Diamond hana washauri?

Diamond hana washauri?

wewe umepata malezi ya baba
wengine hatujapata
tunaona sawa tu, huwezi kumuonea uchungu mtu ambae hujui uchungu wake....
haiwezekani.. cjui nyie mliopata malezi nao
SIO SAWA Mie Sijapata Malezi Ya Mama Alitukimbia Nikiwa Na Miez Minne,,,,so Does That Justify Me Nt Helping Her Out When Im Succesful And She Is In Need Psshit Again SIO SAWA
 
Diamond..anafanya safi sana ivyooo.Ni Bonge la fundishoo.kwa wanaume wanaozalisha kisha kuendekeza Michepukoo Na kuacha watoto wakihangaika kwa kuuza ndizi Na biashara kichwani kwenye juaa Kali huku baba Yupo anapenda Raha akifuatwaa Ni matusi Na kipigoo..Tell you what???? Through Diamond many Dadies will learn how to care. Baba D..learn a lesson....God pays!!!
 
Basi kamsaidie wewe ka unaona mwamae ni hivyo. Kutoa misaada ni baraka, usisahau kututumia picha haswa zile utakazomkuta yupo poa sio ka za kuact ili awekwe magazetini.
 
Wacha apate fundisho huyo mla mirungi! Mtu umemkataa miaka yote lakini leo hii unataka care kulingana na mama yake aliye hangaika nae hadi alipo fika sasa...
 
Kabla ya kupost jiulize kwanza kisha upost, usikurupuke hao ndugu zake umewahi kuwasikia?na je hali zao kimaisha zikoje? Usiteteee ujinga hivi anwezaje kutoa m3 kwenye birthday ya rafiki akashindwa kutoa laki mbili Kwa ajili ya matibabu ya baba take ambaye alikatika mpaka akatokea yeye?
" Baba na mama ni Mungu wako wa hapana duniani"
Hivi huyu Baba Diamond alipo uza nyumba kariako kwanini alishindwa kupeleka hata Tsh kwa mama D ikasaidia malezi?
Huyu Baba acha anyooshwe ni mjinga sana.
 
Diamond..anafanya safi sana ivyooo.Ni Bonge la fundishoo.kwa wanaume wanaozalisha kisha kuendekeza Michepukoo Na kuacha watoto wakihangaika kwa kuuza ndizi Na biashara kichwani kwenye juaa Kali huku baba Yupo anapenda Raha akifuatwaa Ni matusi Na kipigoo..Tell you what???? Through Diamond many Dadies will learn how to care. Baba D..learn a lesson....God pays!!!
Michepuko sio tatizo.....kuna wa2 wanamichepuko ila hom full raha mpka mke akiambiwa baba flan anakimada haamini.....huyo baba alikua na uwezo enzi zake saa hii kachoka kma teja kutumia waandishi makanjanja kumchafue chibu ila ndio anajimaliza mwenyewe.....istoshe lazma anawatoto rundo ila chibu ndio mwenye kisu
 
Ubaba sio kuweka mbegu tu na kukimbia..ubaba ni pamoja na kulea mtoto na kuhakikisha anatimiza ndoto zake!
Hivyo basi kama mama ndio alipigana..''mama yake ndio baba yake"
 
Iko hivi, kuna baadhi ya wazazi wakitengana halafu mmoja akabaki na jukumu la kulea mtoto peke yake, huamua kumjaza sumu kikwelikweli na kauli za vitisho kibao. Mfano: "ukimsaidia babako hata mia, zikupotee mia mara elfu. Yaani chochote utakachotoa, mara elfu nimesema kipotee" Hiyo ni laana. Na kama wewe nunda, jaribu kumpa huyo babako hata kwasiri kama hujaisoma namba. Na changamoto inakuwa kubwa pale ambapo huyo mtoto alipopata akili alikufuata kukuomba mahitaji kama daftari, nguo za shule, ada ukamtolea nje kwa kebehi na nyodo. Sasa basi, yakuambiwa na mama + aliyojionea = utanikoma siku nikizipata. Sasa mtoto kapata, baba unataka kubadili formula. Poa nimekusamehe fadha, haya chukua time, maana hakuna namna inabidi uchukue time tu. Malipo duniani, akhera hesabu tu.
 
wewe umepata malezi ya baba
wengine hatujapata
tunaona sawa tu, huwezi kumuonea uchungu mtu ambae hujui uchungu wake....
haiwezekani.. cjui nyie mliopata malezi nao
unaweza ukawa haupo mbali na ukweli,mana hata mimi nimelelewa na mama pekee na baba yupo hai mzima hadi saiv,nilimtafuta mwenyewe tuna mawasiliano hafifu,imagine neno baba halipo kwenye misamiati yangu mdomoni,me hii issue ya diamond siipi u-serious kivile na hainitouch sana.bado najaribu kufikiria mtu alikutosa ukiwa mdogo saiv umekuwa mkubwa na tajiri ndo umsaidie,anaweza kumsaidia kama binadamu tu lakini sio kama baba ambae utajisacrifice kwa ajili yake,na mwisho wa siku upendo haufosiwi yani ndo ipo hvyo tuu.
 
