Diamond hakuwaza madhara ya kujiita Dangote

Diamond hakuwaza madhara ya kujiita Dangote

Vipi kama Dangote halisi akaamua kushtaki kwa jina lake kutumiwa na Diamond?
Kwa sababu kidunia, Dangote halisi ni maarufu kuliko Diamond.

Hakuna kesi hapo.

Leta uthibitisho kuwa jina Dangote ni la huyo tajiri na si Dangote mwingine


Yani mimi niamue kujiita Lowasa eti anishtaki,kuna Lowasa wangap(huu ni mfano)
 
Unapokaa mbele ya TV na kuutangazia umma kuwa wewe ni a.k.a Dangote ili hali Dangote halisi yupo, na kwamba Dangote ni brand name ya products za Dangote, basi wewe ni sawa na Huawei kujiita a.k a Sumsung. Sijui unaelewa?
Wakina dangote wapo wengi sana duniani na huyu muekezaji was bingo hana atimiliki la jina dangote
 
mkuu wewe ni samaki wa aina gani..? Mfano uliotoa hauna mashiko kwa sababu diamond ni dangote wanafanya shughuli tofauti za kiuchmi...mbona darasa kwenye wimbo wa muziki amejipa aka ya mbwana samatta au kwa sababu ni diamond.....
Issue ni diamond na wala sio jina la dangote.
 
Vipi kama Dangote halisi akaamua kushtaki kwa jina lake kutumiwa na Diamond?
Kwa sababu kidunia, Dangote halisi ni maarufu kuliko Diamond.
Nadhani wewe ndio unafikra ndogo kama pilton. Hivi haujui Dangote ni jina la kampuni brand name ya bidhaa, kwa hapa Tz Cement?

Ni sawa na leo hii Subaru ajiite a.k.a Toyota.
Acha ubishi usio na maana wewe... kampuni inaitwa Dangote Group na sio Dangote! Dangote ni jina sawa na Kikwete, Magufuli, Trump, Obama n.k!!!
 
huyo anaitwa " Aliko Dangote" , na huyu wetu anajiita "chibu dangote" huoni kama kunautofauti?
Anaweza kujiita hata Aliko Dangote na bado hakuna kosa! Ingekuwa kuna walakini endapo angejiita Dangote Group kwa sababu hii ni registered company
 
Diamond a.k.a Simba a.k.a Dangote, hakuwaza kabisa madhara ya kujiita jina hilo (Dangote). Pengine hakuwahi kufikiria kuwa ipo siku Dangote halisi atakuja Tanzania na kuwekeza. Madhara yake ni kwamba alilitangaza na analitangaza jina hilo pamoja na bidhaa zake, ambapo kwa Tanzania ni Cement, bila hata ya kulipwa chochote.

Au vipi kama Dangote halisi akaamua kushtaki kwa jina lake kutumiwa na Diamond? Kwa sababu kidunia, Dangote halisi ni maarufu kuliko Diamond.

Chonde chonde wasanii na Wanamichezo wetu, achaneni na nick names zenye Vitambulisho vya watu hai.
nadhani ni fursa kwa chibu hii..inabidi aongee na management yake Ione ni jinsi kijana anaweza kuwa ambassador wa Dangote..sallam, tale fanyeni mambo..
Nakumbuka pia dangote alimpa pesa mshindi wa Namba 2 wa big brothers baada ya kushindwa na idriss
 
Nacho jiuliza kwanini wasanii maarufu wa Marekani wakija kutalii Tanzania huwa hawa post chochote kwenye social media zao?

Wasanii maarufu wa Marekani walisha upanda mlima kilimanjaro na kwenda kwenye mbuga za wanyama kwanini huwa hawapost hata picha?

