Diamond kuwa msanii wa kwanza kuumizwa na siasa

Diamond kuwa msanii wa kwanza kuumizwa na siasa

Chakaza

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2007
Posts
40,455
Reaction score
73,145
Msanii Diamond ni mmoja wa wasanii vijana waliopata umaarufu kwa juhudi zake na support ya washabiki wake hasa vijana wenzie katika siku hizi za karibuni.

Kwa sasa amependekezwa kuwania tuzo za MTV EMA na ameomba support ya kura ili kupata ushindi.

Lakini response ya safari hii ni tofauti kabisa na huko nyuma hasa baada ya kukubali kujiingiza katika kampeni za kisiasa. Watu kadhaa walimuonya kuwa siasa zitamharibia na kumpotezea washabiki lakini alidharau na wapo Waliompa ushauri eti asijali kwani hata US wasanii wanajihusisha ma kampeni utadhani kampeni zinafanana.

Ukisoma mitandao inaonyesha kuwa wengi hawatamsapoti kwa kura safari hii na kumganya kuwa msanii wa kwanza kiazibiwa na siasa. Wasanii wajifunze kuwa uchaguzi ni kila baada ya miaka 5 ila maisha ya kazi zao ni kila siku.

Mbaya ni kuwa aliamua kulitetea kundi linalowakandamiza wapiga kura wake.
 
Sio yeye peke yake nakumbuka enzi za maro. Hivi huyu maro kampeni za 2010 zilimtupa wap?
 
yani mnanipaje raha,ushabiki hadi akili ni zakijani,roma anaomba kura za tuzo gani? Fact ni kuwa shabiki wa diamond aliye chadema hawez vote kw diamond.
 
Khaa!! Unajua Dangote anapata wapi mshiko wake au unaandika tu? Unajua naye ni mpigakura na ana utashi wake? Acha ujinga bana!

Kwanini asiwe PROF J,NEY WA MITEGO,ROMA na KALA JEREMIAH!!Hivi nyie chaggadema akili zenu zimesetiwa kufikiri upande mmoja tu kwamba mna uwezo wa kumuamria mtu hatima yake.

Tatizo mnaangalia kila jambo kishabiki. Mada imesema kuwa msanii wa kwanza kuadhibiwa na siasa, hii ni kwa sababu yeye sasa hivi ndiye ameteuliwa kushiriki Tuzo hizo na anahitaji sana kura za washabiki wake hasa walio Tanzania.kesho na kesho kutwa Prof J nk nk yatawakumba nao.
Hizi Tuzo kila unaposhinda zina kuongezea umaarufu kimataifa na hata ndani thamani ya matamasha yako inapanda, sasa kuwashauri vijana wetu kuwa waangalifu na hizi siasa za msimu kuna ubaya gani au ujinga uko wapi hapo?
 
yani mnanipaje raha,ushabiki hadi akili ni zakijani,roma anaomba kura za tuzo gani? Fact ni kuwa shabiki wa diamond aliye chadema hawez vote kw diamond.

Mkuu afadhali umeliona hilo. Kuna wakati hawa jamaa nashindwa hata kuwaelewa wanafikiri kwa kutumia nini, Wanamponza kijana wa watu bure wakati ikifika Nov wanamtosa?
 
Tatizo mnaangalia kila jambo kishabiki. Mada imesema kuwa msanii wa kwanza kuadhibiwa na siasa, hii ni kwa sababu yeye sasa hivi ndiye ameteuliwa kushiriki Tuzo hizo na anahitaji sana kura za washabiki wake hasa walio Tanzania.kesho na kesho kutwa Prof J nk nk yatawakumba nao.
Hizi Tuzo kila unaposhinda zina kuongezea umaarufu kimataifa na hata ndani thamani ya matamasha yako inapanda, sasa kuwashauri vijana wetu kuwa waangalifu na hizi siasa za msimu kuna ubaya gani au ujinga uko wapi hapo?

tatizo unakurupuka saaana

Kipindi cha mtv walikuwa hawampigii wanadema wanampigia DAVIDO NA FLAVOUR hao wote ni wachawi wa maendeleo tu

Sahivi wamekuja na propaganda mpya ya kisiasa huo wote uchawi wa maendeleo ukiwemo wewe

MWAKA JANA ALIKOSA HII TUZO, NA HAKUKUWA NA SIASA ila mwaka huu ikitokea amekosa mtaßema ni siasa hahahahaha ni nin kama sio ichawi wa maendeleo ya mtu!!! afu ndio uniambie unamjua RAISI bora ataetetea maslahi ya wanyonge unamfahamu NO!! na hapo untakuwa imeingiaa chaka tu

JUZI KASHASHINDA TUZO MBILI BILA YA HAO MASSHABIKI MAANDAZI.. AMEPATA NOMINATION INAYOZIDI KUMUONGEZEA ÇV BILA YA HAO MASHABIKI MAANDAZI KUTOA HATA KOTA.... TEGEMEA USHIÑDI BILA YA WACHAWI
 
Kama siasa ingekuwa inauwezo wa kumpandisha mtu au kumzika kisanii, diamond angekuwa amekufa kisanii tokea anapigia kampeni 2010 akiwa na tuzo tatu tu!!! Lakini mpaka leo hajashuka na anazo zaidi ya 35 na sio kama 2010 hakuna watu waliokuwa wanataka mabadiliko walikuwepo sana tu!!

Na kwa staili hiyo roma na nay wa mitego ndio wangekuwa nominated mtvema awards na sio diamond hahahahah au video zao ndio zingekuwa zinachezwa vituo vikubwa lakini holaaaaaaaaaaaaaa hata hawawajui mziki sio siasa na siasa sio mziki hata kama kuna mashabiki watazingua sio wote kati ya mamilioni ulionao
 
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂✌✌✌
 
Back
Top Bottom