Diamond ni vyema ukamfukuza kazi Babu Tale au ukatizama upya uongozi wako kwenye Muziki wako maana u

Leak

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2012
Posts
52,916
Reaction score
43,505
Wasalaam wana jamvi.
Ni wazi kila mtu anajua Diamond ni msanii mkubwa na anaye Fanya vizuri na ana tengeneza pesa nzuri kupitia muziki wake.

Bila shaka kila mmoja wetu anajua Kuwa Diamond ana management ambayo inayo ongozwa na Babu Tale na kusema ukweli mnyonge mnyongeni haki yake mpeni .... Babu Tale amefanikiwa kuwa manage wasanii wengi ikiwemo Diamond.

Kwa kutazama kiwango cha Diamond and hatua aliyo piga hadi sasa pengine ndio tunaanza kuona udhaifu wa Babu Tale, kuna mtu anaweza sema Babu Tale kazidiwa kabisa na kwa Diamond anaonekana amepwaya sana.

Mimi Binafsi nimekuwa nikijiuliza hadi sasa ni kazi ya Babu Tale? Nini kazi ya management ya Diamond?

Kuna Mambo yametokea hivi karibuni yamenifanya nitoe ushauri kwa Diamond kumfukuza kazi Babu Tale au kufumua upya uongozi wake hili uende na matakwa ya kumuziki kitaifa na kimataifa.

Mambo yaliyotokea German Diamond kuchelewa kwenda kwenye show na kutokea asubuhi, Diamond kucheleweshewa malipo haya yote yana takiwa kubebwa na Babu Tale au uongozi wa Diamond.

Washabiki tunategemea Babu Tale au uongozi wa Diamond ndio unajua vyema thamani ya Diamond akiwa ndani au nje ya nchi hivyo wao ndio wana takiwa kusign mikataba yote ya show na malipo ya show za Diamond au Diamond atasign mbele ya uongozi wake tena baada ya kupewa ushauri na kushauriana na manager wake kuhusu Terms za mikataba na malipo.

Ndio maana baada ya kutokea matukio hayo yote ambayo kimsingi yana haribu reputation ya Diamond kwenye baishara yake ya muziki nimeamua kumshauri Diamond kumfukuza kazi Babu Tale kazi au ajitazame upya yeye mwenyewe.

Tukiangalia tukio la mtu anaye daiwa kufanya utapeli kwa kuandaa show na kusema Diamond atakuwepo kumbe si kweli na kupekekea kuzuka vurugu na watu wengi kufikiri Diamond kakimbia show.

Ninacho jiuliza katika hili la mtu kufanya utapeli huko UK halafu uongozi wa Diamond bila kuwa na fununu kuwa kuna mtu huko UK anatangaza show bila kuwa na mawasiliano nao ni wazi Babu Tale na uongozi mzima wa Diamond wamepitwa na wakati na wanaendesha biashara yao ki local kabisa.

Nilitegemea Babu Tale akiwa Manager wa Diamond ana connection ya watu huko UK ambao pengine wanamsaidia kutafuta show na kumpa taarifa kama ana hitajika.

Ni kweli Babu Tale hakujua au kusikia au kupewa taarifa kuna mtu anafanya utapeli huko UK kuwa Diamond atakuwa na show huko?

Kwanini Diamond uendelee kuwa na Manager mzigo kama Babu Tale ambaye hajui kazi yake? Ni nani atakusaidia kulinda reputation yako au thamani yako kama Babu Tale anashindwa? Nini kazi yake? Nakushauri umfukuze kazi kwa uzembe na kutokujua wajibu wake.


Kwa upande mwingine pengine Diamond hatoi nafasi kwa Babu Tale na uongozi kufanya kazi zao labda kwasababu anaona hawana faida kwake maana hata swala la malipo anatakiwa kuwaachia wao wahakikishe pesa ina ingia kulingana na makubaliano sio yeye Kuingia kwenye malumbano na mapromoter utafikiri hana management, na kuna uwezekano Diamond ndio huwa ana ingia kwenye makubaliano ya show bila kuwa shirikisha viongozi wake au anawaambia baadae.

Hivyo ni vyema akawafukuza kazi maana sidhani kama anajua umuhimu wao.


Karibuni wana jamvi.
 
Kwani yeye Kama msanii, mbona hata hapa nyumbani bongo Ana chelewa kuja kwenye shoo, au sababu ni ya njee ya nchi ndio inakua na mana? Nilikwenda kwenye show zake 3-5 ya mwisho ilikua ile alo kata hela ya wema alikuja saa6 usiku nikasema Leo ndio mwisho kuja kumuona bishoo huyu .....
 

Mkuu ndio maana nimeandika hayo kulingana na matukio ya hivi karibuni! Swala la yeye kuchelewa kwenye show linaweza sababishwa na yeye au waandaaji wa show lakini hiyo ni kazi ya management kuhakikisha anawai kwenye show hivyo ndio maana nikaomba Babu Tale afukuzwe kazi!

Mimi nimeshawai kuhudhuria show moja ya Diamond lakini hakuchelewa kwenye show... na huu si ushahidi kuwa huwai kwenye show!
 
Mkuu Ruttashobolwa umenena kweli! Kijana nachafuliwa; ile ya Germany nilidhani ingetumiwa kama funzo; haya ya UK tena! Kijana inabidi akae chini na kufanya maamuzi magumu!
 
