Diamond ni Balozi mzuri, asemehewe

Mkuu Mondi hapendi kuwa fursa ila anataka fursa,

Kusema kuwa enzi za kampeni alikosea kujichanganya pesa aziache kisa ni mambo ya siiasa?

Hakunaga kitu cha ivo ata km ungekuwa ni wewe hapo fursa ya pesa lazima uifate ila usiasa haupo mfano mzuri tu kina lady jay dee na misimamo yao amefikia wapi sasa.

Mjini ni fursa sio uwe fursa.
 
Hahahaaah!
Kwani Wizkid kashinda?
Aya Nakamura je?
Na wale wengine wameshinda?
Au nao walifanyiwa petition uchwara za huko twita na kina vigogo wa huko kwao?

Labda sifatiliagi mambo vizuri, Wizkid ashawahi ungana na Buhari wanayemwona kwao km useless prezidaa? Je hakukemea sars?
Sasa kwanini hajashinda?
Vp na hao wengine nao walijiingiza kwny siasa za nchi zao?

Ujinga huu unaonesha ni namna gan una upeo mdogo wa kufikiria... Leta hoja za msingi za kumshauri na sio eti awaombe msamaha hawa wapiga kelele wa mtandaoni, ambao kwa namna moja ama nyingine hakujaathiri chochote katika kukosa kwake tuzo au kazi yake ya sanaa (rejea ile petition uchwara)

Hana sababu ya kumuomba yeyote msamaha zaidi ya kuwashukuru watu waliokuwa bega kwa bega na yeye kwa sababu katika category ile sio yeye pekee ndo kakosa, Kuna wengine 6 nao wamekosa ambao kwa namna moja ama nyingine ni bora zaidi yake

Acha mihemko na unafiki bro hahahaaah!
 

Aombe radhi kwa kosa gani tena jamani!? Sadala endelea kukaza, kila mtu apambane na hali yake.
 
Kuna kitu unashindwa kuelewa hakuna mtu ambaye hajui diamond alichokifanya kwenye tasnia ya muziki amefanya makubwa sana

Lakin suala la Roma kutekwa, mke wake kuangaika mpaka kwenda mortuary, mda huo huo msanii mkubwa Tanzaniakuja kutoa nyimbo ya Bora ukae kimya Bora hata asingeitoa Ile nyimbo akakaa kimya

Na diamond kama angekua mzungu au mstaarabu angeomba radhi kwa Roma na familia yake, Ila hawez kwa sababu busara na hekima hizo Hana
 
Neno samahani Lina nguvu sana ni neno dogo sana lakin inamuiya vigumu kulitamka Ila historia ni hakimu mzuri
 
Acha uongo wiz kid hawajawahi mpigia kampeni mgombea wa urais yeyote

Diamond ana Uhuru wa kumsupport magufuli alikua na uo uhuru, lakin kitendo Cha msanii mwenzake kutoa nyimbo na yeye kwa msisitizo akatoa nyimbo ya anakaa kimya lilikua ni kosa kubwa sana haukua uungwana
 
Lakin suala la Roma kutekwa, mke wake kuangaika mpaka kwenda mortuary, mda huo huo msanii mkubwa Tanzaniakuja kutoa nyimbo ya Bora ukae kimya Bora hata asingeitoa Ile nyimbo akakaa kimya [emoji817][emoji736][emoji1548][emoji1545][emoji1545]
 
Mshana Jr upo sahihi kwa mtazamo wako na wengine kwa jicho la tatu. Ila dogo pamoja na kuwa yeye ni tajiri kibongobongo ana dharau sana kwa wanamuziki wenzake na alishawahi kutoa kauli kuwa wote wajipange wafanye show pamoja alafu yeye atawakalisha, hiyo ni dharau kubwa kwa upande wa medani za kimuziki. Pili ni kuwa anatakiwa abadili management yake maana hao mameneja wake wote wameshapitwa na wakati wanashindwa kumshauri vzr kimataifa ni wakati sasa wa kupata meneja atakayemwakilisha kimataifa.

