Diamond ni mchawi, achaneni naye!

Diamond ni mchawi, achaneni naye!

Nakumbuka nilipokuwa O-level ni wachache waliokuwa na mwandiko mzuri ambao tuliwaomba watusaidie kuandika barua walikuwa wanapiga Division 1.7
 
Ukitaka ufanikiwe, jishushe, acha chuki ambazo haziwezi kukupeleka kokote then kaa pembeni hata kama unajua jambo jifanye hujui utafaidi mengi.

Kiba kiburi na kuvimba kichwa ndicho kinamponza.

Sasa Domo yuko studio anarekodi nyimbo na msanii mkubwa africa ambaye kiba alimvimbia kuwa eti yeye ni mkubwa kuliko Wiz kid kule Kenya
 
Ali anatafuta mafanikio gani makubwa kumzidi wizkid?? Mwenzie kaja kupiga show ana ametoka kwenye show kaunga mpaka bongo aje wasafi.
Ukimsikiliza mzee wa upako utamuelewa kiba mashauzi mengi.
 
Nyimbo za Ali Kiba unaweza kuzikiliza ukiwa umekaa na wakwe zako. Hazina matusi anatumia lugha za staha.

Kwasauti Kiba ni Mfalme wa muziki Tanzania.
Mwache aendelee kutoa hizo nyimbo za kusikiliza na wakweze huku akiendelea kuwa masikini.

Kiufupi tz kizazi kimebadirika mno na diamond anacheza na akili zao na humo ndio unaona najipigia tu mihela
 
Sumbi Sanchez,

Upuuzi mtupu,Ndio ni mchawi wa kutafuta pesa.

Kinachowaumiza kichwa, ni kwmaba imewezekanaje, Mond awapite wote waliomtangulia, Bob Junior, Juma Necha, Lady JayD, Mwanafa, AY, Chege, Prof J, Mr 2, kwamba huyu kijana kutoka uswahilini Tandale imewekanaje akawa na mshiko mkubwa kiasi hiki?

Miaka ya 2000, hakuna aliyekuwa na sauti tamu kama TID, au Dully Sykes! Sasa hivi wapo wapi kwa mshiko!kipindi hicho Mond hayupo,Kiba alikuwepo, kama alikuwa anasauti nzuri,mbona hakuwapita?

Hakuna mwana hiphop mwenyemvuto bongo kama Mr blue!,lakini hamfikii Mond kwa mshiko,
Na nyinyi mkisika wasafi mnamuona Mond tu.

Wasafi ni bonge la chama; kuna watu kibao,mameneja,watu wanaoujua mziki nyuma yake!
Ndio no mchawi,Ila uchawi wake sio wa kupaa na ungo,ni was kusaka mshiko.

Huyo Kiba wenu aliulizwa swali moja tu,mbona uendi kushiriki wasafi festival,akadai na yeye anatafuta mafanikio yake.
Kwahiyo mpaka sasa HV bdo hajapata mafanikio!pamoja na sauti yake unayoisifia.
 
Nyimbo za Ali Kiba unaweza kuzikiliza ukiwa umekaa na wakwe zako. Hazina matusi anatumia lugha za staha.

Kwasauti Kiba ni Mfalme wa muziki Tanzania.
Shemela, Kiba alichemka pale alipotoka kuimba na R Kelly ilibidi fursa ile anyoke nayo... Mwenzie Diamond alipoimba tu na DAVIDO akasema na fursa hadi leo... KIUKWELI KIBA HAMFIKII DIAMOND BANA... Ndo maana wengi wameshindwa kutaja sababu wanaishia KUTAJA UCHAWI... Ndo akili za wapenzi wa KIBA
 
Alikiba naye ni mchawi wa vocals. Sema tatizo yee hapendi show off tu [emoji3][emoji3][emoji3][emoji125][emoji125][emoji125]
 
Mond huwa anazinunuaga views amini hivyo
Diamond ana sauti mbaya. Vocal bwana anazo King Kiba na ana kipaji zaidi cha kutengeneza muziki mzuri kuliko Diamond. Nyimbo za Diamond ni mbaya na hazipendezi masikioni.

Baada ya yeye kutoa ngoma mbovu hapo juzi aliyoiita 'Baba Lao' ambayo haina chochote cha maana kimuziki zaidi ya kelele zisizotoa msisimko wowote Ali Kiba alifuata na ngoma kali mno inayokwenda kwa jina la 'Mshumaa'. Barnabas, Ommy Dimpoz, Aslay na wataalamu wengine wa masauti na muziki kwa ujumla wameusifu na kuupromote sana wimbo wa King Kiba kuwa ni moto wa kuotea mbali.

Lakini mbaka sasa wimbo mbaya wa Diamond umekwenda zaidi YouTube. Upo namba moja kwenye trending na tayari una views zaidi ya 2M wakati hata ngoma kali zaidi 'Uno' ya Harmonize iliyotoka siku zaidi ya nne kabla ya wimbo wa Diamond haujafika idadi hiyo ya views. Oh sorry nilisahau. Hizi views huwa ananunua. Halafu wala sio kigezo cha kupimia mafanikio ya wimbo.

Lakini waliotazama Wasafi Festival waliona namna Diamond alivyoweza kuwapagawisha washabiki waliofurika viwanja vya Posta Kijitonyama kwa kutumia wimbo wake mbaya.

Kiuhalisia hakuna msanii yeyote aliyeamsha shangwe kumzidi yeye ingawa kulikuwa na Wizkid ambaye ana umaarufu mkubwa zaidi.