Kwa mtu yoyote ambaye amelelewa kwenye familia yenye wazazi wawili ambayo baba anatimiza wajibu wake ipasavyo.....

Katika familia ambayo asilimia tisini ya mafanikio yako yametokana na juhudi za wazazi wote wawili kwa kila mmoja kutimiza wajibu wake huwezi kumuelewa huyo kijana diamond.....au huwezi kuhisi vile anavyohisi anavyomuona baba yake......

Ila kama umezaliwa kwenye familia ambayo mama yako pekee anatakiwa adamke alfajiri kwenda kutafuta vibarua ambavyo muda mwingine ni za kumdhalilisha ilimradi tu wewe kijana uweze...kula vizuri ,kuvaa vizuri , kulala pazuri na hatimaye kupata elimu nzuri....
Katika familia ambayo kilele cha mafanikio yako yametokana mahangaiko ya mama yako kipenzi aliyelazimika kubeba majukumu ya watu wawili na kufanikiwa kukufikisha hapo.....unamuelewa vyema Daimond na unaelewa vile ambavyo yeye anahisi pindi aionapo sura ya baba yake......

Nina wakumbusha wanaume wenzangu kuwa kuitwa baba hakuishiii tu kwenye kumpa mimba mwanamke bali kwenye kutimiza majukumu yake kama mzazi ambaye kwa namna moja au nyingine anahusika na upatikanaji wa mimba hiyo.....
mkuu umeongea facts,kuna wengine hawajui situation ipoje kiuhalisia kwa sababu wao walipewa malezi na wazazi wote wawili,mimi nimelelewa na mama pekee,mama yangu anajiheshimu sana lakini amewahi kuwa bar maid ili sisi wanake tupate mahitaji,kifupi kahustle sana.dingi nimekuja kumtafuta na kujuana naye miaka mi3 iliyopita,lakini honestly sina upendo naye,hata nisipowasiliana miez miwili me naona sawa tuu.nahisi hata akihitaji msaada wangu ntamsaidia kwa nafasi yangu coz siwezi jisacrifice kwa ajili yake.ipo hvyo yani
 
wewe umepata malezi ya baba
wengine hatujapata
tunaona sawa tu, huwezi kumuonea uchungu mtu ambae hujui uchungu wake....
haiwezekani.. cjui nyie mliopata malezi nao
Baba anabaki kua baba kukusaidia au kutokusaidia hakuondoi uhalali wakutokua babako
 
M wa pili
me wa tatu,hata kuita hlo jina sijawahi na sifeel comfortable kabisa kumwita mtu yeyote (awe biological father au mtu mwenye umri na sifa nyingine za kuitwa baba) nawaitaga "mzee" mzee=baba.
 
Kwa hili la Baba, Diamond ameshapewa ushauri na watu wengi sana ila inaonyesha kuna jambo la ziada linalompa shida kutekeleza ushauri ambalo wengine hatulifahamu. Kama aliweza kumpa msaada mtu baki kama alivyompa Gari marehemu Gurumo, kwa nini inakuwa shida kwa baba yake.
Angeweza akampa msaada kama mtu tu wa pembeni mwenye Uhitaji.
Nahisi ugomvi wamama ameamua kuuhamisha kwamtoto hapa naona bimkubwa amempa jamaa kiapo asijarib kumsaidia mshua ila kitu nyuma yapazia
 
bushlawyer
Unachosema hakika ni sawa na ndio wajibu wa mtoto kwa wazee.
Ila mimi ninataka kujua zaidi juu ya nani mzee au mzazi kwa mujibu wa aya hizi na hadithi hizi ?
Tuchukue mfano wazee wawili wamepata mtoto na mara baada ya kuzaliwa baba mzazi anakimbia nyumba..haonekani na hataki kujua habari za mtoto wala mkewe . Miaka inapita mama anaolewa na yule mtoto analelewa anatuzwa anasomeshwa na baba wa kambo.....na yule mtoto anafikia kumwita yule ni baba ...na ndio mzee wake alembeba kumpeleka hospitali ...ndio mzee wake alombadilisha nepi za mkojo....Sasa suala hapa nani ni mzee...yule alotia tu shahawa na kutungisha mimba au huyu alopata tabu za kumlea mpaka akafika umri mkubwa?
Quraan inasema nini kuhusu hili? Au hadithi zinasemaje...juu ya tafsiri halisi ya mzee?
Tusimhukumu diamond ...moja kwa moja hali yake ipo kama hivo...tupate tafsiri sahihi ya nani mzee hapa au jee huyu ni baba? .. baba alijitokeza baada kusikia kuwa diamond ni mtoto wake na amekua almaaruf.
Huyu bado ni baba ?
 
