Mkuu
Ruttashobolwa,
Kwa maoni yangu hakuna haja ya kumfuta kazi Babu Talle bali Diamond anahitaji Manager atakaye-deal na international issues/shows. Tutake tusitake, soko la muziki ndani ya ardhi ya Tanzania ni full fitina... no professionalism. Watu pekee wanaofahamu fitina za muziki ndani ya Tanzania ni Babu Talle na Said Fella... PERIOD! Hivyo basi, Babu Tella na Saidi Fella wanaweza kuendelea kubaki ku-deal na issue za kibongo bongo!
Tunavyozungumzia muziki kwenye international level, hilo ni suala lingine... simfahamu Babu Talle lakini namfahamu vizuri sana Saidi Fella... huyu (Fella) nafahamu hana ubavu wa kumuongoza mtu at international level. Huyu Babu Tella wala haonekani kama yupo tofauti sana na Fella... by the way, Role Model wa BabU Talle ni Saidi Fella.
Kwahiyo, binafsi naona badala ya kumtema moja kwa moja, huyu Tale na Fella wabaki na Domestic Market... or may East African Market lakini wanapotaka kutoka nje ya mipaka ya EAC, lazima hayo masuala yashughurikiwe na mtu mwingine mwenye uelewa.