Diamond Platinum na ALIKIBA wamekutana na kumaliza tofauti zao za muda mrefu

Diamond Platinum na ALIKIBA wamekutana na kumaliza tofauti zao za muda mrefu

Kiba haaminiki kesho akiamka vibaya majini yake yanamtuma kulekule
 
Wamekutana wapi wakati mpaka jana Diamond alikua Canada huko
 
Niliwahi kuandika humu iko siku hawa jamaa watapatana nilitukanwa ..
 
Mmmh.....good strategy. Hii dunia sio lazima kupata kwako wengine wakose. Mnaweza kupata wote na mambo yakaenda "muswano" tu.
 
atakayeshindwa kujua hii ni photoshop nae atakua na matatizo yake
 
Niliwahi kuandika humu iko siku hawa jamaa watapatana nilitukanwa ..
Nina wasisi sana na jinsi mwaliko ulivyotoka kwa mondi na jinsi majibu yalivyojibiwa na kuombwa na kiba kwa kudhamini tamasha jinsi mondi alivyokukari na kuhashitagi bidhaa kadha wa kadha za kwake kwa kuzamiwa na bidhaa moja ya kiba natilia mashaka sana yoote haya.
Ila tusubili muda utatuambia
 
Vi redio na vi tv chonganishi watalala njaa hili beef liliwapa ugali wengi sana
 
Baada ya kuwa katika upinzani wa muda mrefu, hatimaye wasanii nyota nchini Tanzania, Diamond Platinum na ALIKIBA wamekutana na kumaliza tofauti zao za muda mrefu.

Hatua hiyo imepokelewa kwa furaha na mashabiki wa pande zote mbili ambao wengi katika mitandao ya kijamii wamepongeza hatua hiyo.

Hivi karibuni, msanii Abdul Nasib maarufu kama Diamond akizungumza na waandishi wa habari, alimkaribisha mwenzake Alikiba kujumuika naye katika Tamasha La Wasafi 2018 linalotarajiwa kuanza Novemba 24.

Lakini katika kuonesha wawili hao wako tayari kufanya kazi kwa pamoja, Alikiba alijibu kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa amepokea mwaliko huo lakini kutokana na muingiliano wa ratiba yake ya kuzindua bidhaa yao ya Mofaya hataweza kushiriki na badala yake ametangaza kudhamini tamasha hilo kupitia bidhaa hiyo.
View attachment 926187
wp_ss_20181109_0001.png
 
Nina wasisi sana na jinsi mwaliko ulivyotoka kwa mondi na jinsi majibu yalivyojibiwa na kuombwa na kiba kwa kudhamini tamasha jinsi mondi alivyokukari na kuhashitagi bidhaa kadha wa kadha za kwake kwa kuzamiwa na bidhaa moja ya kiba natilia mashaka sana yoote haya.
Ila tusubili muda utatuambia
Kwani alikiba ana bifhaa ngapi?
 
Naona mond na dai wamekutana bifu tupilia kule
 
Back
Top Bottom