Wakuu Salaam Sana.
Nimejaribu kusikiliza mahojiano ya diamond kwenye kipindi cha Jahazi kazungumzia suala la TRA kwenda kumdai kodi ilihali yeye kama msanii akiwa bado anadhulumiwa haki zake hasa kataja kipengele cha caller tunes wanachopoteza mapato yao mengi kama wasanii, tukumbuke alifikia kuongea hadi kwa jazba kua serikali isiwalazimishe kuhamia vyema vingine, mimi binafsi nimemuelewa sana kwani Ni muhimu serikali kuandaa mazingira Rafiki ya kibiashara ili Biashara ziwe rahisi na wao wakusanye mapato ya kutosha.