kwenye bidhaa zako.. Na hata biashara ya Juice mteja mmoja anaweza akawa anakunywa Juice yako angalau mara tatu kwa wiki lakini hizo Perfume na nguo anaweza purchase once in a lifetime.. Akina Pdidy na 50 Cent wao wanatajirikia kwenye liquor sasa wewe si mnywaji basi fanya hata Juice hizo au hata Non-Alcoholic drinks..
Demu wako Wema alikuja na biashara gani sijui lakini pamoja na mvuto wake kwa mashabiki wake alifeli, kuwa tofauti usifate mkumbo na usifanye biashara za sifa (kwamba perfume yangu inauzwa ghali).. Hujafikia level za kutengeneza prestigious products maana mashabiki wako ni watu wa hali ya chini..