Diamond na Ali Kiba mkakati August 21

Diamond na Ali Kiba mkakati August 21

KAFA.cOm

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2013
Posts
1,301
Reaction score
739
Hebu tujaribu kuunganisha hizi dot… kwanza

Agosti 21, vituo viwili vya redio nchini, Clouds Media Group na EFM, vilizindua matamasha yao mawili makubwa watakayoyafanya mwaka huu. FIESTA na MZIKI MNENE!

Hii FIESTA nafikiri inafahamika. Ni miongoni mwa tamasha kubwa nchini linaloandaliwa na Clouds Media. Tamasha kubwa kweli kweli! Wasanii wadogo, wakubwa nchini na wale wakubwa zaidi wa nje ya nchi, hukutana kwenye jukwaa moja kushusha burudani.

Hakika ni msimu wa mavuno kwa wasanii. Na wanavuna kweli kweli! Ukielewa hilo, huitaji kuwa na elimu kubwa kufahamu kuwa Clouds, nao huvuna pia kupitia FIESTA!

Hii MZIKI MNENE, ni mpya. Si kubwa kihivyo, japo tunaweza kuhisi ukubwa wake kutokana na kishindo kilichoonyeshwa na redio ya EFM, hawa waandaji wa hili tamasha. Bila shaka kuna shamba lingine la mavuno linaandaliwa hapa.

Maswali ya kujiuliza..

Ilikuwaje matashamasha haya mawili ya redio kubwa nchini kwa sasa kutangazwa siku moja? Kwanini Agosti 21? Walipangana? Wanataka kufunikana? Au tuamini ni ‘Coincidence’….

Teh teh teh… Usipaniki, gonga kwanza KUNG-FU moja kuweka mwili sawa, kisha tuendelee.

Kuna hii ishu ya pili hapa. Hivi mnafahamu kuwa hii Agosti 21, siku ambayo EFM na Clouds Media waliyazindua matamasha yao, ndio siku ambayo FID Q aliachia wimbo wake wa FRESH REMIX?

Ule wimbo aliomshirikisha Diamond Platinumz, ambapo ndani yake kuna mstari Mfalme huyu wa Madale, akimdisi Mfalme wa Kariakoo, ALI KIBA!!!!?

Naomba niunukuu kwanza huo mstari
“Ukinichukia sikosi hela, hivyo kwangu sio kesi,
Kunikompea na Cinderela, Aaaah haiwezi kuwa fresh,”

Kuna maswali yakujiuliza hapa..

Kwanini Diamond ameamua kumdisi Ali Kiba kipindi hiki? Bifu lao lina miaka zaidi ya mitatu sasa, kwanini Mondi ameichagua Agosti 21, kumpiga dongo KIBA?

Kwanini ameitumia ngoma ya FID Q? Ni kweli ile biti ya Fresh ilikuwa na ubora wa ajabu kiasi cha kumfanya Diamond aandike mistari na kurekodi fasta kiasi hiko?

Tunamjua Diamond bwana!

Ni mfanyabiashara makini sana wa muziki. Hafanyi mambo yake kwa kukurupuka. Mondi si mtu wa kurekodi ngoma haraka na kukubali iachiwe fasta kiasi hiko? Tena akiwa ameimba ‘mipasho’ mingi namna ile halafu akubali itoke OFFICIAL na logo ya WCB?

Jiulize tena… biti ya FID Q ni ya maajabu kuliko biti zote za Hip Hop zilizopigwa kwenye miaka mitatu ya hivi karibuni?

Swali la kwanini FID Q amekubali Diamond amdisi KIBA kwenye nyimbo yake, lina jibu rahisi sana. ALIWAZA KIKI!!

Si kweli kwamba hajui KIBA ana nyimbo inaitwa CINDERELA, Fid amedanganya. Anafahamu ila aliwaza KIKI. Kwa miaka ya hivi karibuni amekuwa msanii mkubwa asiye na nyimbo kubwa sokoni.

