Nilikuwa napata elimu kidogo ya kibiashara sehemu, na jambo kubwa lilikuwa namna ambayo Diamond kaja nayo juu ya Perfume yake, nimemfikiria Diamond kwa sababu ni staa kama wanavyoweza kuwa mastaa wa michezo pia wakaanzisha biashara zao.
Swali kubwa lilikuwa bei lakini pia Chapa (brand) aliyoingia nayo sokoni.
1. Bei ya Perfume ya Diamond ni 105000, yaani laki moja na elfu tano. Hii ina maana kuwa wenye uwezo wa kununua hii ni kwa kiasi kikubwa nusu ya wale walioweza kulipa Elfu Hamsini kuingia kwenye show yake Mlimani City. Nasema hivi kwa sababu kwa bei hii kuna brand kubwa Ulaya zenye bei jirani na hiyo ambazo watu wataendelea kuzinunua.
2. Washabiki Wengi wa Diamond ni watanzania. Kipato cha siku cha Mtanzania wa kawaida ninaambiwa hakizidi elfu 70 kwa siku kama tukiamua kukadiria juu sana, lakini wengi wanaishi chini ya Dola 5, yaani elfu 12 hivi. Hii ni changamoto.
3. Biashara ya msanii au staa yoyote ni nadra kuhusishanishwa na kazi yake. Kwa mfano Rihanna viatu vya Fenty vipo chinii ya kampuni kubwa za Puma, sio kwamba hawezi kuanzisha kampuni yake. Air Jordan zipo chini ya Nike, sio kwa sababu hakuweza kuanzisha kampuni, Ronaldo na Pestana Hotels aliingia ubia na wafanyabiashara wakubwa. Msingi wa hili ni kuondoa fikra za watu wanaonuua kuendana na mziki au kipaji chako, ili siku ukishuka ubaki katika soko.
Mikataba ya ushirikiano hii uweka mlinganyo wa kudumu zaidi. Hapa Diamond angeweza kuja chini ya nembo ya kampuni yoyote kubwa, na Fragrance zake zikaitwa hata Armani Chibu, na hii ingefanya Giorigio Arman wafungue kampuni yake nchini.
4. Lakini pia huwa namkubali Diamond kwenye promotion. Sidhani katika hii chibu kama alifanya maandalizi sahihi. Ile amusement na excitement (kufurahia na kuitamani) bidhaa hajaiweka kipindi hiki. Hata yeye mwenyewe hajaonekana katika promo hata kujaribu kuonyesha ina harufu gani, inafaa chumbani kwa namna gani, mtu atafeel vipi akiwa nayo ofisini na mambo mengine ambayo yangevuta wateja wake.
5. Mwisho, bado naamini Diamond ni mpiganaji, kijana wa kipekee na ambaye anajaribu kuleta utofauti wa kufikiri katika kila jambo na kuweka misingi ya fikra za ujasiriamali. Lakini nahisi hili hapa lilichangiwa kwa kiasi kikubwa kuamini katika jina lake kabla ya kufanya utafiti wa walaji wake. Hii ingeambatana na Deodorant na Spray ambazo zingekuwa bei rahisi, angewachota wa Masaki na kwa bibi yangu Magu pale Mwanza.
Mwisho wa siku, bado anahitaji kupongezwa, ni uthubutu wa kipekee huu. Akili yake nimeshindwa kuifananisha na staa yoyote wa Tanzania kwa sasa, katika sekta zote. Hawapo jirani yake, lakini alipoelekea sasa, Menejimenti yake inatakiwa kuwa makini. Uwekezaji huu sio wa muziki sasa, misingi ya uchumi, biashara izingatiwe. Sio kipaji tu huku, ni mahesabu kwelikweli.
Ni mimi mpendasoka Nicasius Agwanda (Coutinho). Nimeandika baada ya kupewa elimu pia.
COPY AND PASTE
Hahahaa daaah kwa bajeti hizi ni hatari tupu hapo hujahesabu na chumba cha kupanga ili ulale kumaliza siku yakoBEI yake ni 150:000/=
1..Sukari hapa kwetu na kwake Tandale BEI kwa kilo... 2600
2.. Unga wa kupikia ugali ( Dona na sembe) kilo moja ni 2000
Dagaa za Mia Nne na hamsini
3...nyanya mbili kila moja BEI yake ni shilling Mia mbili yaaani nyanya mbili ni shilling Mia 400
4.. kitunguu kimoja ni shilling Mia na hamsini ambayo jumla yake ni shilling Mia tatu
5... mboga za majan kupunguza muwasho wa dagaa za mwanza fungu Mia mbili
6... mafuta ya taa kwa Ajili ya jiko langu la mchina kuweza kupata mlo safi kwa siku ni shilling Mia sita
***** Naseeb Domo umetusahau brother
Mwambie atengeneze ata Boflo tule co pafyumu upake ujikute unanukia kama Fenesi[emoji14] [emoji14] [emoji14]Hivi ile clothing line yake aliyoanzisha ya WCB inafanyaje sokoni?
