maatope
JF-Expert Member
- Sep 19, 2013
- 1,422
- 957
- Shukrani kwa mchumi grade one niliyekuwa nimekaa naye jana kwenye ka pub kamoja kalichozungukwa na maji machafuyaliyoshindwa kupata njia ya kupita kutokana na serikali za mtaa chini ya CCM kupuuza miundo mbinu.
Huku akishushia konyagi na nusu kilo ya kitimoto aliniambia" kijana,Profesa Ndulu alitaja mambo ya Tanesco na kununua mabehewa naye waziri magu aliongelea suala la wahisani kugoma kutoa hela kutokana na wale wazalendo wa ccm walioiba hela za Escrow lakini wamesahau kitu kimoja,Diamond platinumz"
"Huyu kijana kila akienda nje anarudisha nyumbani dola nyingi kama laki mbili na watalii wengi wameongezeka bongo kwa ajili yake,wewe unadhani ni kwanini hadi Rais anamfagilia?unadhani ni kwanini aingie kwenye kitabu cha miaka 51 ya Muungano kina Mbaraka mwinshehe,Moris Nyunyusa waachwe?"
Siku hizi haendi sana nje kwa hiyo dollar zinazoingia nchini zimepungua ndiyo maana shillingi inashuka,aliongeza expert huyo wa uchumi
Mwishowe akanidokeza kwamba yeye ndiye anhusika kumtafutia Diamond na zari,private jet ya dollar million 20 ambayo itatua bongo soon
Adios.