Diamond hana washauri?

mama duamond alizaliwa ndani ya ndoa basi anao wajibu kidini kumuangalia baba yake bt kama ni mwanaharamu(mtoto wa njee ya ndoa) basi mzee hana haki n haki inabakia kwa mama tuu
 
Kwa mtu yoyote ambaye amelelewa kwenye familia yenye wazazi wawili ambayo baba anatimiza wajibu wake ipasavyo.....

Katika familia ambayo asilimia tisini ya mafanikio yako yametokana na juhudi za wazazi wote wawili kwa kila mmoja kutimiza wajibu wake huwezi kumuelewa huyo kijana diamond.....au huwezi kuhisi vile anavyohisi anavyomuona baba yake......

Ila kama umezaliwa kwenye familia ambayo mama yako pekee anatakiwa adamke alfajiri kwenda kutafuta vibarua ambavyo muda mwingine ni za kumdhalilisha ilimradi tu wewe kijana uweze...kula vizuri ,kuvaa vizuri , kulala pazuri na hatimaye kupata elimu nzuri....
Katika familia ambayo kilele cha mafanikio yako yametokana mahangaiko ya mama yako kipenzi aliyelazimika kubeba majukumu ya watu wawili na kufanikiwa kukufikisha hapo.....unamuelewa vyema Daimond na unaelewa vile ambavyo yeye anahisi pindi aionapo sura ya baba yake......

Nina wakumbusha wanaume wenzangu kuwa kuitwa baba hakuishiii tu kwenye kumpa mimba mwanamke bali kwenye kutimiza majukumu yake kama mzazi ambaye kwa namna moja au nyingine anahusika na upatikanaji wa mimba hiyo.....
 
Kama hujawahi kutelekezwa na mzazi huenda ukaona Diamond anamakosa. Lakini kwa waliowahi wanajua uchungu wake. Kuna wakati mtoto anakosa hata hela ya percetamol lakini utasikia baba anahama bar na kuoa kila siku. Hivi baba huyu nae utapewa lawama baadae?

Kwa bahati nzuri, mzazi ambaye hakukulea, hakukujali, alikukana, alikuacha bila kujua utaishije, Hawezi kukupa LAANA abadani. Na hapa ndio maajabu ya Mungu yanapojionyesha.

Lakini pia kuna wakati wazazi wa namna hii wakabaki kua kama somo kwa akina baba wengine.
 
Nawe ungeamua kufikiri basi ungeiona mantiki ya muuliza swali! Je, mtoto ni Diamond peke yake? Jibu HAPANA... mwingine anayefahamika ni Queen Darleen! Je; Queen Darleen anamsaidia baba ake? Kama ndiyo ni kwanini hatumuoni Mzee Abdul akitumia magazeti ya udaku kama kawaida yake akionesha kumshukuru mwanae?! Au nae hamsaidii?! Kama nae hamsaidii ni kwanini hatuoni magazeti ya Shigongo yakiandika habari za Queen Darleen kutomsaidia baba ake?!

One more thing! Hivi ni kwanini issue zote zihusishe magazeti ya udaku? Unataka kusema celebrities wote wa Kibongo wanawajali wazazi wao? Mbona hatuwaoni hao wazee wakilalamika kwenye magazeti ya udaku?

February mwaka huu, magazeti hayo hayo ya Shigongo yaliandika habari za Mzee Abdul kwenda studio ya Diamond!




Haya sasa nisaidie wewe! Global Publishers walijuaje kwamba Mzee Abdul alitaka kwenda Studio kwa Diamond hadi wakafanikiwa kupiga picha zote hizo not mentioning vile walivyofahamu kwamba anaenda hospital hadi wakafanikiwa kuwahi na kupiga picha akiwa bado mapokezi!!!

Ukiamua kufikiri hutachelewa kuona kwamba huyu Mzee anatumika na Shigongo kuuza magazeti yake ndio maana Diamond ana-keep distance na huyu mzee! Ingawaje mimi co Mungu but trust me; Diamond akishajiweka close na huyu mzee atakuja kujuta!
 
hakuna dhambi yoyote hapo, mzazi ana wajibu kumlea na kumtunza mwanawe sasa kama kakataa , kwann yy atunzwe
 
kweli kabisa ilibidi amsamehe. kwani bila yeye diamond asingekuwepo. me naomba diamond amsamehe mshua. ampeleke hospital. mungu atamjalia zaidi na zaidi. rihanna nae alikuaga name bifu name baba yake ishu Kama hiyo lakini akamsamehe had I Leo mzee anakula bata maisha matamu
 


Mimi nimeanza kupata wasiwasi kuona Al Qaeda wameingia humu JF, jamani tujihadhari sasa!
 
Anayejua baba wa mtoto ni MAMA pekeyake,inawezekana huyu ni baba wa bandia
 
Usituletee ujinga hapa, kwamba uislam ni dhaifu kiasi hiki, kwamba mwenye wajibu ni mtoto kwa Baba lakini Baba hawajibiki kwa lolote kwa mtoto ?????
 
Mimi nimeanza kupata wasiwasi kuona Al Qaeda wameingia humu JF, jamani tujihadhari sasa!
Hajui chochote kuhusu dini kajiandikia tu,kwanza kwa mujibu wa hiyo dini yake mtoto wa haramu (nje ya ndoa ) hawajibiki kwa lolote kwa Baba,angalau angeongelea kibinadamu angekuwa na pointi si dini. Mtoto wa haramu ni mali ya mama kwa mujibu wa hiyo dini yake na mtoto hapati dhawabu (malipo kwa mungu) kwa kumuhudumia huyo Baba, na hapati dhambi kwa kutomuhudumia. ( KUMBUKA MAMA DIAMOND NA HUYO BABA HAWAKUWA WAMEOANA)
 
Unainukuu Quran kwa mambo ya kipuuzi,halafu unakariri vifungu dhaifu ili wenye dini yao waione kuwa inamapungufu sana ili iweje, wabadili dini au .......... acha kuishirikisha dini kwa mambo ya kipuuzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…