Diamond na wema sasa mapenzi yao ya kiutu uzima

Diamond na wema sasa mapenzi yao ya kiutu uzima

Ni mapema mno kufanya tathmini. Tusubiri tuone kama watafika mwishoni mwa 2015 wakiwa pamoia hapo ndio mada hii itakuwa na mshiko.
 
Ni baada ya kukubaliana kuishi pamoja kama wapenzi wa muda mrefu ...

[h=2]Diamond: Mkali wa ngoma, pesa na vidosho[/h]
star.gif


tf0502diamond3.jpg

Msanii Diamond. Picha/HISANI Na THOMAS MATIKO
Imepakiwa - Friday, January 24 2014 at 11:17Kwa Mukhtasari
Mwanamuziki Diamond Platinumz ndiye msanii kipenzi cha Afrika Mashariki kwa sasa na bado anatamba kutokana na nyimbo kama vile Mawazo na Number One. Kwa maneno matatu ya Kiingereza unaweza kumtaja kama; 'Hitmaker’, 'Heart Breaker’ na 'Moneymaker’.



DIAMOND Platinumz ndiye msanii kipenzi cha Afrika Mashariki kwa sasa ambaye kwa maneno matatu ya Kiingereza unaweza kumtaja kama; 'Hitmaker’, 'Heart Breaker’ na 'Moneymaker'.

Kwa ufupi ni mwanamuziki mwenye uwezo wa kuachia fataki wakati wowote kutokana na ubunifu mkubwa alionao, mzuri inapokuja katika suala la mauzo na mtundu inapofikia hatua ya kuwabadili vichuna.

Sifa hizo tatu zimemfanya kuwa msanii kichwa kwenye Ukanda huu akitajwa kuwa mwanamuziki ghali katika eneo hili.

Ukweli ulipo ni kwamba umchukie au umkubali, Naseeb Abdul, ni msanii anayeshiriki ligi tofauti kabisa na wengine na wala hana mpinzani kwa wakati huu.

Lakini kama wasemavyo waswahili, safari ndefu huanza kwa hatua moja na licha ya umaarufu pamoja na utajiri mkubwa aliojipatia kwa kipindi kidogo, kuna alikoanzia Diamond Platinumz 'Rais wa wasafi.’



HISTORIA

Fauka ya kuwa ghali kwa huduma zake, Diamond hakosi shoo zaidi ya mbili wiki baada ya nyingine, kwani mapromota kila uchao humpapatikia.

Akianza hakuna aliyemwandama kwani alionekana kuwa mbwa wa kubweka tu, ila sasa anang’ata kiasi cha kuhitaji walinzi wa kutosha kuhakikisha kwamba yupo salama.

Wengi hawafahamu alikochimbukia kijana huyu mzaliwa wa Kigoma, aliye na historia ndefu iliyokumbwa na umaskini wa kuogopesha enzi za utoto na ujana wake.



UTAJIRI

Fataki ya 'Kamwambie’ aliyoifanya 2009 ndiyo iliyomfungulia milango ya rehema na kumwezesha kuwa nyota akiwafukuzia Lady Jay D na Jose Chameleone kwa ukwasi.

Tangu mwisho wa 2011, kwa mujibu wa blogu kadhaa ya Tanzania, akaunti yake ya benki haijawahi kushuka chini ya Ksh5.3 milioni (Tsh100 milioni). Na mali yake kwa ujumla inakadiriwa kuwa yenye thamani ya KSh64 milioni (Tsh1.2 bilioni).

Kutokana na kipato chake kizuri cha muziki, Diamond ameishia kuwa mjasiriamali mzuri akimiliki nyumba kadhaa za kupangisha, maduka ya nguo, vipande vya mashamba na magari makubwa.

Mtaani Tegeta, Dar-es-salaam, msanii huyo anaendelea kujenga jumba lake la kifahari ambalo linakaribia kumalizika na tayari yupo kwenye mchakato wa kujenga hoteli yenye hadhi ya 4-Star.

Aidha ana simu nne za rununu moja ikiwa na laini mbili hivyo basi kumaanisha ana nambari tano za simu. Hivyo wakati mwingi yeye hulazimika kuziweka kwenye milio ya chini kutokana na simu nyingi ambazo hupokea kwa siku.

Kando na hayo, makampuni mengi yanamlipa mamilioni ya pesa ili kutangaza bidhaa zao. Kampuni ya soda, Coca Cola na ile ya huduma za simu nchini Tanzania, Vodacom ni kati ya nembo kubwa zilizoko na mikataba minono naye.



MAISHA YA MUZIKI

Ndiyo kazi yake inayompa riziki na vile vile kumfanya kutoa ajira kwa timu yake kubwa ya zaidi ya watu 12, inayojumulisha madansa wake, msaidizi wa kibinasfi, wapiga picha na wapambaji.