Mnao mlaumu Diamond hamjapitia aliopitia ,ndio sio vizuri anavofanya but muacheni mungu ndie hakimu nyie wenyewe mna dhambi ngapi ambazo hatuzijui
Fanyeni yenu waachieni mambo yao ya kifamilia
Wanaume ishini vizuri na wapendeni watoto wenu huwezi jua atakua nani baadae
Hata km umeachana na mama ake be there kwa ajili ya mtoto wako
Ndo kinachomtesa sasa hv baba Diamond anatafuta simphathy kwenye social media
Kutokamjali bado hakuondoi haki yakua baba hapa naona bi mkubwa kamzuia mond
 
mimi namchukulia huyu mondi kam wapenda sifa wengine waliopita...siku zote mzazi akosei...mondi kalewa misifa anayoipata kwenye mitandao ila akae akumbuke kuwa huwezi kuwa bingwa milele siku moja utashuka ili apande mwingine...mafanikio ni kama gari la abiria...kila mtu atapanda...wako wapi wakina mr.nice (mzee wa kuku kapanda basikel) yuko wapi tid (mzee wa zeze) wote walipanda gari la mafanikio wakalewa umaarufu wakafanya mambo ya kijinga mwisho waka zima kama taa...joks maana ya mond hayanihusu
mkuu umeenda nje sana ya mada,mzazi hakosei? kuna wazazi wanawabaka binti zao,je na wao hawakosei? sema mkuu umeongea mengi ya moyoni ambayo ni OP ndo tatzo.
 
mkuu umeongea facts,kuna wengine hawajui situation ipoje kiuhalisia kwa sababu wao walipewa malezi na wazazi wote wawili,mimi nimelelewa na mama pekee,mama yangu anajiheshimu sana lakini amewahi kuwa bar maid ili sisi wanake tupate mahitaji,kifupi kahustle sana.dingi nimekuja kumtafuta na kujuana naye miaka mi3 iliyopita,lakini honestly sina upendo naye,hata nisipowasiliana miez miwili me naona sawa tuu.nahisi hata akihitaji msaada wangu ntamsaidia kwa nafasi yangu coz siwezi jisacrifice kwa ajili yake.ipo hvyo yani
Unafanya vyema utamtambua kama baba mana huwez nunua mwingine pia kama inaweza kumsadia mpe usimhukum japo hutampa favour kama mama nadhan atajutia mwenyew nawew utakua huna hatia kuliko kufanya kama mond ya hatakumtambua hatak hii sio sawa baba nibaba hatakama alitaka kukuua mungu atakulipia
 
Although mambo ya ngoswe kuitwa ngoswe tumuachie ngoswe mwenyewe lkn as per Islam, baba halali ni yule aliemuoa mama mtoto kabla! Nahisi kwa issue hii is not applicable sababu mama ndio ana jukumu na mtoto wake!
 
Katika hili la mzazi wake wa kiume mimi binafsi limenigusa hasa kwa imani yangu ya dini. Siwezi kuhukumu moja kwa moja kwa maana sijui chanzo cha ugomvi wao wala status yao kwa sasa na pia MIMI SI HAKIMU, lakini nina haki ya kutoa maoni yangu hasa kumsaidia pia diamond ajitambue.

Katika hali ya kawaidia inatakiwa ingekuwa rahisi kama mzazi wako anapata msaada wako by then kila siku awe analalamika au tunamuona kwenye mitandao huo tayar ni udhaifu wako wewe mtoto kwa kuruhusu mzazi wako awe anakutia aibu wewe au familia yenu kwa ujumla. Kwa namna yoyote ni lazima suala la wazazi wako ukalipa umuhimu mkubwa sana katika maisha yako.

Katika mafundisho ya dini yanatufunza nini kuhusu wazazi?

