Diamond Platinumz ameamua sasa kuuza karanga

Kumbe zilikua zinauzwa mia mbili kwa hyo hiyo mia ndie yake kwa ajili ya kutangaza?
 
Anzisha na wewe kama hujazila mwenyewe, kitu hata kama ni chajinga akianzisha mtu mashuhuri basi lazima kitapata wafuasi sana
 
20*30=200

Kukariri kuna waharibu sana,
Biashara siku zote watu hawapigi hesabu za siku 30 maana biashara haifanyiki kwa siku 30 kuna siku 8 za kutofanya kazi......
Na pia biashara huwezi uza constant ya idadi ya bidhaa husika kuwa kila siku uuze 1000, ndio maana nikasema chukulia mfano kwa siku akipiga 1000 kwa mwezi hawezi kosa 200mil
 
Ukijua namna ya kutumia fursa hutakaa ushinde njaa.. Kwa namna jinsi watu wanavyozidi kushangaa na kutaka kujua zaidi ndiyo namna hiyohiyo wanamuongezea wateja na kupata mtonyo zaidi.. Tumia fursa kijana..
 
Jamaa una wivu sana
 
Never ever be afraid of making a ridicule amount of money
 
safi sana biashara nzuri hii hasa ukizingatia mashabiki wake weingi ni watu wa kawaida.
 
Ajishughulishe...maana nchi ya magu hakuna kupiga dili
 
Kuna shida gani mbona ni jambo la kawaida sana,,,, hapo Diamond kainunua hiyo biashara na brand kwa hiyo hata akiwa anapata 150 basi kwakwe ni faida kubwa sana.... Hakika Diamond ana akili sana... hata kama hizo karanga zilikuwepo toka miaka 10 mtaani lakini ni baishara yake sasa anaifanya kinacho jalisha ni yeye kuingiza Tsh hata kama ni kwa gawio...
 
Diamond ana akili sana, karudia asili yake. Kaona muziki unamkimbia, kusoma alama za nyakati ni muhimu sana katika maisha.
 
Nampa mwaka mmoja atarudi na maji ya kandoro kwa sh 150
 
Kweli kabisa wengi wasichojua hii biashara ina tajirisha haraka sana kuzidi hata zile kubwa..
Diamond kapiga hatua kubwa sana hata kama kainunua hiyo biashara

amepiga bao haswaa,
tena aongeze na vibidhaa vingine vya bei hizo-hizo like crisps nk atauza hadi ataona mziki haulipi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…