Kila juma Diamond hupata shoo mbili hadi nne ambazo huhakikisha anakusanya ujumla wa zaidi ya KSh2 milioni ndani ya Tanzania hesabu za haraka zikionyesha kuwa kwa shoo moja huwagharimu mapromota Ksh350,000.

Anapoalikwa kutumbuiza nje, malipo yake kwa shoo moja huwa haipungui dola 25,000 (Ksh2 milioni). Miaka miwili iliyopita, alitumbuiza nchini Rwanda kwenye tamasha kubwa la uwanjani na kupokea Ksh10 milioni.

Katika taaluma ya muziki, amerekodi zaidi ya nyimbo 133 na mwanamuziki anayemuhusudu sana ni Usher Raymond wa Marekani.

Baada ya kutumbuiza kwenye ufunguzi wa shindano la Big Brother Africa 2012, wakati huo akitamba na 'Mbagala’, msanii huyo alitangaza ada mpya ya kufanya kazi naye.

Kupitia Facebook yake alisema mwanamuziki yeyote ambaye angetaka kumshirikisha katika wimbo wake, angelazimika kumlipa Ksh265,000 kwa audio na ikiwa ni video, ada hiyo inakuwa maradufu.

“Nimefanya colabo nyingi ila nyimbo hizo huwa hazitokei katika albamu yangu na wala hazininufaishi kwa lolote. Sasa hivi muziki una maana ya biashara na ndio maana najipa thamani hii. Ikiwa wasanii wa mbele wanalipisha kwa collabo kwa nini mimi nisifanye hivyo,” alisema.

Diamond alianza muziki kwa kujaribu kuwa rapa lakini marafikize wakamshauri ajaribu mtindo mwingine kwani huo wa kufoka hakuwa akiumudu.

Nguli huyo humtaja mamake kuwa kigezo cha mafanikio yake kwani aliishi kuandamana naye kwenye tamasha nyingi za kusaka vipaji na talanta na angemsubiri muda wote.

Wimbo wa 'Mawazo’ alimwandikia mwigizaji wa filamu za bongo Jacqueline Wolper aliyewahi kuwa mpenzi wake. Ule wa 'Kamwabie’ na 'Mbagala’ alimtungia mpenziwe kwa jina Sarah, aliyemkataa sababu hakuwa na uwezo. 'Ukimwona’ alimwimbia mchumba wake Wema Sepetu waliyerudiana, baada ya kumsaliti.



MAISHA NA VICHUNA

Pamoja na sifa nzuri za kuwa 'hitmaker’ maisha yake upande wa pili yamekuwa yakiandamwa na kashfa nyingi za kimapenzi kwa tabia yake ya kuwabadilisha wanawake kila anapohisi kufanya hivyo.

Japo aliwahi kudai kuumizwa sana na Wema aliyemtuhumu kwa kutokuwa mwaminifu kwenye uhisiano wao, kisura huyo ambaye ni staa wa filamu za bongo pia aliwahi kudai kulizwa na Diamond kwa maana moja wanafanana inapokuja kwani wanawezwa kutajwa kuwa 'heartbreakers’.

Uhusiano wao umekuwa wa kukosana na kurudiana na hata wakati ambapo walikuwa njia panda, mara kwa mara waliripotiwa kutafutana na kuendelea na usuhuba.

“Mimi na Naseeb tuliachana baada ya yeye kunidanganyia na Jokate (Mwegelo) baada ya mimi kuwafumania wakipigana busu wakati huo tukiishi pamoja. Muda wote nimekuwa naye sikuwahi kumsaliti na nilijichunga sana kwa ajili yake maana nilikuwa nisharidhika naye licha ya ugomvi wetu wa kila mara,” Wema alinukuliwa na gazeti la Mzuka walipotemana mara ya kwanza.

Kwa sasa wawili hao wamerudiana na uhusiano wao ni wa mtu na mchumbake na wala sio mpenzi tena.

Wakati ambapo Diamond anakutana na mtangazaji Jokate, mrembo huyo alikuwa tayari yupo kwenye uhusiano na mwanavikapu wa NBA, Hasheem Thabeet uliodumu kwa miaka miwili na Jokate alikiri kuwa alikuwa akimpenda sana mchezaji huyo.

Hata hivyo kutokana na uhusiano huo wa mbali Jokate akiwa Tanzania na mwenzake Marekani, kichuna huyo alijipata kwenye hali ya upweke na hivyo kumpa nafasi Diamond.

“Ilitokea tu kwani nilikuwa kwenye hali fulani akatumia nafasi au fursa hiyo lakini angenitongoza mwaka huu (2013) nisingemkubali,” gazeti la Ijumaa lilimnukuu Jokate, Oktoba mwaka jana.

Ni uhusiano ambao Diamond alikiri kuwepo katika mojawepo ya mahojiano na Clouds TV, kitu ambacho alionekana kujutia.

