Diamond laana hiyo!

Diamond laana hiyo!

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Wakati akimpa mama yake, Sanura Kassim ' Sandra ' gari la Sh . milioni 38 huku akitawanya mamilioni ya fedha kwenye matukio mbalimbali , staa wa Bongo Fleva , Nasibu Abdul ' Diamond Platnumz ' anadaiwa kunyemelewa na laana kufuatia baba yake , Abdul Jumaa kuugua na kuvimba miguu bila msaada wowote .

Kwa mujibu wa chanzo makini cha Ijumaa , baba wa staa huyo anayeishi Magomeni - Kagera jijini Dar , amekuwa akisumbuliwa na tatizo la kuvimba miguu na hakuna msaada wowote anaoupata kwani chanzo cha mapato anachokitegemea ni kodi tu ya nyumba ambayo anaipata kutoka kwa wapangaji wachache alionao.

"Yaani tunashangaa kusikia Diamond ana fedha nyingi , juzikati tuliona katika gazeti kamnunulia mama yake gari la milioni 38 ( Toyota Lexus - Harrier ) sasa kwa nini asimthamini baba yake hata kidogo? "Ukweli ni kwamba baba Diamond anasumbuliwa na tatizo la miguu kuvimba. "Amekuwa akilalamika mara kwa mara lakini Diamond hatujawahi kumuona , " kilinyetisha chanzo hicho na kuongeza : "Juzikati hapa baba Diamond alishikika kwelikweli miguu , akaugulia mwenyewe ndani pasipo kuwa na msaada wowote tena nasikia mzee huyo hataki hata kuongelea lolote kuhusu Diamond maana haoni umuhimu wa kufanya hivyo wakati amemsusa muda mrefu sana ."

MATIBABU HAYAZIDI MILIONI
Katika aya nyingine , chanzo hicho kilidai kwamba ugonjwa wa miguu ambao unamsumbua mzazi huyo , gharama za matibabu haziwezi kufikia hata shilingi milioni moja za madafu achilia mbali mamilioni anayoyatapanya staa huyo. "Ingekuwa tatizo kubwa sana, hapo sawa , kwa sababu miguu huwa inamvimba lakini akipata dawa za kutumia huwa inarudi katika hali ya kawaida , kwa nini lakini anamfanyia hivyo baba yake ? Amemkosea nini?" Kilihoji chanzo hicho.


UTAJIRI WAKE WAANIKWA
Wakati chanzo hicho kikiweka nukta hapo kwa muda , mapaparazi wetu walipewa malalamiko mengine kutoka kwa jirani mmoja wa baba Diamond ambaye alimsihi amsaidie mzazi wake kwani anaamini uwezo anao kupitia kumbukumbu ambazo Diamond mwenyewe alizithibitisha kupitia vipindi mbalimbali vya runingani kama Take One na Spora Show vya CloudsTV .

Pia kwenye vyombo vingine vya habari zikiwemo redio na magazeti pendwa ya Global Publishers . Jirani huyo alidai kwamba mwaka jana Diamond alitangaza kuwa ana utajiri wa Sh . bilioni moja ikiaminika kwamba mwaka huu umeongezeka mara dufu.

"Nakumbuka mwaka jana kupitia Kipindi cha Spora Show na kile cha Take One , Diamond alikiri kuwa ana mkwanja usiopungua bilioni moja, hiyo ilikuwa kwa mwaka jana, sasa mwaka huu unadhani atakuwa na shilingi ngapi? Aache hizo bwana , amsaidie baba yake hata kwa kumpa mtaji mdogo wa biashara ambao unaweza kumsaidia, " alisema jirani huyo.
 
Amtibu babake ajui bila yy kutoa mbegu yake leo asingekuwepo.. ivi na huyo mama si aongee na mwanae
 
Nikweli baba yake Abdul mgonjwa ila ngoswe mwachie ngoswe

Upo jiran nae nini mkuu? Nataka nimfuate nifanye nae bonge la collabo ,atatoka tu na sisi tutakuwa juu, mi ntakuwa manager wake
 
watu hawajui mamake alihangaika vipi na mtoto ..baba mtu si alimbwaga mtoto akihisi anapunguza najukumu...sasa atulie tu sio kupiga kulele hasaidiwi wakati yeye hakusaidia
 
Dunia ni mapito asamehe tu mana ni mzazi no one is perfect with exception God awe makini
 
Msamaha uhusike hapa! Jaman dimondo muhurumie baba ako! Japokua kuna mengi alikufanyia ukiwa mdogo...!
 
Mzazi ni mzazi tu daimond jipange

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Hawa wasanii shida sana. Kanumba nae alikuwa hivi hivi na baba yake.!!!


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Iwe funzo kwa wanaume wote...
Mkishakojoa shahawa mnasepa

Wengine mimba wanazikataa

Mtoto akifanikiwa unaenda mikono nyuma mie baba yako.mie baba yako...

Baba ni zaidi ya kukojoa....


Mwisho wa siku mtoto hana uchungu na wewe

Hawezi kushtuka

Unaishia kulalama
 
acheni ujinga..
abdul atabaki kuw baba diamond hata kama alimfanya nini..

mtu akishakuwa mzazi n mzazi tu milele hata akukosee nini,kama alikasirishwa sana na alichofanyiwa na huyo babake basi asijiite NASIBU ABDUL atafte mzazi mwngne wa kiume..

alafu kwa yeyote aliyeeishi na mwanamke(kuoa) n lazima atamuonea baba diamond huruma,hakuna watu wasumbufu kama wanawake,huwez jua alimkera nini hadi kumkimbia..
 
Wa kulalamikiwa hapa ni serikali ya CCM kwa kutoboresha huduma za afya. Lakini kulalamikia watu eti wanakunywa bia huku wengine wakiugua hilo linakuwa zengwe.
Anyway, ukiona hivyo huyo sio baba yeke.
 
jamani haya maswala msimlaumu sana Diamond kama baba alimkataa na unaweza kuta alitoa maneno mengi mabaya juu ya mama yake au mtoto mwenyewe
Hivi mliona ile news ya mtoto alyemshoot baba yake ,Kuna mambo mengi sana yanachangia mambo haya ,Sisi wote ni wanadamu na kuna room ya kusamehe ni hekima itumike katika sakata hili,na kuomba mwenyezi mungu kuingilia kati
 
ila tuseme tu huyo baba angekua bakresa domo c angeungana na dada yake kuwaunganisha na angemuimba hata kwenye miziki na udhaifu wake wote?!anakimbia tu majukumu ya kutunza wazee wake wote.ye mwenyewe kazi kubadili vidada c ajabu ashatelekeza pia watoto
 
Back
Top Bottom