Diamond haji kuandika mashairi kama haya tena

Diamond haji kuandika mashairi kama haya tena

Bora umesema wewe mzee baba tungesema sisi tungeitwa Haters.
 
Et anatungiwa? Mondi ni mjanja sana katika Lusaka pesa na kwenda na mida, yani akiamua atoe nyimbo ya Ujumbe huwa anaandika haswaa na akitaka kutoa ngoma ya biashara basi huwa ni mtu Nouma sana ndo mana fan base yake inakua siku hadi siku mfano anapohitaji kuwashika wabongo kwa jumbe nzuri ndo ngoma kama, lalasalama, kamwambie, mbagala, chanda chema, ukimwona, kizaizai , nitampata wapi, je, utanipenda?, nataka kulewa, mapenzi basi, nalia na mengi ila anapotaka kufanya biashara ndo Nana, kidogo, na zngine zngne.. Jamaa ni mjanja sana
 
yaani wasafi sijui huwa wanaimba upuuzi gani.harmonize katoa wimo mzuri ila nenda kwenye mashairi sasa upuuzi mtupu . africa tutabaki nyuma tu

Utakuwa kidot ww sio buree,Wasafi ndo habari ya mjini ukiwaunganisha kwa sasa na kiboko ya Mabishooo.
 
Thibitisha...
Yeye diamond alisema alitunga huu wimbo akiwa kwenye ndege anaenda Uingereza baada ya kuwa wamegombana na wema sepetu...
Kumbe elmagnifico!!! anaweza tu kama ataweza kurudiana na Wema na kuachana tena au we mwenzangu unaonaje
 
Kumbe elmagnifico!!! anaweza tu kama ataweza kurudiana na Wema na kuachana tena au we mwenzangu unaonaje
Hahaha kweli nyimbo nyingi alizotunga akiwa na wema safi sana kama lala salama, mawazo n.k
 
  • Thanks
Reactions: Iza
One of the best song among the best of DP. Hapa hisia ndo zilitawala kwenye uandishi. Na nyimbo zote zilizoandikwa kwa hisia lazima ziwe 'kubwa'.
 
Nyimbo nyingi diamond alizoandika kipindi ana sepenga zilikuwa zimeshiba sana kuanzia melody hadi mashairi....kwa mfano kuna wimbo unaitwa kesho jamaa aliimba sana mule.....
Naweza kukubaliana na wewe, Kuna pia Moyo Wangu
 
Diamond Namkubali KWney Nyimbo kama tatu tu:-Hapa Aliandika Kweli.
1.Mbagala
2.Kamwambie.
3.Nitarejea.
 
Siku anasema,,,
"Mwambie kwetu, usiku kopo na mchana twalala,
Uking'oa usicheze peku, jivalishe ndala"
 
of all the songs, za diamond huu wimbo huwa naukubali Sana.
Mimi sio mshabiki sana wa wabana pua lakin kuna nyimbo zao huwa nazikubali.
Huu wimbo sijawai kuuchoka, to be honest I like the song.
 
Unajiita mbishi na hujui unabisha nini.


Nimekuambia Diamond si mwanamuziki.....tofautisha kati ya mwanamuziki na msanii. Unaweza kulinganisha vipaji vya kina Barnaba Boy, Lady Jay Dee, Banana Zorro na Diamond? Hao niliokutajia ni wanamuziki pure lakini si Diamond japo ana jina kubwa pengine shinda ya hao niliokutajia. Kuwa mwanamuziki si lele Mama, kile ni kipaji na kazi ya watu sema tu kuna wengine wanaiga na kufika mbali Zaidi ya wahusika.
 
Thibitisha...
Yeye diamond alisema alitunga huu wimbo akiwa kwenye ndege anaenda Uingereza baada ya kuwa wamegombana na wema sepetu...


Anaweza kusema hivyo utambishia? Wangapi wananunua nyimbo toka kwa watu na kupata all the rights kisha wanasema wametunga wao?
 
mmmmhhhh
Mungu aliumba dunia mapenzi tangu na tangu
yashanipiga sasa sinabudi nielewe
siwezi kung'ang'ania maana sio fungu langu
japo ni shida ila, nitabaki mwenyewe
ohh ila, mpe shukrani kwa kuniumiza suraya
mwambie mi bado mahututi nauguza kidonda changu
na asisikie asilani, mwambie mapenzi mabaya
hata angali hai Kairuki asingetibu gonjwa langu
kutwa nzima moyo unanidunda dunda (dunda)
sina amani nasaga rumba (rumba)
ohh unani dunda
sema chine tembee moyoo
unanidunda dunda (mamii moyooo)
sina amani nasaka rumba (oohh mimii)
ohh unani dunda
eeeeeeehhhhhhhhhh ukimuona
ukimuona ukimuona
ukimuona ukimuona ukimuona
we nenda mwambie marafiki, marafiki wabaya
tena wengi waongo, wala wasimdanganye
oya ni mashoga rafiki, oohh marafiki wabaya
oooohhhh oooohhh mmmmmhhh
tatizo mi bado, nilipoteleza nkakosa sipajui
mpaka akafunga virago, na akaamua kuondoka sitambui
ubaya, kinacho niumiza, maneno neno maneno
mara kwa ndugu rafiki, kwanini anawapa misemo
najaribu papasa, mbona kwa macho ataona chochote
ila ndo kutwa mikasa, na nazidi kuanguka, niokote
kutwa nzima moyo unanidunda dunda (dunda)
sina amani nasaga rumba (rumba)
ohh unani dunda
sema chine tembee moyoo
unanidunda dunda (mamii moyoo)
sina amani nasaga rumba (ooohh mimii)
ohh unani dunda
eeeeeeehhhhhhhhhh ukimuona
ukimuona, ukimuona
ukimuona, ukimuona
ukimuona

Read more: Diamond - Ukimwona Lyrics | MetroLyrics
Nikweli.
Kwangu Dai hata aimbe vipi lakini kwenye hii alimaliza.
 
Back
Top Bottom