Sasa Diamond anawezaje kupendwa na washabiki wengi kiasi hiki wakati uwezo wake wa kimuziki ni mdogo mno? Hata yeye mwenyewe aliwahi kusema kuwa wapo wasanii wengi mno, na wengine hata hawajatoka na hawajulikani na wana uwezo wa kuimba kuliko yeye.

Hapa Diamond alifanya vyema sana kukiri kuwa kipaji chake cha muziki ni cha kawaida mno ukilinganisha na watu waliojaliwa sauti na ujuzi wa muziki.

Unapojaribu kufikiri kuhusu hao wenye vipaji zaidi ya Diamond lisikujie jina la Ali Kiba peke yake kwenye kichwa chako kwa sababu unazozijua mwenyewe.

Ali Kiba ana sauti kuliko Diamond. Lakini hana uwezo wa sauti kumzidi Ibra Nation, Beka Ibrozama, Ben Pol n.k.

Hata huko majuu Justin Bieber ni star na anapendwa zaidi kuliko watu wenye uwezo wa sauti na muziki kwa ujumla kumzidi yeye. Kisauti Justin Timberlake, Adam Levine na wakali wengine wako juu zaidi yake lakini sokoni amewaacha mbali mno.

Kwa hiyo ni wazi kuwa sauti pekee haitoshi. Ni lazima uwe mbunifu kwenye muziki na maisha yako nje ya muziki ili uwe na soko zaidi. Zaidi ya hapo unatakiwa kuwa na mbinu mbadala za kuutangaza muziki wako.

Vinginevyo utaishia kusifiwa tu wakati wabunifu wanaendelea kukuacha mbali kwa mafanikio na umaarufu.

Sasa majaribio ya kuwashawishi watu kuwa eti Diamond hajui kuimba na kuna wakali zaidi yake kwenye swala la muziki kwa lengo la kumshusha hayana maana.

Hao wenye vocal na mashairi mazuri watu wanawafahamu lakini macho yote yapo Kwa Diamond na wengine wenye uwezo wa kawaida kimuziki. Wamiliki wa makampuni ya Pepsi, Parimatch, Niceone na wengine wanaomtumia kama balozi wao na kumpatia mpunga wa maana wanajua kuwa nyimbo zake ni mbaya.

Hata Vodacom, Coca-Cola na wengine waliowahi kumpa dili nono miaka ya nyuma nao wanafahamu kuwa Ibra Nation, Barnabas, Ben Pol, Beka Ibrozama, Christian Bella, Ali Kiba, Ommy Dimpoz, Mario, Aslay na wengine wana sauti nzuri zaidi ya Diamond na wana nyimbo nzuri zaidi ya zile zake.

Lakini dili wanampa Diamond kwa sababu ndiye ambaye muziki wake na habari za maisha yake binafsi ni dili kuliko kiumbe chochote Afrika Mashariki na Kati.

Hata wasiompenda Diamond cha ajabu huwa wanampromote mitandaoni. Mara ooh ameiga wimbo wa mtu, mara ngoma yake hii ni mbaya wakati nyimbo mbaya na zinazoibiwa zipo nyingi lakini za kwake huwa zinaongoza kujadiliwa.

Hii yote kwa sababu Diamond ni mchawi. Na uchawi wake ni ubunifu alio nao. Kumchukia Diamond na kutegemea anaweza kushushwa na binadamu ni kujipa maumivu ya kipumbavu.

Mimi nilikataa upumbavu huu miaka mingi mno. Nawasihi na nyinyi pia, achaneni na Diamond. Huyu jamaa ni mchawi.
 
Eric Thomas aliwahi kusema "There is no such thing called talent, there is always hard work and objective"

Kama kijana mwenye ndoto za mafanikio Diamond ana ni inspire sana japo mishe zangu hazipo kwenye mziki but his attitude ya kutoridhika na mafanikio kama wasanii wengine inaongeza motivation kubwa sana kwa vijana wenye vision na njaa ya mafanikio.
 
Nani kakuambia Diamond sio muandishi mzuri wa nyimbo? Refer these songs
1. Ukimwona
2. Moyo wangu
3. Utanipenda
4. Lala salama
5. Number one
6. Kamwambie
7.Mbagala
8. Nataka kulewa
9. Nitampata wapi
10. Marry you
11. Mdogo mdogo
Na nyingine kibao tu, uandishi umetulia kabisa. Na alianza kumfunika Kiba tangu kipindi hicho anaandika ngoma zenye ujumbe, sasa hivi Diamond kubadilika na kuandika hizi ngoma za kuchezeka kama Baba lao haimaanishi kuwa hajui kuandika. Dogo ni mjanja sana, anajua kucheza na soko la muziki wa bongo na ndo maana anafanikiwa.
Lala salama , ntarejea, ukimwona, nataka kulewa, mapenz basi aisee hzo nymbo n dope
 
Point nzuri
Ukitaka kumsaidia mtu afanikiwe mpe mfano wa Alikiba na Diamond.

Alikiba ana sauti nzuri anatunga vizuri ila tatizo lake kubwa na linalofanya asifike alipo Diamond ni tabia ya kujiona mfalme, kujiona yeye anapaswa kukimbiliwa,kujiskia na kuvimba.

Diamond sio muandishi mzuri ila anajua kucheza na akili za watu,anaheshimu mashabiki wake,anawalilia na kuwafanya wajione wanamsaidia,ni mnyenyekevu na anatangaza kazi zake kama vile ni msanii chipukizi. Diamond hana kiburi.

Watanzania wengi wanapenda kunyenyekewa na ukilijua hilo utawapata sana.
 
Wimbo wa "AJE"[emoji443][emoji444]
Hata ukipigwa 2025 hautochuja,,upo vile vile tu
 
Back
Top Bottom