Diamond na Mavoko kuja na kazi mpya hivi karibuni

Diamond na Mavoko kuja na kazi mpya hivi karibuni

Mshamba wa kusini

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2015
Posts
2,857
Reaction score
3,593
Mkali wa wimbo ‘Salome’ na mkurugenzi wa WCB, Diamond Platnumz amewataka mashabiki wa muziki kukaa mkao wa kula kwa ajili ya ujio mpya wa Rich Mavoko.

Diamond amesema Rich Mavoko ana nyimbo nyingi ndani huku akidai kuna wimbo unaitwa ‘Sijaona’ ambao WCB nzima imekubali lakini yeye anasea bado anaandaa kali zaidi.

“Mimi mwenyewe nimefanya nyimbo nafikiri mbili na
Richard na muda wowote zinaweza kutoka,” Diamond
alikiambia kipindi cha FNL cha EATV. “Sema Richard ni mtu fulani ambaye anajipanga hivyo kipindi hiki anajipanga akianza kufumuka na mabomu yake ni hatari, maana anajipanga kila wimbo akirekodi anakwambia hii bado, akirekodi nyingine tena anakwambia hii bado yaani naweza kusema Richard ni msanii ambaye ana nyimbo nyingi sana kali,”

Aliongeza, “Kuna wimbo pale unaitwa ‘Sijaona’ WCB nzima wanaikubali lakini yeye anakwambia hii bado, ila akisema hivyo akileta ngoma nyingine inakuwa kali zaidi. Kwa hiyo ni mtu ambaye Mwenyezi Mungu kamjalia kipaji na mwenyewe anakuaga hana papara”
Muimbaji huyo kwa sasa anafanya vizuri kitaifa na kimataifa na wimbo ‘Imebaki Story’.
 
Kichwa kimoja matata sana pale WCB, na huyu jamaa mimi nasema muziki wake bado haujaendana na anachostahili.
 
Ali Kiba na Maprosoo ni nani zaidi?
 
Back
Top Bottom