Diamond kwepa hili mapema la udini. Fata ushauri wa Vanny Boy

Pemba empire

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2018
Posts
467
Reaction score
1,339
Mdogo una shida sana kwa masuala mawaili 1. Udini 2. Uccm

1.Mdogo wangu diamond unasifika sana na sidhani km utashuka leo wala kesho. Wewe ni celebrity unapendwa na wote wakristo kwa waislamu.
Nakushauri acha kaudini ambapo unako. Chukua ushauri wa Rayvanny jenga na makanisa ili uonekane hauna udini. Unajisifia kujenga misikiti yes ni jambo..but jenga na kanisa basi..Tanzania ni ya wote na fata mfano wa Rais anbaye anachangia both misikiti na makanisa. Na ushauri wa bure mwambie Tale apunguze udini. Wakristo wanakusapoti wewe sidhani km ni vyema ukijisifia kujenga misikiti au ukajifanya wewe ni mwislamu sana.Magufuli ni Rais anajenga kote..celebrity mzuri ni yule ambaye hajihusishi na dini. Rayvanny na Baba levo wameshakushauri jenga na makanisa uonekane hauna udini.

Na Tanzania hatuna uhaba wa vyumba vya dini..jenga shule au mahabara..au hospitali.
2.Uccm

Hivi ile shoo ya juzi kigoma umeona jinsi ulivyokuwa kituko..mambo ya kualika wakina pole pole ..mkaanza kupiga nayowe ccm oyee..watu wamekuja kuangalia shoo unaleta mambo ya kujipendekeza sijui ccm oyee..mara ccm itashinda asilimia 100. Dogo fanya mziki siasa huwezi na acha kuwa praise team wa ccm wewe siyo afisa chama au ikulu..muulize marlaw. We unadhani ccm wanakupenda wewe as Nasibu au Diamond. Licha ya kuwa wewe ni mbunifu sana kwenye mziki kuliko Alikiba..but Alikiba hana shobo z kishamba km wewe..huwezi ona Alikiba anakuwa praise team au mwimba mapambio km wewe.
Umepewa soko la jioni pale kigoma kabsa baba levo ulitakiwa kulikarabati kidogo tu na soko lingeandikwa jina lako ila kwakua aliyekupa soko na idea si ccm ukaona hutopata Kiki. Hivi unajua kwann wasanii wenzako wanakuzimia Data?

Mm siyo ccm na siwezi kumsupport msanii ambaye najua ni icon ya taifa analeta uccm kwenye kazi yake. Wakati mwingine shule inasaidia hata kidogo we unadhani tunaokesha angalia miziki yako ni ccm tu. Angalia wenzako wakina burna boy hawana umama huu. Leo nenda Us.canada..china..uk..n.k club zao zote wanapiga nyimbo za wananigeria.
 
we jamaa chizi nini ?

Diamond ni muislamu, akijenga msikiti wewe kama mkristo inakuuma nini ?

Kwani wewe unamshabikia Diamond au Naseeb Abdul?

Haya maneno ulipaswa uwaambie kina Ay, Ney wa mitego , Roma na wasanii wakristo wengine wakajenge nyumba za ibada kwa wakristo sio kulazimisha au kupangia watu ambao wameamua kusaidia imani zao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo Diamond anauwezo wa kujenga kanisa?labda Jengo la Sunday School...

Pia sidhani kama ni sahihi kwa Diamond kuukabidhi huo msikiti wakati usiku wa kuamkia hiyo siku alikuwa kwenye mibalaaa ya kibao kata na bunyero bunyero. Clear lack of respect na njaa ya hap waislamu walioupokea
 
Binadamu ni washahuri wazuri wa maisha ya wengine
 
Dini yao inaruhusu wasaniikujenga misikiti ila sio sis wakristo
Nani & wapi kasema uislamu unaruhsu kujenga nyumba za ibada kwa pesa isiyo kuwa ya halali? Kama unatoa fatua toa ktk dini yako,ila kwa dini usiyo ijuwa undani wake ni bora ukae kimya ,kuliko kuandika pumba.

Kama wamejenga,wamejenga hakuna m2 atakaye wazuia ila kiuhalisia masheikh walio kubal nyumba ile ya Mungu kujengwa ,kwa pesa ya music wamefanya kosa .hakika watakwenda kujibu mbele ya Allah.

KWA SBBU UMEJENGWA ,SII KOSA KUFANYA IBADA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…