Tatu aweze kusapoti muziki wa watanzania wenzake mana naona kila wanamuziki wenzake washindani wake wakitoa nyimbo badala ya kuwasapoti na yeye anakimbilia kutoa nyimbo na kwa kuwa ana access na media basi anajitahidi kuwashusha wenzake ili atrend yeye tu hilo ni kosa kubwa. Nne anapenda sifa kuliko chochote wakati watanzania wengi wanaomsapoti ni maskini kwa kiwango kikubwa sasa anapojibrand kila akinunua magari au majumba watu wengi hawapendi na wanakuwa na chuki kubwa moyoni aige mfano wa kina Bahresa hawapendi show off na wana pesa nyingi tu. Ni hitimishe dogo kazingua sana kmmk inabidi aombe radhi pia abadilike.
 
Nimetimiza wajibu wangu kumtetea.. Hayo mazonge mengine apambane nayo mwenyewe.. Kama kawafanyia wengine usnitch sina kikao cha kumkingia kifua
 
Mnavyosema ana dharau kisa alisema wakusanyike wasanii wote na ye awe pekeake anawakalisha mnajua haya mameno aliyasema kipindi gani? Hii kauli aliitoa kipindi media zote zimemsusa hazipigi nyimbo zake wala kumpa support yoyote. yaani wakusanyike hao wasanii wanaopewa saupport na yeye ambaye hapewi na bado atawakalisha. Na tangia hapo dogo kapambana pekeake hadi kawakalisha hadi wenye Media zao[emoji38]. Mbona hamkujitokeza kumtetea? Kama ni chuki au roho mbaya ni nyie wenyewe ndo mlimtengeneza kijana wenu hakuna wa kumlaumu.

Kuhusu kubadilisha mameneja wake, hakuna kubadilisha. Hawa mameneja ndo waliomfikisha hapo alipo. Cha kufanya waongeze ubunifu. Wajifunze kwa wenzao ili msanii wao azidi kupanda.

Eti aombe msamaha, kwa kosa gani labda? Mtu kutamba na mali na mafanikio aliyo jaaliwa na Mwenyezi Mumgu ni kosa? Diamond endelea kutamba baba endelea kuonyesha neema ulizo pewa na Mwenyezi Mungu. Na Mungu ataendelea kukupa hadi wenye wivu wajinyonge..

Na nyie msasubili Diamond ashuke mtasubili sanaaa!.
 
😂😂😂😂 Aige mfano wa bakhresa!!!!
We jamaa bna bakhera yeye ni mfanyabiashara 100%, si ajabu hata sura yake huijui ndivo alivyo. Diamond ni msanii anajulikana kila pembe hapa bongo ivi kweli aishi kama Bakhresa asiejulikana hata sura yake inawezekana kweliii????

Halafu mashabiki wanatamani waone mziki unamfanyia kitu msanii wao, na sio diamond tu mbona kina marioo, harminize nao wanaonesha sana mafanikio yao.

Na hiyo kuwasupport wasanii wenzie ni katika nyanja ipi mkuu, kuna msanii ambe nyimbo yake haipigwi wasafi?? Au unaongelea kuhusu kupost instagram?? Atapost za wangapi sasa, mambo mengine yanahitaji ufikiri kidogo tu.

Na ishu ya kumlaumu kwa kutoa nyimbo baada ya kiba kutoa mbona ni kawaida sana na si yeye tu alietoa nyimbo hata harmonize katoa pia. Na hawa wasanii mara nyingi wanatoa nyimbo zao kwa ratiba, sasa ulipanga nyimbo yako utoe leo eti usitoe kisa flani katoa ilhali unajua ngoma yako ni kali. Acheni chuki za ajabu aisee.
 
Izo tuzo ni mara kadhaa kazikosa, sidhani kama kua upande wa kayafa ndio sababu ya yeye kukosa tuzo. Hao washiriki wengine kama Wizkid ni wakubwa zaidi yake, ingekua ni bahati ya yeye kushinda japo ingeweza kutokea.

Hana haja ya kuomba radhi, hana kosa alilofanya keshashukuru waliomsaidia inatosha.

