Paula kilaki
JF-Expert Member
- Jun 26, 2014
- 1,909
- 1,290
Hizi timu zinakoelekea kubaya... Huenda sisi mashabiki tunajenga au tunabomoa kabisa.
Kama Diamond alipost hii picha kwa kumjibu Alli kiba zile picha za watoto au kuwajibu wanaomwita MGUMBA.... ALIKOSEA SANA.
Kama kweli kasababisha kwa Zari , hakukua na haja kabisa ya kuanza tapatapa. Angetulia tuli ,, ije ituchukue kama bonge la surprise. Sasa hapa kashawapa ulaji waganga.,, haters watafanya lolote wawezalo. Sijui.
Yes honey angalia vizuri hiyo picha kapiga zari (kuna kidole cha kike hapo) akamtumia mondi,Mondi naye akaturusha roho.
Kama zari akijifungua kweli mie nitasubiria wakati wa matokeo ya DNA
Kwanini mumy?huamini kama mondi anaweza kuzaa na mrembo Zarinah?
Diamond mbona anaandika kiingereza cha kishamba namna hii jaman?? Yaani haya mambo ya kukulia maisha ya kayumba na baadae kuja kujidai mtu una swaga ni mambo mabaya sana
Naona kama anadanganywa haiwezi kuwa kweli ila ngoja tusubirie
kweli kabisa, hapa dogo kaanguka kabisa wala sio kuteleza, nadhani amepost kukata vidomo domo vya watu lakini hakufikiria vizuri ndio maana naona kama alipanic flani, haukuwa muda sahihi kabisa wa kuweka haya mambo hadharani.
Wanaotumia kichwa kufikiri badala ya matumbo walishajiuliza, miongoni mwa mademu ambao Chibu amepitia kv Wema, Jokate, Penny, Wolper, Najma na wengine sawa na wao ni nani miongoni mwao tumepata kushuhudia au kusikia amebeba mimba kutoka kwa wanaume wengine ambao wameshiriki nao... tukimchukua Wema ambae tunaweza kusema ni Bi. Mkubwa; kabla ya kukutana na Chibu amekuwa na uhusiano na Kanumba, Charlz Baba, Mwinyi, TID na Mr. Blue... je, huko kote Wema ameacha watoto wangapi!? Mtu akipata jibu na akaendelea kutumia akili zake sawa sawa ndipo anaweza kuhoji wal wanaosema Chibu hana uwezo wa kumpa mwanamke ujauzito wanatumia vigezo ikiwa wanawake wenyewe ndo hao, wamepita huku na kule lakini hatujawahi kuzisikia hizo mimba... mtu anayetumia akili yake sawa sawa anaweza kuhoji hivi miongoni mwa hao mademu tuliowataja hapo juu ni nani iongoni mwao anaonekana kwamba yupo tayari kuachana na ujana akaanza kulea!!!!Ukweli anaujua Mwenyezi mungu kama anauweza wa kumpa mtu ujauzito au laa,na vile vile nimapema sana kusema kama hazai kwani umri wake bado na sidhani kama linamumiza kichwa hilo kwa sasa zaidi ya mziki......
Naona kama anadanganywa haiwezi kuwa kweli ila ngoja tusubirie
Zarinah kwa mondi ni bomu linalosubiri kulipuka.Yule mama ana malengo yake usimuone mjinga au labda kakolewa na mapenzi.
Let's wait then....
Nawaza kama wewe...
Upuuzi mtupu! Hili jukwaa ni shidaaa! Ngoja nirudi zangu!
Hapana msifikilie hicho zari ana upendo wa dhati nachoamini ndio maana kaamua kuzaa naye! Kwa nn asingezaa nao kabla ya daimond. Kwa jicho langu naona zari anampenda zari kwa dhati kabisa
Zari amezaa na Diamond lini na wapi?