Diamond Na Wema Sepetu Wafumwa Wakipeana Denda Hadharani Bila Hata Aibu

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
MASUPASTAA ambao ni wachumba (wanasema wenyewe), Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu na Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond', walijikuta wakionesha upendo wao mbele za watu kwa kudendeka barabarani, Amani lilishuhudia.
Ishu hiyo ambayo wapendanao wengi huifanya kwa faragha, ilijiri hivi karibuni maeneo ya Bamaga- Mwenge jijini Dar es Salaam ambapo ni hatua chache kutoka kwenye Ofisi za Global Publishers ambao ni wachapishaji wa Magazeti Pendwa ya Amani, Risasi, Uwazi, Ijumaa, Championi na Ijumaa Wikienda.

ILIVYOKUWA
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo, Wema alikuwa kwenye shughuli zake za kila siku maeneo hayo ambapo alikuwa ameegesha pembeni gari lake la rangi ya pinki aina ya Toyota Lexus Harrier bila kujulikana alikokuwa ameelekea.




DIAMOND AIBUKA PEKE YAKE
Ikadaiwa kuwa, mara Diamond naye alitokea bila kujulikana alikotokea akiwa anaendesha gari lake aina ya Toyota Prado na kuegesha gari lake jirani na alipoegesha Wema.

SIMU YAPIGWA CHUMBA CHA HABARI GLOBAL

Mapaparazi wa Global wakiwa katika kazi za kila siku ndani ya ofisi, simu ilipigwa kwa mmoja wao na kutonywa kuhusu wawili hao kuwepo eneo hilo kimahabamahaba.





"Jamani Global hapa jirani na ofisi zenu Diamond amekuja sasa hivi, lakini inaonekana amemfuata Wema maana Wema alishakuwepo muda mrefu uliopita, njooni mchukue picha si ndiyo zenu au bado mna bifu na Wema tangu siku ile alipokuja kuwafanyia fujo?"

PAPARAZI AWAFIKIA
Haraka sana paparazi mmoja alibeba kamera yenye uwezo wa kupiga picha kwa umbali wa mita hata 250 bila mhusika kushtukia na kutoka nayo.

Kweli, lilikuwa tukio lilionesha kushangaza kwani paparazi alikuta wapita njia wakiwa wanapunguza mwendo ili kuwashuhudia wawili hao walichokuwa wakikusudia kukifanya bila kuogopa watu.



WEMA NJE, DIAMOND NDANI
Kamera ya paparazi wetu iliweza kuwanasa wawili hao, Wema yeye alisimama nje ya gari la Diamond upande wa dirisha la dereva na kuongea na mwandani wake huyo jambo ambalo hakuna mpita njia aliyeonekana kushangaa.

Hata hivyo, mshangao ulianza pale Diamond alipotoa mkono nje na kumshika kiuno Wema huku wakiendelea kuongea ndipo baadhi ya wapita njia nao walipokoleza macho kodo, wengine wakihoji kama aliyesimama nje ya gari ni Wema, nani alikuwa ndani ya gari hilo!
Haikuwa rahisi kupata majibu kwani wengi walikuwa wanashindwa kumwona Diamond. Wengine waliamini kwamba, Wema alikuwa ameshikwa kiuno na mwanaume mwingine ambaye huena akampindua Diamond kama na yeye alivyompindua yule kigogo wa ikulu ‘CK'.

"Sasa mbona Wema anakubali kushikwa kiuno hivihivi tu, haoni watu?" alihoji mpita njia mmoja ambaye alijitambulisha kwa jina la Salome, mwanafunzi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama jijini Dar.

DENDA NJE NJE
Katika hali isiyotarajiwa, baada ya kushikwa kiuno, Wema alikwenda mbali zaidi pale alipomwinamia ‘baby' wake huyo na kula naye denda ambapo naye mwanaume hakufanya ajizi hata kidogo.

"He! Jamani! Naona wenzetu leo wameamua, hata barabarani? Huu ustaa nahisi unawafanya watu wawe vichaa mbele za watu. Mimi siwezi kabisa kudendeka mbele za watu," alisema mrembo mmoja ambaye hakutaka kutaja jina lake lakini naye ni denti wa Chuo cha Ustawi wa Jamii ambacho kipo jirani kabisa na eneo la tukio.

DIAMOND ACHOMOKA KWA KASI
Baada ya denda hilo lililodumu kwa dakika moja, Diamond alimuaga Wema na kukanyaga mafuta kuondoka katika eneo hilo huku wananachi wakimfuatilia kwa macho yaliyojaa mshangao.
 
Kweli kuwa good marketer ni inborn character... Sio vya kusomea darasani
 
huu usupa star umezd ndo nini kudendeka mbele za watu na kuwafaidisha
 
Two hearts beats together as one.
 
Jamaa wanajua sana kuhusu marketing strategy maana walijisogeza eneo la washirika wao kibiashara GPL hapo wamefanya yao ndugu zangu wa Mtwara lazima wajae kuwaona kesho maana stunt created ili show ya kesho iwe poa.,twenzetu ukiona fursa.
 
Vyombo vya habari bongo havina kazi kabisa.
 
Wacha movie iendelee

Hii ni series bwana, tuko season ya tatu!! season 1 ni Wema na Domo, Season 2 ni Domo na Penny na Season 3 ni Wema na Domo baada ya kurudiana, so bado inaendelea
 
Wema sepetu Miguu hana kabisa aisee !

Kanyimwa sura mpaka miguu !



 
kawaida ila ni ulimbukeni tu

Kupigana picha kama ivyo ktk ilo tukio na kulifurahia ndio ulimbukeni, but kumpa Kiss la nguvu unayempenda hata kama adharani si ulimbukeni, kwa watoto wa uswazi kwenye majungu wataongea saaanaaa, ila wanaojielewa ni kawaida!
 
Ku maintain umaarufu ni shidaaa!!!
 
Uwepo wa wasomaji wa taarifa fake kama hizo,ndio unaowapa nguvu za kutengeneza taarifa fake.
 
duuh hilo ---- la wema ka furushi....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…