Last edited by a moderator:
Mimi sjaelewa. Kwan ni kwamba kuna mtu alikuwa anadanganya kuwa domo atapiga show. Au ni kwamba domo alichelewa

Yaah kuna jamaa UK katapeli with kwa kuwadanganya watu Diamond atakuja kumbe sivyo!
Ninacho jiuliza uongozi wa Diamond huko local na hawana connections kiasi cha kwamba Diamond anatumika kutapeli watu bila wao kupata hata fununu?
hawajui hii ina muharibia Diamond? Ndio maana nimemuomba Diamond amfukuze kazi Babu Tale maana ni mzigo sio Manager!
 

Attachments

  • 1411214083804.jpg
    42 KB · Views: 1,961
Mkuu Ruttashobolwa umenena kweli! Kijana nachafuliwa; ile ya Germany nilidhani ingetumiwa kama funzo; haya ya UK tena! Kijana inabidi akae chini na kufanya maamuzi magumu!

Babu Tale na wenzie wameshindwa kummanage Diamond ndio maana yanatokea haya!

Babu Tale yeye anafikiri kuwa manager ni kuongozana na msanii kwenye show na kwenye interview!
Ana sahau kuwa ana jukumu La kulinda jina na thamani ya Diamond kwa mashabiki wake!
Naomba Diamond achukue maamuzi ya kumfukuza kazi!
 
Last edited by a moderator:
Hii Show Diamond alikuwa anaifahamu maana alikuwa akiiPromote hata kwenye ukurasa wake wa IG sema atakuwa ameingizwa Mjini na huu ndo mda wa diamond kubadilisha Menejiment Babu Take pengine anaweza hizi fitina za hapa bongo ila kwa nje nadhani pamemumshinda ni bora akaachia ngazi wapatikane watu watakao msaidia Diamond afike mbali zaidi

Kwenye ile Show ya Ujerumani moja ya Komenti za Babu Tale alisema pamoja na mambo mengine mabaya lakini zile Vurumai Zimemsaidia Diamond kujulikana zaidi sisi tunaweza tukadhani pengine Diamond anahujumiwa na Mapromota kumbe wenzetu wameona ile ndio njia ya Kujitangaza Zaidi/Kutafuta umaarufu wenyewe wanasema wame-make Headline
 

Mamanger asiye na uwezo kupima mazuri na mabaya, pamoja na uzito wake hafai hata kidogo...
 

Diamond anapaswa kumfukuza kazi Babu Tale aina hii ya mamanager hawana tofauti na waganga wa kienyeji!
Wakati Diamond ana lalamika kuhusu vurugu yeye ana shangilia kwa kufikiri inamsaidia Diamond na haya ni mawazo ya mwaka 47!
Ni wazi Babu Tale kapitwa na wakati kabisa!
 
Hana lolotw huyo dom9....

Kwake yeye promo ni promo tu..iwe mbaya au nzuri ni promo

Mpaka anaitangaza show ig.....

Anapanda ndege.......

Anazunguka london

Hajui inabidi amaliziwe malipo???

MMh na alivyokuwa anaipaisha hiyo show, yaliyomkuta maskin had namuonea huruma

Ndo arudi shule akasome, watu washamuona ndomo na manager wake wote mburulaz, manager haeleweki ndomo mwenyewe ndo vile vile vichwa box, sasa 0+0 unategemea upate 100 toka lini? Watupishe apa tushawachoka
 
Hana lolotw huyo dom9....

Kwake yeye promo ni promo tu..iwe mbaya au nzuri ni promo

Mpaka anaitangaza show ig.....

Anapanda ndege.......

Anazunguka london

Hajui inabidi amaliziwe malipo???

Ndio maana nasema kuna tatizo la management hadi watu wanafikia kuita wenzao matapeli lazima kuna tatizo!
Pengine Diamond anafanya kazi zisizo mhusu hadi anafikia huku kuwachukiza mashabiki!
 

Attachments

  • 1411216183069.jpg
    58.1 KB · Views: 378
Marketing strategy ya Babu Tale ina-base kwenye kufanya fitina tu naamini hakujua kama Diamond atatusua mpaka nje ya mipaka ambako yeye kama meneja naamini hakujipanga alidhani wataishia kwenye umaarufu wa ndani,Tale ni mzuri kwenye local market maana music industry yetu inaamini kwenye fitina za kumzima fulani ili wewe utoke.
Shule ni tatizo pia maana kwenye timu yao nadhani wamebebana kimazoe sana kuanzia msanii,meneja,Dj etc naungana na mtoa bandiko kua it's high time now kwa dogo kuajiri watu wenye proffesional zao na exposure,vurugu za Germany Tale akasema kwao zina faida cause zinamtangaza msanii wake duh hapo nikajua kabisa Mkurya kapewa mashairi ya taarabu na hili la UK utawasikia wakiwalaumu waandaji hawawezi kujitathimini wao wenyewe wapi wanakosea.
 

Mkuu warumi ni wazi Diamond alikuwa anaijua hii show lakini kutokana poor management ya Babu Tale sasa hayo ndio yanamkuta haya! Ni wazi alikuwa ana tapeliwa ndio maana kakimbia show!
 
Last edited by a moderator:

Unanikumbushe mambo ya business communication, ila asikwambie mtu kusoma raha bhana.
 

Babu Tale ni tatizo sana na hajui kazi take kabisa ndio maana Diamond ndio anachukua jukumu la kuanza kudai pesa yake wakati Babu Tale ndio alitakiwa kuhakikisha Pesa inalipwa kabla ya show au kulingana na makubaliano!

Babu Tale anaendesha mambo kienyeji na hajui maana ya manager!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…