Diamond fata ushauri huu mapema or else!

ma2mbo

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
697
Reaction score
326
Kwanza nianze kwa kuweka wazi mimi ni die hard fan wa Diamond kutoka siku ya kwanza na Kamwambie yake. Tumekuwa tukitoa sapoti kwa kila hali kwa Diamond ambaye ni msanii wa mfano kwa taifa letu.

Ila kinachoendelea sasa mitandaoni kwa kweli sidhani kama kuna shabiki wa Diamond anakifurahia labda asiwe shabiki wa kweli, yani kifupi jamaa anaharibu kabisa image yake na muziki wake kwa ujumla na anatukera mno .

Ata kama uwe umeudhika vipi na maneno ya chinichini ya wapinzani wako haukutakiwa uripuke kiasi hicho... kwa kweli umetoa maneno mabaya sana ambayo hayafanani na Diamond. Uwa simkubali Ommy Dimpoz lakini maneno uliyomtolea ni makali sana kwa mtu kama wewe,

umetukosea sana mashabiki wako na mbaya zaidi Ommy kaenda kukumaliza kabisa kwenye interview Xxl kwani Yeye alienda kuucheza mchezo wake kwa akili nyingi akaiomba huruma kwa wananchi na mwisho wa siku wewe ndio umeonekana mpuuzi... Umeenda mbali zaidi unatoa post za majigambo ya kipuuzi kabisa mtandanon tena ukimuusisha Mungu dah unafeli sana sijui umelewa nini mwanangu!!

Naomba uchukue ushauri huu.
Tuombe msamaha mashabiki wako kwa utoto unaofanya sababu huyu sio Diamond tunaemjua na tunaemsapoti.

Angalia sana kuhusu huyo meneja wako Sallam ni jamaa mzuri kwenye biashara anaijua biashara ila sio mzuri kwenye PR, image anayotaka kukupa sasa hivi sio yako. Diamond ni mpole very innocent asiyependa ugomvi mwenye adabu hiyo ndio image yako sio hii anayokuingiza Sallam.

Sielewi kwa nini Sallam ndio sasa ana take over! Fella yuko wapi? anayaona haya? Kuwa makini sana na Sallam sisi wengine tunamjua toka Forest hill boma road mpaka akibeba pochi la Merei. Ni mgomvi, mpambe mpambe na mchonganishi kwake kuwagombanisha watu sio ishu kubwa.

Linda sana biashara yako biashara yako inategemea image yako kumbuka unayo kampuni Wcb na kuna makampuni yameweka pesa kwenye image yako so chunga sana hao unaowapa kick hawana cha kupoteza wewe una vingi vya kupoteza. Endelea kuwa yule Diamond mpole mwenye heshima kwa wote.

Mwisho kama ulivyonrudisha Kiba kwenye game sasa unamrudisha Ommy Dimpoz pia soon ataanza kushine, uhoni Kama unajitengezea wapinzani wasiokuwa na ulazima?

Diamond tuombe radhi mashabiki wako, futa upuuzi ulioandika mtandaoni achana na Ommy na Kiba usiwape ukubwa kupitia huruma za udogo wao kwako kutoka kwa watu unawapa kiki kubwa sana. Pambania Wcb isimame then msikilize sana Fella na msikubali Sallam awacontrol team nzima changanyeni na zenu kidogo.

Kumbuka kupanda ni kazi ngumu ila kushuka ni dakika mbili tu
ni hayo tu!
 
Jamaa unaakili sana...miye ni fun pia WA diamond.. Msanii wetu katuangusha. Nadhani sallma brand meneja hajui majukumu yake..kazi kubwa ya brand manager ni kutengeza PR nzuri ya msanii kwa mashabiki pamoja na wasanii wenzake...!! Sallam mtoto wa forest Moro.namjua yule.. Mjanja mjanja sana, mtoto wa mjini..! Kesho ntaandika threads kuhusu diamond na sallam... Diamond ajue pia sisi mashabiki tunataka mziki mzuri siyo kujisifia sifia eti mungu anamsaidia mwema..
 
Mwenyezi Mungu akubariki... Ila atakusikiliza?
 
Ni kweli kabisa ulichoandika! Ila kibinadamu inaudhi na inakera sana pale unapotafuta mafanikio mtu mwingine anakuja kubwabwaja tu mbele za watu, kama binadamu wa kawaida lazima nyongo ichafuke!!