Hii ya kuimba na DIAMOND, ilimfanya ajione mkubwa zaidi kimziki na kuwaangusha wapinzani wake wa Hip Hop, kwenye majukwaa. Hili alilifahamu vyema, ila hili la AGOSTI 21, huenda kweli alikuwa halifahamu. ALISETIWA, AKASETIKA!!!

Tuendelee na doti zetu sasa…
Baada ya disi hiyo, KIBA akamjibu MONDI mitandaoni. Hapakutulia tena, DIAMOND akarudi tena Studio na kuchana tena… Teh teh teh… Tangu lini DIAMOND akapenda malumbano ya namna hii?

Salam SK na umakini wake aliruhusu hili? Babu Tale, Said Fela na RUGE, watu tuliowahi kuambiwa kuwa huwa wanazisikiliza kwanza nyimbo za Mondi na kutoa maoni yao, walifichwa hili? Usinijibu, tuendelee kutiririka zaidi..

Tuseme kuitwa ‘MALKIA WA NGUVU’ kulimuumiza zaidi kuliko zile picha za ZARI AKIWA NA MWANAUME kwenye swimming pool?

Neno hilo la KIBA, limemuumiza kuliko matusi yote aliyowahi kutukanwa maishani mwake? Achana na matusi aliyoyakoga kipindi kile WEMA alipopewa Mimba na IDRIS, hili neno MALKIA WA NGUVU lilimchoma sana?

Tazama. Mara ya pili aliporudi studio. Hakumjibu KIBA PEKEE, safari hii akamchanganya na OMMY DIMPOZ!!

Diamond alikuwa kwenye akili zake KWELI?

Kwanini OMMY DIMPOZ? Jibu lililo mtandaoni eti anaamini ndiye aliyeandika posti ya KIBA, swali lingine, NANI ALIMWAMBIA? Kama yupo, NI NANI HUYO? Huyo aliyesimama KATIKATI YA team Diamond na Team Kiba??

Tuendelee… OMMY DIMPOZ ambaye ni ‘TEAM KIBA’ na pia ni ADUI wa DIAMOND kabla hajawa TEAM KIBA, akainunua kesi. Akatoka nje ya topic.

Unafikiri ilikuwa bahati mbaya OMMY kumtukana DIAMOND? Ni mwehu kiasi hiko? Tusi lile si angeweza kulitoa kipindi kile alipotukanwa na TEAM DIAMOND kwa kuitwa SHOGA!?

Kwanini alitusi wakati huu? ALITAKA KUIBUSTI BIFU ILIYOKUWA IKIENDELEA???? Usinijibu kwa sasa, gonga KONG FUU nyingine tuwe sawa.

Baada ya msuguano ule, siku chache baadae, KIBA akaachia nyimbo.

SEDUCE ME!! Tuliza akili vyema upaelewa hapa!

KIBA alitoa nyimbo IJUMAA MCHANA, Agosti 25. Kama ulifatilia vyema mitandao ya kijamii, kutoka muda ule mpaka kiza kilipoingia, mjadala mkubwa ulikuwa huu, NYIMBO MBOVU au NYIMBO KALI! UONGO?

Tuwe wakweli hapa. Mpaka usiku, upande uliokuwa ukisema NYIMBO MBOVU ulikuwa unaongoza mbele ya wale waliokuwa wakisema NYIMBO KALI. Kweli au sio kweli!!!?

Kwanini diamond aliachia nyimbo usiku ule ule? LABDA kweli alitaka amfunike KIBA baada ya kugundua wananchi hawajaielewa, au LABDA alitoa kwa ajili ya KUIBUSTI nyimbo ya KIBA???

Tazama hili, kituo cha kwanza kuicheza ngoma ya Diamond sekunde baada ya kutoka ni CLOUDS MEDIA, tena katika kipindi cha SHILAWADU, kipindi kinachoongoza kutazamwa na watu wengi kwa sasa?

