Jannatul Firdaus
JF-Expert Member
- Aug 4, 2026
- 446
- 1,113
Mwanamuziki maarufu wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, ameibua gumzo mtandaoni baada ya kutoa kauli ya utani yenye ushauri mzito kwa wanaume wanaotarajia kumposa binti yake, Sandrah, hapo baadaye.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, Diamond amepokea heri za siku ya kuzaliwa kutoka kwa binti yake huyo, hatua iliyomfanya aandike ujumbe uliowavutia na kuwafurahisha mashabiki wengi.
Katika ujumbe huo, Diamond alieleza changamoto na "hekaheka" anazopitia katika kumlea na kumtunza mtoto wake huyo, huku akionya kwa utani kuwa hatakubali posho au mahari ndogo pindi binti huyo atakapokua.
"Hekaheka unazonipa halaf eti baadae mtu alete mahari Uchwara eti kisa tu Umempenda, utakula Makofi wewe na yeye," aliandika Diamond.
Kauli hiyo imepokelewa kwa hisia tofauti na mashabiki mtandaoni, wengi wao wakichekeshwa na namna msanii huyo anavyoonyesha mapenzi yake na uwajibikaji kama baba anayepambana kwa ajili ya mwanaye.