Mi nafikiri tumsamehe tu ni sehemu ya maisha asiyekosea ni Allah peke yake!!Amefanya kazi nzuri kuutangaza muziki wetu kweli ifike leo hii hili la ommy lifanye tumurudishe nyuma!!
Nafikiri atajirekebisha asiwe mwepesi wa kupanic ,kwani kulingana na umaarufu alionao loloto atakofanya ndio linasambaa kama alivyo....mfano jana kujibu tu imekua shida
 


Diamond ndio nembo ya bongo fleva kwa sasa anatakiwa aelewe nafasi yake awa watoto wanaotaka mbeleko awaachie wadogo zake kama Kiba anavyomtumia Dimpoz
 
Rick Ross alipoteza mkataba wake na Reebok baada ya kutoa mistari ambayo ilikua ikichochea ubakaji katika wimbo wa UOENO.

Lil Wayne alikosana na mashabiki baada ya kusema I beat the p*ssy up like Emmet Till. Na juzi akawaharibia watu siku aliposema yeye haungi mkono na haoni kama movement ya 'Black Lives Matter' inamhusu.

Kanye West aliwagawa mashabiki alipopanda jukwaani kunyang'anya maiki na kumtaja Beyonce kama aliyestahili kushinda katika tuzo za Mtv.

Image kwa msanii inamatter ila hii naamini ni kwa wenzetu zaidi ndiyo maana wanaajiri professionals kwa kazi hizo, hapa msanii elimu dunia hana lakini kuajiri pros anakua mbahili.
 
Jamaa umemaliza

Naongezea kwa kuwataka kina Fella na Babu Tale waingilie kati hii ishu, Huyo Sallam kama ni mtu wa show za nje aandae ma bif ya kimataifa si vurugu anazo leta hizi, anafeli hapo. majivuno huja kabla ya kuanguka, Diamond huyu wa siku mbili hizi si Diamond wa kila siku.

Kwa kweli ni bora kuwa kimya uwape watu doubt ila kuongea watu wathibitishe kuwa ni mjinga, kama shabiki wa Diamond nime mind sana hii ishu.

*kwenye lugha kali tuvumiliane
 
INAVYOONEKANA WATU MNA VIPAJI SANA VYA UTABIRI NA KUSHAURI - SASA KWANINI NINYI HAMTUMII TABIRI KAMA HIZO KUJITABIRI UTAJIRI ILI MUACHANE NA TABIA ZA AKINA DIMPOZ !! ANYWAY MIMI NIMEUMIZWA NA JINSI DIMPOZ ALIVYOMTUKANA MAMA YAKE DIAMOND KWA BIFU ZAKE NA DIAMOND - NADHANI MWENYE WAZAZ ANAJUA
 
Kufanikiwa katika maisha haina maana wewe ni bora zaidi ya wale ambao hawajafanikiwa.
Diamond amelewa sifa, hivyo anaona wengine ni takataka tu katika Muziki wa Bongo Flavour.

Ameingia kwenye mtego wa maneno yake, amempa Ommy Dimpoz Jukwaa la kupiga hatua zaidi na yeye Diamond kurudi nyuma zaidi.
Muda sio mrefu watu wataanza kumchoka, na hapo ndipo utakuwa mwanzo wa Muziki wake kupotea kabisa.
 
Kiba Shtuka Kumbuka Mashabiki Wako Wengi Ni Wale Anti-diamond, Sasa Inavyoonekana Watahamia Kwa Dimpoz Nyembo Halafu Wewe ukabuma.Kaa Chonjo
 
Mleta thread well said.
Hata asipoomba msamaha na wala asiombe ila arudi kuwa diamond tunaye mfahamu.
Siyo diamond huyu wa kujibu kila kitu na mipasho.
He is on the top lakini kuna msemo wa Kingereza unasema kwamba there is a rise before a fall.
Namkubari sana diamond kwa hustles zake yani from zero to hero ila design sasa ameanza ku loose control anabwabwaja ovyo mipasho mingi personally week hii kanikera sana japo bado mimi fan wake.
Ommy leo kwa mara ya kwanza nimemwona wa tofauti maana siku zote nilidhani yeye ndiye mwenye matatizo sasa after that interview nimeona kumbe sio.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…