Diamond Fanya mziki, achana na 'Janja Janja'

FirstClass

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2016
Posts
1,100
Reaction score
1,363
Nalazimika kusema kati ya mataifa yote duniani, huenda 'waTz' ndio tukaongoza kuwa na watu wenye akili 'ndogo' ama labda tutumie 'hatujatukuka kifikra'..

Sababu za kusema hivi, ni uwezo wetu 'Mdogo' wa kung'amua mambo na kuyatafakali kabla ya kuingia 'Mkenge wazima wazima'..

Yani tunauthamini sana 'Ufake' ama 'kick' kuliko uhalisia. Tumekalia 'kuchezewa' akili kama watoto wa kike. Kitu cha ku-'trends' social media et 'tunapangiwa na watu flani'.. Na sisi bila hata kutafakali, tunaingia wazima wazima.. Upuuuzi


Majuzi tumetoka kuchezeshwa 'Ndomboro ya Soro' na Mzee wa Liquid.. Mara tukamuona Bungeni, hivi ni nani yupo nyuma ya hawa watu. Anatugeuza vile atakavyo.. Apana kwa kweli..

Mbongo fleva, Naseeb Abdul, Chibu Denga, Diamond Plutnum's , kama wengi wanavyomuita, ni mmoja ya vijana waliofanikiwa/wamefanikiwa kuwalisha cha kuongea watanzania..

Kwa tafsiri isiyo rasmi, ni kuwa jamaa
'Ametuweza..' Yani Atupindui. Si wanaume wa Tarime, ama wale wa Dar. Si madem wa kshua, ama wale wacheza visingeli..

Jamaa kwa sasa kila akitaka kuja na bidhaa flani, basi watanzania lazima wapewe kitu flani cha kuandika Mitandaoni. Nao kwa akili yao 'ndogo' watafata 'maelekezo' Toka juu.. Upuuuzi

Majuzi kama sikosei Jamaa alitambulisha ile frequency kwa wanaume wa dar, ila cha ajabu Discussion zikawa ni kumuhusu mzazi mwenzake, yule Mjasiamali aishiye Bondeni kwa Madiba.

Mara tuone yupo na mzee wake, binafsi nikasema 'tayali watz wamepewa cha kuandika'

Ushauri
Kijana aongeze juhudi kwenye kazi, aachane na mambo ya kick. Leo watanzania hawazungumzii tena kazi yake mpya, ila wanachozungumzia ni kile alichosema kumuhusu 'Aliyekuwa mpenziwe'

Pia apunguze kuimba matusi.

Hitimisho
Watz ninyi ndio sababu ya haya mambo ya kick kutrends social media, mkiyapuuza hayatajirudia tena..

Nitoe rai yangu kwa Serikali yangu tukufu, serikali inayojinasibu kuwa ndio serikali ya wanyonge, iweke tozo kwa hawa wanyonge ya angalau mia tatu'300' ili tu ku-acces kwny mitandao ya kijamii.. Hii itasaidia gharama za bando kuwa juu, hivyo kupunguza mambo ya kijinga kutrend mitandaoni.

Pia itasaidia hawa wanyonge kuendelea kuwa wanyonge zaidi na zaidi ili serikali yetu tukufu iendelee kuongoza wanyonge.


Nawasilisha
 
Team kariakoo mnataka.adii balance kuntrend kwny ishuu ambazo haziwahusuu alafuu hata america mbn aya mambo yapooo kila.konaa yapoo bhn uyuu ni msaniii
 
na wew mtoa mada ukiwa mmoja wa wapenda ubuyu
 
Ukiwa masikini utakachojua ni Majungu na Umbea tu
 
Unatoa rai kwa serikali gani?

Rais mwenyewe anapenda ubuyu

Mawazir wake

Hali kadhalika Wakuu wa Wilaya na Mikoa

Wananchi ndo usiseme, Kwa ufupi

Hili ni Taifa Limekaa kiubuyu ubuyu

Linaongozwa ki ubuyu ubuyu tu
hahahahaha Ubuyu's nation is governed by Ubuyu's leaders. Umetuchoka sana sisi tunaojielewa ambao ubuyu tunaona kama wastage of time
 
Amefanikiwa kuwafool haohao.

Kijana makini kama mimi sina mda nae wale upuuzi wake wowote ule.

Wanashabikia huu upumbavu stress tupu hawana pakulala ila wana jero la MBS.
 
Kama mpunga ashaupata mwenzako ac yke inasoma level ya mabilion,ww hpo si ajabu hata laki mbili kwenye ac yko huna
Alafu unataka kumfundisha mtu aliyekuzidi hatua milion 3 mbele

Ova
 
Kama mpunga ashaupata mwenzako ac yke inasoma level ya mabilion,ww hpo si ajabu hata laki mbili kwenye ac yko huna
Alafu unataka kumfundisha mtu aliyekuzidi hatua milion 3 mbele

Ova
Rudia kusoma utanielewa mkuu..
 
Kwenye maisha kuna kitu kinaitwa option hata Marekani pamoja na maendeleo waliokuwa nayo katika nyanja zote vipo vitu vya kipuuzi vinatrend na kupendwa sana,hilo huwezi badili na mpaka wengine wakaamua wajiajili kwa kuwa na vipindi vya reality kama akina kardashian wanapiga hela ila ukiangalia vipindi vyao ambavyo unavyiona ni upuuzi,lakini wanapiga hela na serikali inapata kodi.

Hata hapa JF wameweka jukwaa kama hili la kujadili macelebrity,eventhough kuna majukwaa kama ya intelligence ,international ,siasa ,habari na hoja nk so kama wewe unaona labda maisha fulani ya mtu hayakuhusu achana nayo,ila ukiyafuatilia alafu ukajifanya kuponda jua unayapenda,alafu yatakupotezea mda wako,so hao wengine waache wayajadili sababu huwezi kumtenganisha msanii na umaarufu wake,watu watataka kumjua kiundani na kufahamu kazi zake ndio kazi yake.


Alafu unaoneka una lako kwenye hii nyimbo ya THE ONE hebu nioneshee hata tusi moja.
 
Mkuu kinachokusumbua ni ushamba tu , ukitembea utaona kuwa hivi ni vitu vya kawaida dunia nzima
 
Mbona uliyoyawaza hata mtto wa standard three anaweza kujawaza
 
Mtoa mada naomba ujiunge CCM, kuunga mkono juhudi za mwenyekiti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…