Diamond hawiki Clouds fm bali wasanii wa Fiesta

mwanamabadiliko

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2010
Posts
938
Reaction score
1,540
Jamani nini kinachoendelea clouds FM na wasanii wa fiesta? Wanakuwa promoted kupita kiasi, interview za kutosha , nyimbo zao zinapigwa kila saa, nyimbo zao zipo juu katika chati ya top 10. Ni kweli kuna upendeleo wa wazi kabisa.

Diamond nyimbo yake ya Salome hata katika top 20 ya nyimbo bora Clouds fm haipo, kidogo kidogo ndo ipo nafasi ya 17 inakaribia kuondoka. Nyimbo zake hata za Ali Kiba hazipigwi kwa wingi na wala hazishiki chati katika radio Clouds. Radio nyingine nyimbo za Salome, Aje za Ali Kiba na Diamond zipo chati za juu.

Kwanini mnapendelea, au mnataka kumshusha Diamond? Iweje nchi za nje na mtaani nyimbo za wasafi zinapigwa wakati wote na wala si katika kituo cha clouds, ambako wakina Maua Sama na darasa ndo wanashika nafasi za juu , na kina mboga saba. Hii ni aibu!

Kama nimekosea au mtazamo wangu unaegemea upande mmoja, nikosoe kwa coments na hoja kali, labda hili suala nalitafsiri vibaya.

Mungu Ibariki Tanzania mungu wabariki wasanii wetu wote, HAKI SAWA KWA WOTE
 
Fiesta Dar, napendekeza hawa jamaa kiba na mond wasusie lishow lao hilo!
 
Kwani wasipompiga wanamshusha?
Au yeye yupo kwenye fiesta?

Wakiweza kumlipa Nov naamini atatumbuiza Dar.
 
Huyuu jamaa mimi nilisha sema sio redio na tv za huko bongo zina mbebaa..!! Sikiliza redio station za mikoani ndo zina mpa kiki sanaa ndo utajua nini nasemaa....!!
 
Diamond ana mkataba na vodacom, fiesta clouds wapo na mkataba na tigo. Ni upepo tu wa fiesta ndo maana promotion imekuwa kubwa kujaza show na kujitangaza mikoani. Bila promotion ya kutosha mashabiki watakuja wachache uwanjani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…