Ila tu kwa chuki iliyoonyeshwa na mashabiki zake waliokua upande tofauti na chama chake , inampasa kuchukua hatua kuhusu kujihusisha kwake kwenye siasa.
 
Bakhresa hayuko kwenye showbiz hivyo mfano wako hauna uhalisia.
Kusema atawakalisha wanamuziki wenzake ni majigambo ya kawaida kwenye ushindani wao, kumdhihirishia walitakiwa wamshinde kwa vitendo ili maneno yake yaonekane ni pumba.

Abadili management? Are you serious? Hakuna management team inayoweza mikiki mikiki ya music industry ya Bongo kama ya kwake, hapo labda aongeze manager labda kutoka USA kwa ajili ya mitifuano ya kimataifa. Kibongobongo hakuna msanii wa Bongo flavor anayeweza kupambana naye na sababu kubwa ni timu yake ya managers.

Kuhusu kuwabania wanamuziki kwa kutumia media yake that's a very cheap excuse, tokea akibaniwa na media kubwa na influential kwenye tasnia ya muziki alikuwa akiwapiga bao wengine wote ilhali walikuwa wakibebwa, kuna media kongwe na popular bado zinatoa support kwa artists wengine zaidi ya zinavyotoa kwake hivyo hana ubavu wa kumbania yoyote hata kama anataka.

Alipaa sana kwa kutumia social networks na You Tube na bado hiyo ni silaha kubwa sana kwake pia hana milki nayo hivyo hata huko hawezi kumbania mtu.
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
 
Mkuu KIBRI hakimsaidii huyo. Aombe radhi hadharani ili Watanzania wamsamehe vinginevyo atapata tabu sana. Watanzania ni wepesi sana wa kusamehe. Kama haoni makosa yake basi aendelee kushupaza shingo. Wahenga walisema mkaidi hafaidi hadi siku ya ……….

Natambua wazi alijiharibia pakubwa alipojiunga na KAYAFA kupitia kazi zake. Na niliwahi kuandika uzi kumhusu yeye na Konde boy kwamba kitendo hicho kina athari kisanii huko mbeleni.


DIAMOND IKIKUPENDEZA OMBA RADHI
 
Aombe msamaha kwa kosa gani? Kama ni kufanyia kampeni ccm mbona wasanii wengi tu walifanya? Tena karibia wote. Mbona wao hamwafanyii hivyo? Nandy anafanya nandy festival mbona hamfanyi figisu ili watu wasiende kwenye show yake? Acheni chuki kwa kijana wa tandale bana. Kama ni kweli ebu anzeni kuwawajibisha na wengine sio mnamuandama Diamond pekeake.
 
Huwa simkubali Diamond ila ngoja nimtetee kidogo.
Alisema acha akae kimya kwa maana ipi?
Anakubali kilichompata au anaogopa yatamkuta na yeye?
Asa mtu kusema anakaa kimya anaogopa yatamkuta ni kosa? Yangemkuta ungemsaidia nini wewe hapo? Roma alisaidiwa nini baada ya kutekwa? Iko wazi hakuna alichopata.

Hakukemea mauaji.
Inasikitisha aseee, hata kama muuaji anahisiwa vipi uliwahi kuwepo ushahidi wa wazi kuwa ni fulani kafanya hivi hapaswi kuungwa mkono?
Mfano, Naseeb aikemee serikali kwa kumshoot lissu hadharani, hata hao kina mbowe waliwahi sema hadharani kuwa serikali imemshoot bwana Lissu?
Hakuna aliyewahi sema hadharani waliogopa, asa kwanini mnataka kijana wa watu agomee kupiga kampeni ( hakujipeleka aliitwa) kwa sababu ambazo wapinzani wenyewe wanaziogopa?
Afu eti kupotea kwa Ben saanane.
Nakuhakikishia mimi huyo Diamond haijui hata sura ya Ben saanane inafanana vipi, asa ataanza kuhoji mahali alipo mtu ambaye wala Sura yake haijui?
 
Very powerful. Ikimpendeza aombe msamaha
 
Mpuuzi mkubwa kabisa wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…