Hakika ametakasika yule ambaye amewajibisha na kuamrisha wema na kutimiza haqqi na kuiegemeza kwa kila anaestahiki na akawajibisha haki kwa wazazi wawili, na ikawa ni amri iliyoenea kwa walimwengu wote. Hakika ameamrisha ALLAH tabaaraka wata’la katika aya nyingi kuwafanyia wema na ihsani wazazi wawili.
Mfano wa kauli yake aliposema:

{وَقَضَى رَبُّكَ أَلاَّ تَعْبُدُواْ إِلاَّ إِيَّاهُ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَاناً إِمَّا يَبْلُغَنَّ عِندَكَ الْكِبَرَ أَحَدُهُمَا أَوْ كِلاَهُمَا فَلاَ تَقُل لَّهُمَا أُفٍّ وَلاَ تَنْهَرْهُمَا وَقُل لَّهُمَا قَوْلاً كَرِيماً* وَاخْفِضْ لَهُمَا جَنَاحَ الذُّلِّ مِنَ الرَّحْمَةِ وَقُل رَّبِّ ارْحَمْهُمَا كَمَا رَبَّيَانِي صَغِيراً}
Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa hishima. Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea huruma. Na useme: Mola wangu Mlezi! Warehemu kama walivyo nilea utotoni.


Akaamrisha ALLAH tabaaraka wata’la ihsani kwa wazazi wawili katika namna zote za wema, nao ni katika kauli [unapozungumza nao] pale aliposema [basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa hishima]. Vivyo hivyo kuwafanyia wema katika matendo; kimwili na kimali kwa kauli yake aliposema: (Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea huruma).
Na akanyanyua ubora wanapofika katika hali ya uzee, kisha akakataza kuwavunjia adabu na kuwatusi, achilia mbali kuwaacha wakiteseka.

UWAJIBU WA KUWAFANYIA WEMA WAZAZI WAWILI:

Hakika ameamrisha Allah tabaaraka wata’la, na akawajibisha kwa njia ya wasia kuwafanyia wema wazazi wawili katika aya nyingi za qur’an. Pale ilipokuja amri ya wazi juu ya kuwatii, aliposema:
وَوَصَّيْنَا الْإِنسَانَ بِوَالِدَيْهِ إِحْسَاناً
Na tumemuusia mwanadamu awatendee wema wazazi wake wawili[1]


Ikaonesha wazi kuwa kuwafanyia wema wazazi wawili ni jambo la wajibu kwa kuwa ni wasia wa Allah kwetu. Bali akaliambatanisha jambo hilo la kuwafanyia wema wazazi wawili na twaa’ yake Allah tabaaraka wata’la pale aliposema:

وَقَضَى رَبُّكَ أَلاَّ تَعْبُدُواْ إِلاَّ إِيَّاهُ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَاناً
Na mola wako mlezi ameamrisha kuwa msimuabudie yeyote isipokuwa yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema.[2]


Na kauli yake aliposema:
وَاعْبُدُواْ اللّهَ وَلاَ تُشْرِكُواْ بِهِ شَيْئاً وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَاناً
Na mwabudieni Allah wala msimshirikishe na chochote, na muwafanyie wema wazazi wawili.[3]


Zikakusanya aya mbili hizi kuwa kufanyiwa wema wazazi wawili ni haqqi yao, bali akaifafanya haki hiyo kuwa ni ya pili baada ya tawheed yake Allah tabaaraka wata’la akionesha ukubwa wa jambo hilo [la kuwafanyia wema].

Amesema Al qurtwubiy [Allah amrehemu], kauli ya Allah “Na wazazi wawili kuwafanyia wema [ihsani]” maana yake ni:
برهما وحفظهما وصيانتهما وامتثال أوامرهما

Kuwafanyia wema na kuwahifadhi, kuwatunza na kutekeleza amri zao.


Katika kulisisitiza hilo, mpaka ikawa [wema kwa wazazi wawili] ni wenye kutangulizwa mbele hata kabla ya Sunnah za kujitolea kama vile Sunnah za kabla ya swala nk. Na kwa hili akaweka imamu muslim [Allah amrehemu] mlango katika swahih yake akiuita:
باب تقديم بر الوالدين على التطوع بالصلاة وغيرها

By the way mimi nimekubusha tu. Kama ni kweli mzazi hapati msaada basi ajitahidi kumsamehe, kama anapata msaada ila ndio umaarufu basi Diamond anisemehe maana binadamu tumeumbwa kukOsea. Na huu ni mwezi wa toba hakika atakuwa amenisamehe.

Asante.
ahsante kwa speech nzuri mkuu@lakini tambua al-kisasu khak ni haki ya kila mtu kulipiza kisasi hakuna ubaya wa kulipa kisasi ktk dini@ kama alikutenga na wewe mtenge tu LAKINI sio alikutenga wewe ukampiga vita......ni khaki yake kulipa kisasi kwa uadilifu N.B vizuri kusamehe
 
Back
Top Bottom