Leak
JF-Expert Member
- Feb 22, 2012
- 52,916
- 43,505
Wasalaam wana jamvi.
Ni wazi kila mtu anajua Diamond ni msanii mkubwa na anaye Fanya vizuri na ana tengeneza pesa nzuri kupitia muziki wake.
Bila shaka kila mmoja wetu anajua Kuwa Diamond ana management ambayo inayo ongozwa na Babu Tale na kusema ukweli mnyonge mnyongeni haki yake mpeni .... Babu Tale amefanikiwa kuwa manage wasanii wengi ikiwemo Diamond.
Kwa kutazama kiwango cha Diamond and hatua aliyo piga hadi sasa pengine ndio tunaanza kuona udhaifu wa Babu Tale, kuna mtu anaweza sema Babu Tale kazidiwa kabisa na kwa Diamond anaonekana amepwaya sana.
Mimi Binafsi nimekuwa nikijiuliza hadi sasa ni kazi ya Babu Tale? Nini kazi ya management ya Diamond?
Kuna Mambo yametokea hivi karibuni yamenifanya nitoe ushauri kwa Diamond kumfukuza kazi Babu Tale au kufumua upya uongozi wake hili uende na matakwa ya kumuziki kitaifa na kimataifa.
Mambo yaliyotokea German Diamond kuchelewa kwenda kwenye show na kutokea asubuhi, Diamond kucheleweshewa malipo haya yote yana takiwa kubebwa na Babu Tale au uongozi wa Diamond.
Washabiki tunategemea Babu Tale au uongozi wa Diamond ndio unajua vyema thamani ya Diamond akiwa ndani au nje ya nchi hivyo wao ndio wana takiwa kusign mikataba yote ya show na malipo ya show za Diamond au Diamond atasign mbele ya uongozi wake tena baada ya kupewa ushauri na kushauriana na manager wake kuhusu Terms za mikataba na malipo.
Ndio maana baada ya kutokea matukio hayo yote ambayo kimsingi yana haribu reputation ya Diamond kwenye baishara yake ya muziki nimeamua kumshauri Diamond kumfukuza kazi Babu Tale kazi au ajitazame upya yeye mwenyewe.
Tukiangalia tukio la mtu anaye daiwa kufanya utapeli kwa kuandaa show na kusema Diamond atakuwepo kumbe si kweli na kupekekea kuzuka vurugu na watu wengi kufikiri Diamond kakimbia show.
Ninacho jiuliza katika hili la mtu kufanya utapeli huko UK halafu uongozi wa Diamond bila kuwa na fununu kuwa kuna mtu huko UK anatangaza show bila kuwa na mawasiliano nao ni wazi Babu Tale na uongozi mzima wa Diamond wamepitwa na wakati na wanaendesha biashara yao ki local kabisa.
Nilitegemea Babu Tale akiwa Manager wa Diamond ana connection ya watu huko UK ambao pengine wanamsaidia kutafuta show na kumpa taarifa kama ana hitajika.
Ni kweli Babu Tale hakujua au kusikia au kupewa taarifa kuna mtu anafanya utapeli huko UK kuwa Diamond atakuwa na show huko?
Kwanini Diamond uendelee kuwa na Manager mzigo kama Babu Tale ambaye hajui kazi yake? Ni nani atakusaidia kulinda reputation yako au thamani yako kama Babu Tale anashindwa? Nini kazi yake? Nakushauri umfukuze kazi kwa uzembe na kutokujua wajibu wake.
Kwa upande mwingine pengine Diamond hatoi nafasi kwa Babu Tale na uongozi kufanya kazi zao labda kwasababu anaona hawana faida kwake maana hata swala la malipo anatakiwa kuwaachia wao wahakikishe pesa ina ingia kulingana na makubaliano sio yeye Kuingia kwenye malumbano na mapromoter utafikiri hana management, na kuna uwezekano Diamond ndio huwa ana ingia kwenye makubaliano ya show bila kuwa shirikisha viongozi wake au anawaambia baadae.
Hivyo ni vyema akawafukuza kazi maana sidhani kama anajua umuhimu wao.
Karibuni wana jamvi.