Kuachana huko kukawa ndio mwisho wao licha ya mwanamuziki huyo kumnunulia gari la thamini ya Ksh800,000. Ukaribu kati ya Diamond na Wema uliendelea licha ya tofauti zao.

Ni ukaribu ambao kwa kiasi kikubwa uliwaumiza wengi, muhusika mkubwa akiwa mtangazaji Penny Mungilwa ambaye kwake msanii huyo alikuwa mwanaume wa kipekee.

Penny aliishi kusikia uvumi akawa anaupuuzia kutokana na jinsi alivyomwamini Diamond lakini picha za mwanamuziki huyo wakiwa na Wema, Hong Kong zilipovuja, zilivunja moyo wa hidaya huyo ambaye tayari alikuwa kahamia nyumbani kwake.

tmatiko@ke.nationmedia.com
 
Mwanaume anavaa cheni mwanamke anavaa cheni,mwanaume katoboa sikio mwanamke katoboa sikio. Duh!....
 
Hawa bana pamoja na yote wanapendana na wanajuana na wanawezana sn bt wanatuzingua tu

Nway bt freshhh
 
Wema na Diamond ni wazinzi waliokosa haya kwa kuamua kutangaza uzinzi wao hadharani ili dunia nzima ijue kwamba wao ni wazinifu
 
Mh...... mie huwa ninahisi kama hawa huwa wana kamisheni kwenye mauzo ya Shigongo. Sijui kwa nini nitahisi wataliibua tena

pesa kitu kingine kabisa, kila mtu aitafute kwa nguvu zake zote, kijana katakata sasa, from mbagala-ngololo dunia mbili tofauti.
 
Hivi na mitaa hii huwa unatembelea Pasco


Nahisi kama wako pamoja not for true love but for show off tuu, wanapobaki wawili peek yao kunako, ni majanga!, kila mmoja ana yake, mmoja hakolei, mwingine alizoe kila aki.. anaachiwa 1.M!, dogo hana!.

Enzi za ujana wangu, nilikuwa na kuwa MC sana kwenye mashindano ya urembo inluding Miss TZ!, baada ya show, huwa tunawachukua the runners up na the loosers kuwa "console!', sasa sijui ni mimi tuu, kila siku nilikuta hawakoleagi kabisa!, waangalie hivyo hivyo na hivyo vijisura, body na shapes zao nzuri!, ni machoni tuu!. Asa a results kila nikiwaona hawa top beauties, reference yangu inanituma kwenye sifuri!. Dogo hajatulia!, mrembo hatatosheka na kwa kuzingatia mzazi amemfanya bintie ni "cash cow!", huku dogo yuko still attached to "mothers apron strings!" Sijui kama watadumu!.
Wish them all the best!.
Pasco.
 
Last edited by a moderator:
Diamond,wema loading.................................
 
Kuna wanaume wengine hawana kinyaa Kabisa. Diamond is among them. Mimi nikijua kuwa demu huyu keshapitiwa na watu kibao tena wengine ninawafahamu Napata kinyaa kabisa. Maana najua ninao uwezo wa kupata mtu mwingine tena mkali zaidi asiyekuwa na skendo, sasa kwa nini kufanya show-off kwenye mambo ya uhusiano?
 
I think diamond and wema should have a share in global publishers maana bila ya wao magazeti hayauziki.
 
hakuna kitu hapo.tatizo wameona wameshuka wakaona watafute hbr ya kuwapaisha.hv kila mtu akiamua kuonyesha mapenzi na mwenzi wake kutakalika humu jamani?ni utoto tu unawasumbua wakikua wataacha
 
mheshimiwa Masaki ,suala la kujichukulia shria mikononi ni fano mkubwa ambao unaonyesha jinsi gani sheria imeoza nchini,angalia jeshi la police jinsi lilivyokuwa duni hawana communication ya kutosha ,magari na vyombo vingine vya mawasiliano vimeshindikana kupatikana kutoka kwa government hii inachangia sana kwa jeshi hilo kutofanya kazi zake kwa ufanisi zaidi,hapa wa kulaumiwa ni serikali na wla sio hao police kwani kama serikali ikihitaji watu hawa kufanya kazi zao kikamilifu watazifanya.Serkali lazima ifanye investment kubwa sana katika jeshi la usalama wa raia (police)kama walivyoinvest katika jeshi,kama kuna kijinchi kitakachojaribu kutuletea tabu basi9 hapo ndipo mtajionea jinsi gani imewekeza ndani ya jeshi letu,na vivyo hivyo inaweza ikafanyika kwa jeshi la police.Vibaka wote watakapoyeyukia hatutojua.

peace!!!

Sasa wataandikwa tu ata kama hawana jipya? Basi kila siku wangekuwa wanaandika habar na sijui kama wat wangenunua tena magazeti
 
Back
Top Bottom