Diamond Kuvuka Boda Hadi Marekani Texas

Diamond Kuvuka Boda Hadi Marekani Texas

Ibrahim300

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2010
Posts
390
Reaction score
68

July 26 mwaka huu, wasanii wengi wakubwa Afrika kutoka katika mataifa ya 17 watakutana Dallas, Texas, Marekani kuhudhuria utoaji wa tuzo za kiafrika zinazojulikana kama ‘AFRIMMA Awards', na tayari Diamond Platinumz tayari ameshaonesha uthibitisho wa kuwa katika daftari la mahudhurio siku hiyo.

Diamond amepost kwenye Instagram video inayomuonesha akifanya promo maalum iliyoandaliwa na watayarishaji akiwaambia mashabiki kwa swag za kimarekani kuwa atakuwepo siku hiyo, na kisha akaisindikiza na maneno yanayosomeka, "Yess! i'll be ryt there....Afrimma Awards 26/07/2014 Texas, Dallas (USA)."

Tuzo hizo zilizoandaliwa na Big A Entertainment na African Muzik Magazine, zimelenga katika kuwatunuku wasanii mbalimbali wakubwa wa Afrika waliopo duniani kote na itagusa nyanja mbalimbali za burudani ikiwa ni pamoja na wasanii wa muziki, wachezea santuri aka Dj's, watayarishaji wa muziki, mameneja na watu wanaousapoti utamaduni wa Afrika.

Tuzo hizo zinatarajiwa kusindikizwa na vicheko vya mara kwa mara kwa kuwa mshereheshaji wa shughuli hiyo ni mchekeshaji maarufu wa kimataifa, The Basket Mouth na atakuwa na muigizaji mrembo wa Nollywood, Juliet Ibrahim.

Stori: bkuHABARI
 
Natumai Diamond atatuchekesha na sisi kama vile Nigeria alipovalia kile kisuruali chake
 
hongera sana diamond...

itumie fursa hii kukutana na kufanya kazi za muziki na magwiji kama jay z, beyonce, r kelly, akon, lil wayne, ronaldinho gaucho, rihanna, eminem, lady gaga, excel, maino, justin bieber, neymar, katy perry, j. cole, rooney na drogba.

ila usijiunge na freemason!!

:A S 13:
 
Kwanini tuzo za wasanii africa zinatolewa marekani? Na kwanini BET award itolewe marekani na sio africa!?
 
Muda anao wa kutosha huu ni muda wa kupambana na kujifunza lughq kimtindo had mwez wa saba akikaza atajua hata cha kutungia collabo hahahaa
 
Labda atajifunza akiona kuwa msanii wa kimataifa unakuwaje. Ataacha kuimba kwa play back. Ataona wasanii wanavopiga ala mbalimbali
 
hongera sana diamond...

itumie fursa hii kukutana na kufanya kazi za muziki na magwiji kama jay z, beyonce, r kelly, akon, lil wayne, ronaldinho gaucho, rihanna, eminem, lady gaga, excel, maino, justin bieber, neymar, katy perry, j. cole, rooney na drogba.

ila usijiunge na freemason!!

:A S 13:

hao ni magwiji wa muziki?
 
Be positive meeen , roho mbaya itakutoa nyongo uzeeke haraka

Tukubaliane kutokukubaliana inatoooosha

sijaisema kwa ubaya...ni kutoa tu ucheshi flani....
Hilo jambo la kawaida kwa watu maarufu kufanyiwa utani....bigs up Platinumz
 
hongera sana diamond...

itumie fursa hii kukutana na kufanya kazi za muziki na magwiji kama jay z, beyonce, r kelly, akon, lil wayne, ronaldinho gaucho, rihanna, eminem, lady gaga, excel, maino, justin bieber, neymar, katy perry, j. cole, rooney na drogba.

ila usijiunge na freemason!!

:A S 13:

ha ha ha ha tisha mkuu.
 
Back
Top Bottom