Kwa mujibu wa QWISSA MZEE MKAVU (atanisamehee kama nimekosea jina lake) alisema LIVE kuwa wameamua kuipiga nyimbo ya Diamond bila kukaguliwa katika kitengo chao maalumu cha kukagua nyimbo pale CLOUDS, kwanini WALIJILIPUA VILE?

Clouds hawa waliopata umaarufu kwa kustopisha kipindi cha MKUU WA MKOA kwa sababu flani flani za ‘kiprofeshno’, ndio hawa waliojivika mabomu ya kucheza nyimbo bila kuikagua?
Imetokea bahati mbaya au ILISHASIKILIZWA KABLA na ILIKUWA KWENYE MPANGO?

SHILAWADU SASA!! Kitu cha kwanza walichokifanya ni kuzishindanisha nyimbo hizi mbili, tena kwa kasi kweli kweli. HAUKUWA MPANGO WA kubusti biashara ya wasanii hawa kwa ajili ya biashara zao za MATAMASHA YAO??

HII NI BIFU PASUA KICHWA KWELI KWELI!!!

Tazama hili tena. Kituo cha kwanza kumfanyia KIBA Exclusive Interview!! Ni EAST AFRICA RADIO. Kile kituo cha redio na TV, kisichopiga nyimbo za DIAMOND.

Jiulize, kwanini KIBA hakuhojiwa na CLOUDS kwanza? Kwanini hakuwahiwa na EFM? Hawajui wasikilizaji wao wanataka nini? Kwanini walijifanya kufunga macho katika hili?

Ni waliwakosa au waliwaacha makusudi ili KUZITUMIA MEDIA nyingine bila kujijua ili KUBUSTI mpango ule ulioanzishwa AGOSTI 21?? Najiuliza tu!!

Katika hili Shikamoo Ruge… Shikamoo Majizo…. Teh teh teh… Nyie ni VIPUSA HASWAAA!!!

Acha tuisubiri FIESTA,
Acha tuusibiri MZIKI MNENE,

Acha tukashindane kuzomea na kurusha chupa jukwaani, huku watu wakivuna PESA WALIZOZITENGENEZA KIMKAKATI AGOSTI 21.

Kudadadeki!!!!
 
Kama mleta mada akinifanyia Summary sita guess anachomaanisha!
 
Umepoteza muda kuandika gazeti lote hilo kama unataka kuuza.
 
Too long bro hata ukiambiwa usome wewe mwenyewe tena hauwezi
 
"......kipindi cha SHILAWADU, kipindi kinachoongoza kutazamwa na watu wengi kwa sasa?" Hapa umeongopa wengine hawaangaliii hiki kipindi
 
"......kipindi cha SHILAWADU, kipindi kinachoongoza kutazamwa na watu wengi kwa sasa?" Hapa umeongopa wengine hawaangaliii hiki kipindi
Amesema wengi mkuu, hajasrma wote. Hata mimi hua sikifuatilii, ila wanaokifuatilia ni wengi
 
Mleta mada ameandika kitu cha maana kwa upana wake.

Ila kama kawaida, ukitaka kumficha kitu mwafrika kiweke kwenye maandishi.
 
Kumfikiria sana mtu mwingine hua naona kama napoteza muda

Hongera mleta mada kwa kukaa na kufikiria hao jamaa.

Hata hii mada pia sijasoma mpaka mwisho.
 
Nmekata tamaa ya kusoma nimeishia katkat, mara utoe matangazo ya kungfu unalipwa nini
 
Tatizo mtu wa kwanza ku comment kwenye thread wengi hufuata huyo,kama manyumbu vile.
Sio poa,kama mtu huwez kusoma yote/au hujasoma kabsa pita Kama vile hujaona kitu sio lazima jina lako lionekane umecomment.
 
Wanaume wa dar mna kaz kweli kweli kutwa nzima kujadili hela wanazoingiza wanaume wenzenu
 
Mda uliotumia kuandika huu uchafu si bora hata ungeutumia kumuomba mungu
 
Back
Top Bottom