Kama ile ameshindwa hivi kweli perfume nani atanunua kwa hiyo bei? Exposure yote aliyonayo pamoja na kwenda ulaya kila siku bado hajui apart from mziki nini kitampatia pesa matokeo yake yeye kila siku kujaribu jaribu tu mambo.. Mara App sijui ya kuuza mziki, huko hajafanikiwa karukia perfume..
Diamond una jina kubwa sana, clothing line sijui maperfume havijawahi kumtoa msanii yeyote mkubwa hata huko duniani. Tafuta biashara ambayo inagusa matumizi ya watu ya siku kwa siku.. Angalia biashara wanazofanya akina Mo na Bakhressa.. Ushauri tu ebu jaribu hata kutengeneza kinywaji chako, iwe Juice au Soda kama za Azam au Mo hapo utatoboa mara moja maana mashabiki wako wengi ni wanafunzi na watoto wa uswazi ambao hawana kipato kikubwa ukilinganisha na hizo bei unazoweka kwenye bidhaa zako.. Na hata biashara ya Juice mteja mmoja anaweza akawa anakunywa Juice yako angalau mara tatu kwa wiki lakini hizo Perfume na nguo anaweza purchase once in a lifetime.. Akina Pdidy na 50 Cent wao wanatajirikia kwenye liquor sasa wewe si mnywaji basi fanya hata Juice hizo au hata Non-Alcoholic drinks..
Demu wako Wema alikuja na biashara gani sijui lakini pamoja na mvuto wake kwa mashabiki wake alifeli, kuwa tofauti usifate mkumbo na usifanye biashara za sifa (kwamba perfume yangu inauzwa ghali).. Hujafikia level za kutengeneza prestigious products maana mashabiki wako ni watu wa hali ya chini..
Hivi kwani ni lazima nae kiba atoe yake?mbona biashara nyingi tu?ubunifu mwingine utamsaidia kuteka soko lake kiba sio lazima huko alikoenda mwenzakeMmmh... hapa sina la kusema ngoja nisubiri ya kiba huenda yeye akatujali mashabiki wake akapoza bei kdg
Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
Ila unaona fahari ukipita unanukia fragrance ya designer mzungu?!Yaani nijipulize chibu perfume?! Nikipita nanukia watu yuleee ananukia perfume ya chibu! ...ha ha ha
Hizo za laki watu wanazo zaidi ya kumi.Yaani nitoe laki kwa ajili ya kunukia tu!?
Perfume inakaa mwilini au kwenye nguo??Hii pafum ni nzuri sana nimenunua Leo inarufu nzuri Na inaonekana inakaa mwilini vizuri haimsumbui hats yule aliekaa jirani yako kama ile kursumu ya kariakoo
Hii pafum ni nzuri sana nimenunua Leo inarufu nzuri Na inaonekana inakaa mwilini vizuri haimsumbui hats yule aliekaa jirani yako kama ile kursumu ya kariakoo
nilikuwa nadhani ni pesa mingi yenye unaeza nunua nayo shamba. nilipobadilisha kwa currency ya Kenya, nikapata ni pesa moja mbuzi sana.
Yaleyale ya Lipstick 50000Huyu nae sifa zitakuja zimfilisi abakie historia tu.....kipindi shigongo anamdisi kuhusu gharama za show nilimuona kama hater kumbe alikuwa sahihi......toa bidhaa ambayo hata shabiki yako wa kawaida ataimudu....ingekuwa za buku ten au angalau twenty iv tungejichanga.....akanunue mwenyewe na wasafi wenzio.
km huna helà tùlia wacha povuHuyu nae sifa zitakuja zimfilisi abakie historia tu.....kipindi shigongo anamdisi kuhusu gharama za show nilimuona kama hater kumbe alikuwa sahihi......toa bidhaa ambayo hata shabiki yako wa kawaida ataimudu....ingekuwa za buku ten au angalau twenty iv tungejichanga.....akanunue mwenyewe na wasafi wenzio.