Diamond hapaswi kujiita Simba - Darassa

mr gentleman

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2012
Posts
3,222
Reaction score
4,689
Msanii wa bongo fleva Darasa ameweka wazi ule mstari wake wa "sio simba, sio chui, sio mamba" kwa kusema Diamond hakupaswa kujiita simba kwani simba ni mnyama ambaye anaweza kuuliwa anapozidiwa nguvu.

Akipiga story kupitia eNewz Darasa amesema Diamond ni msanii ambaye amehangaika sana kutoka kimuziki hivyo mafanikio yake na uwezo wake wa muziki alitakiwa ajiite jina lingine kwa kuwa Daimondi ni zaidi ya Simba kwa sasa kwani ni zaidi ya mnyama Simba.

"Ningekuwa Diamond nisingejiita simba, ninavyomuona Diamond ni zaidi ya Simba, kuna watu wanaua simba, simba, kajichanganya, kaingia kijijini kapotea, Diamond kwa kitu anachofanya ni zaidi ya simba, angeweza kujiita jina lingine lolote kubwa, kafanya vitu vingi sana". Amesema Darassa


Darassa amemalizia kwa kusema wanyama wote ambao amewataja katika wimbo wake hawaogopi kwa kuwa ana kitu kikubwa ndani yake na yeye ni mwanaume na anajiamini kwa muziki wake anaofanya.

"Kwa upande wangu nimesema siyo simba, siyo chui siyo mamba, mamba ni mnyama anayetisha sana kwenye maji, simba anatisha sana porini, chui ni hunter mzuri, so katika vitu vyote ambavyo viko humo, mimi humo kote simo, ninacho kitu ambacho kinaweza kunifanya nikwambie aaaaah". Amemalizia Darassa
 
Ameongea kwa akili, kuna mashabiki wa Diamond walimkubali baada ya wimbo wa Muziki, jinsi alivyompamba inamhakikishia kuendelea kuwa na hawa mashabiki.

Naamini angeulizwa anamuonaje hasimu wa Diamond kimuziki bado angemsifia ila kwa levo yake.
 
Watamuingiza wasafi sasa hivi....ili wamcontrol kwa sababu anakuja kwa kasi ya treni.
 
hongera sana darasa majibu yako yako vizuri sana
 
Kajieleza vizuri sana,ila hapo aliposema "angetafuta jina lingine kwa vile Simba watu wanauwezo wa kumuua" Nadhani kasahau kuwa hakuna kitu kilichoshindikana kuangamizwa na binadamu,hata angejiita ANAKONDA.
 
kwa wale wanaosoma 'taito' pekee watapovuka hapa.
 
Basi ajiite bomu la nuclear , likilipuka,Binamu hawezi kuliangamiza kabla halijammaliza .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…