Sio Tanzania tu bali Africa kwa ujumla labda south Africa

Tatizo ni perception zao juu ya Afrika bado zinaexist, they may look charming loving and caring but moyoni bado wana ile ya kuona Africans are not important or classic as they are,so wanafikiri watadharauliwa watakapo jitangaza wako Africa
 
Uwezo wako wa kufikiria ni mdogo kupita kiasi...
Je,anayetumia jina la Dangote ni Aliko Dangote(Bilionea kutoka Nigeria) pekee..?
Au Dangote ni Surname ambayo inatumika na watu mbalimbali kutoka West Africa..?
Pia Dangote ni Surname au ni Jina la Kampuni..?
Majibu ya hayo maswali yatakusaidia sana kufuta UJINGA..!
Acha ku undermine other people's intelligence,ni mawazo yake na namna yake ya kufikiri tena inawezekana we ndo unauwezo mdogo wa kufikiria

Yeye alichokimaanisha pale ni business matters na sio matumizi ya kawaida. Wale watu wawili wote ni business people na wapo kutangaza na kukuza majina yao hivyo haiwezekani kwa bidhaa/brand mbili tofauti kuwa na jina moja linalofanana,unafikiri marketing watafanya vipi?! Hivyo inawezekana mwenye jina halali akaweza kudai jina lake mahakamani ili aweze kumaintain soko la bidhaa zake, au hata kulinda jina lake lisije haribika

Mfano na maelezo ni mengi hayawezi tosha hapa ila inabidi uelewe hiyo ni business matters na sio matumizi ya kawaida,matumizi ya kawaida hata we zaa mtoto mwite Dangote,hawezi kufanya chochote

Kwa mfano kwanini mwanamuziki na mfanyabiashara Kylie Minogue alimpeleka mahakamani Kylie Jenner akitaka abadilishe brand name ya jina Kylie katika bidhaa zake? Akidai kwamba yeye ndo alitangulia kutumia jina hilo kama brand ya biashara zake na ukizingatia sasa hilo jina ni la kuzaliwa na sio a.k.a?
 
Hivi naruhusiwa kujiita a.k.a SISIEMU
 
Wasanii wengi hawajitambui..kidogo huyu diamond amejitahidi kujielewa!

Msanii kama diamond hata anapokunywa maji hadharani ni lazima atoe nembo ya kampuni inayozalisha hayo maji, ie kama ni dasani au kilimanjaro anatakiwa kuficha nembo!
 
Vipi kama Dangote halisi akaamua kushtaki kwa jina lake kutumiwa na Diamond?
Kwa sababu kidunia, Dangote halisi ni maarufu kuliko Diamond.
Dangote ni jina, na diamond katumia kama jina pia, kuna bidhaa yoyote ambayo diamond anauza kwa brand ya dangote? Hivi mbona mnashindwa kujiongeza? ni wapi ambapo Mondi katumia dangote kama brand? kwa hiyo na Mimi nikijiita dewji anaweza kunishtaki?
 
Kwa hiyo mohamed trans anatangaza biashara ya mohamed enterprises na wa kina mohamed woote maarufu wanatangaza bidhaa za mohamed enterprises bila malipo
Upatikanaji wa hayo majina uko tofauti, kwa case ya Diamond yeye alijiita on behalf of Dangote mwenyewe maarufu,hakufikiria jina tu as normal from any Dangote ambae hamfahamu au hakutafuta kwenye dictionary au Quran kama anavyoweza mtu kujiita mohammed bila kumaanisha mohammed trans au enterprise

Infact Dangote ni jina unique sio rahisi mtu kulifikiria na kuliita na ni vigumu kulifahamu bila kuwa na influence na sio jina kama la Mohammed,hivyo hapo inaonesha Diamond alijiita akimaanisha Dangote tajiri. Au we kabla ya kulisikia jina la Dangote kwa Diamond na Dangote Mwenyewe ulikuwa umewahi kuliskia? Au umewahi tena liskia kwa mtu mwingine? Ni sawa na kuskia leo mtu akijiita Kikwete moja kwa moja utarefer ni kwa sababu na ni baada ya kumfahamu mtu maarufu mwenye jina hilo Rais Kikwete,na sio kama utakavyo sikia mtu akijiita Mrisho hutawaza hata ni kwa sababu ni jina la Raisi Kikwete, tofauti inakuja kuwa Mrisho ni Jina common na Kikwete sio jina common
 
Back
Top Bottom